Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,240
- 44,485
- Thread starter

- #81
mkuu mwanakijiji kuna maswali mazuri ya waberoya ambayo majibu yake yatakuwa elimu tosha na pengine mjadala kutoa changamoto zaidi.

Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?

Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?

Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?

Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?

Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?

Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:

a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.

b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.

Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:

a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.

b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

my two cents plus the other fifty
Wataalam kama Jatropha mpo lakini mnaacha watu kama Maghufuli wanatufanyia mambo kijanja hivo kama akina Kakobe wanavyofanya na Biblia yetu!
Hizo sheria zilipitishwa na vikao halali vya Bunge. Isitoshe ignorance of the law is no excuse... Bila barabara bora hatuwezi kurealize maendeleo lazima tuunge mkono jitihada za Magufuli, watakaoathirika waombe kudra kwa JK walipwe japo fidia kiodogo.
Jamani watanzania tunasifa moja kuu, nayo ni kutosoma na kurukia vitu. Gazeti la Tanzania Daima liliropoti kuwa PM alimwita na kuka na Magufuli mara mbili na kumtaka asitishe bomaa bomoa holela hii kabala hata ya hajaenda katik ziara Kagera. Akakaidi na kutunga msamiati kuwa nimeapa na kumtaja Mungu.Hivi kwa nini kwa wakati mmoja Raisi na PM wanamwandama Magufuli katika utendaji wake tena hadharaniiiii????????????????????????????
we Jatropha inaelekea ni mmoja wa waathirika wa bomoabomoa ndiyo maana unaongea even out of context. Nijuavyo mimi ipo ramani ya jiji zima la Dar, ukiangalia ramani hiyo na hali halisi on the ground ni kichekesho. Yaani watu wamejenga kiholela sana na walifanya hivyo kwa kudanganywa na maafisa ardhi kuwa ramani ingebadilishwa in their favour, hiyo ilikuwa miaka kama 10 au 20 iliyopita, hatua zisipochukuliwa basi daima hatutakuwa na barabara zenye ubora. njia pekee ni kubomoa baadhi ya nyumba ili kupisha ujenzi wa barabara, na hatua hii ni kwa faida ya taifa lote kwa ujumla. As I see it labda muombe fidia kidogo kwa JK.
Magufuli sio kiongozi wa Principle, na hii imejidhihiriasha sasa. Magufuli ni kama robbot unaliprogram halafu linafanya kazi kulingana na ulivyo liprogram, nasema hivyo kwa sababu kila wizara anayoenda anakariri sheria na miongozo yake na kuanza kutekeleza bila kuipa nafasi akili yake kupambanua. Na ndio maana nje ya uongozi hana kitu anachoweza kufanya. Hana principle zake anazozisimamia.
Kwa maelezo uliyoyatoa,he will make a good president pindi tukishabadili katiba...Kwasababu ameonyesha sifa nzuri ya usimamiaji wa sheria,then tubadili katiba halafu kama atasimama kwa sera nzuri,then he will make a good contender for presidency.Good kwa maana ya good for the country.
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?
Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?
Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?
Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?
Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?
Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:
a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.
b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.
Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:
