Magufuli bila madaraka yukoje?

Magufuli bila madaraka yukoje?

Tuangalie kwa