a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.
b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.
my two cents plus the other fifty
Jatropha ndio maana bado kwa kipimo chochote kile Magufuli hana budi kujiuzulu:
a. Kama alikuwa sahihi (kwamba yote uliyoyasema juu yake si kweli) na Rais alimtaka asiendelee namna ile alipaswa kujiuzulu
b. Kama hakuwa sahihi (kama unavyoonesha) na Rais amemuacha anaendelea na kuvuruga wizara hiyo na kutumia madaraka vibay abado alitakiwa kujiuzulu na kama kuna ushahidi mzito kushtakiwa kabisa kwa kutumia madaraka vibaya na kulisababisha taifa hasa.
Mkuu MMKJJ mambo mengi anayoonge Jatropha tumekwisha yaongeea na kuyarudia mara nyingi sana katika threads zilizopita, tatizo ninaloliona mimi humu JF kuna watu wa Magufuri na baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara yake ambao labda walishauriana naye hili swala kisiasa zaidi, na sasa wanapoona kuna wataalam wanaolijua zaidi wanakimbia na hawa jibu hoja yoyote badala yake wanafungua thread mpya, wewe subiri utaona wanakimbia humu katika hii thread kabisa na wataanzisha nyingine, lakini kitu wanachotakiwa kujua ni kuwa Tanzania hivi sasa ina wataalam tena wazuri sana katika kila kona za Dunia hii, pia inaonekana hata hapo Wizarani kwao kuna wataalam wazuri ambao mawazo yao yanapuuzwa kwasababu wao hawapo katika malengo ya Magufuri ya kisiasa, nasema hivi kwasababu ukichambuwa vyema hili swala mi naona dalili ya kuwa Waziri Mkuu alitonywa na wataalam wa Wizara hiyohiyo kuwa huyu jamaa anatengeneza bomu hapa wizarani ebu zueni haraka sana!
We angalia kwa mfano walijenga Jengo la Meneja wa TANROADS kwa gharama za walipa kodi alafu anakuja kulibomoa haraka haraka kwa ajili ya sifa, lakini Mwanakijiji ukae ukijua hii yote ni kuumiza walalahoi na walipa kodi kwasababu ya uzembe wa wachache, kwanini hatujaambiwa sababu ya hasara hiyo na imetugharimu kiasi gani?, maana kama unajenga nyumba ya serikali sehemu amabayo baadae unakuja kubomoa maana yake nini? na sehemu kubwa ya ujenzi uliobomolewa pale ulifanyika Magufuri akiwa Waziri wa wizara hiyo. kwanini watanzania wasiambiwe nini kilitokea mpaka fedha za serikali zikawekezwa sehemu ambayo haiitajiki?, na waliosababisha wamechukuliwa hatua gani? Sisi tunatakushabikia kubebeshwa mzigo ambao sio wa kwetu, maana ki ukweli ubomoaji wa jengo la TANROADS ulipaswa kwenda na hatua za kinidhamu dhidi ya Muhusika aliyeleta hasara hiyo! kwani Tanzania tunashida ya ardhi kiasi cha kuingiza serikali hasara kiasi hicho? kama walijua watabomowa baadae kwanini hawakuweka majengo ya temporary kama mbao, kontena nk. Hii peke yake inatosha kutia shaka juu ya walichokuwa wanafanya maana kama lile eneo ni Right of Way na wao ndio watunzanji wa RoW ilikuwaje wajenge jengo la kudumu ndani ya RoW?! na kwa hasara ya nani?
Mambo ya kitaalam hayapaswi kufanywa kisiasa hata siku moja, watanzania tunataka wanasiasa kutatua matatizo ya kitaalam ndio maana hatuendi mbele badala yake ni kurudi nyuma kila siku.
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?
JIBU: Kwa kumfukuza yule CEO wa TANROADS
Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?
JIBU:L Hapana. CEO wa TANROADS or rather chini ya uongozi wake gharama ya kutengeneza kilometa moja ilipanda hadi ilikofika leo, 1.5billion. Extra hiyo ndo mgawo kwa walomweka madarakani. Wamechukizwa na hilo na consequences, tunaziona
Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?
JIBU: Indirectly Mrema amekula meza moja na waliomweka pale. Mafisadi wenzake.

Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:
a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.
b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mambo ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.
... Not true Sir!!
Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:
a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.
JIBU: Akijiuzulu ni wazi watam-Kolimba! Hakuna ubishi kwamba he is very popular kule kanda ya ziwa. Ni asset kubwa sana. Thanks to his contributions, leo hii unachanja mbuga toka Mwanza all the way to Kampala. Lami tupu. Likewise, hadi Kigoma
b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.
KWELI
my two cents plus the other fifty
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?
Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?
Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?
Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?
Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?
Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:
a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.
b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.
Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:
a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.
b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.
my two cents plus the other fifty
Hawezi simama peke yake bila ya uwaziri kwani hana ujasiri kama wa kina selelii, lembelii na hata akina ole sendeka ktk kusimamia maslahi ya tz ila akipewa rungu(uwaziri) utasikia wavuvi haramu, bomoabomoa, zuia magari ya serikali na mengineyo.
FOR YOUR INFORMATION HAKUNA JENGO LOLOTE LA TANROAD LILILOBOMOLEWA, PALE UBUNGO. ZILIKUWA NI MBINU ZA MAGUFULI KUWATISHA WATU WABOMOE NYUMBA ZAO ILI AJIPATIE SIFA. KILICHOBOMOLEWA NI MAJENGO MAKUU MAKUU YALIYORITHIWA NA TANROAD KUTOKA KWA UJENZI, AMBAYO NAYO ILIYARITHI KUTOKA KWA CONTRACTOR ALIYEIFANYIA BARABARA YA DAR-MLANDIZI UKARABATI MWAKA 2001 ALIYEITWA SCANPHIL KOLAS.
hIVYO HIYO ILIKUWA NI YADI YA CONTRACTOR, HIVYO TANROAD HAIJAWAHI KUJENGA JENGO LOLOTE HAPO UBUNGO. KWA KAWAIDA CONTARACTOR HUCHAGUA MAHALI PAZURI NA KUJENGA YADI KATIKA SITE YAKE. KWA TAARIFA YAKO MARA TU BAADA YA CONTRACTOR KUKABIDHIWA KANDARASI YA BARABARA ENEO LOTE LITAKALOKUWA CHINI YA UJENZI HUITWA BUILDING SITE. HIVYO UKWELI NI KWAMBA CONTARACTOE AITWAYE SCANPHIL KOLAS ALIJENGA YADI YAKE KATIKA SITE ALIYOKUWA AKIFANYA KAZI ZA UJENZI.
BAADA YA KUKAMILISHA KAZI ZA UJENZI, NA SITE HIYO KUFUNGWA. MAJENGO, MAKONTENA NA UZIO VILIVYOKUWA VIKITUMIWA NA CONTRACTOR HUYO VILIRIITHIWA NA MHANDISI WA TANROAD PWANI NA DAR.
HIVYO HAIKUWA SAHIHI KWA MAGUFULI KULIDANGANYA TAIFA KUWA TANROAD IMEJENGA KATIKAHIFADHI YA BARABARA. ALITAKIWA KUSEMA UKWELI KUWA MAJENGO HAYO YALIKUWA NI MALI YA CONTRACTOR SCANPHIL KOLAS.
Utaona kumbe hatumjadili mtu kama mtu bali mtu na kanuni inayomuongoza; ndiyo maana sijasema "Magufuli yukoje?"; swali ni Magufuli bila ya madaraka. Na utaona wachangiaji karibu wote wanachangia - ukiwemo wewe- kwa kuangalia kiongozi aitwaye magufuli akiwa na madaraka au pasi na madaraka. Huku si kumjadili mtu kama mtu.
sn2139 - ndio maana naamini ya haya maswali na uchokozi wangu hapa.. of course tunajua mawaziri wanafanya kazi at the pleasure of the president.. kwa hiyo upande mmoja ni kuwa ili aweze kuendelea kuwa madarakani na kufanya anayotaka hana budi kulamba miguu ya bosi wake. Swali langu ambalo ndio msingi wa hoja (natumaini Waberoya naye ataliona) ni kuwa viongozi hawa wanapotofautiana hivi ni nani ajiuzulu on principle? Swali langu halihusiani na upiganaji n.k linahusu kutawala na kuwabika kama kiongozi pale tofauti za msingi zinapotokea.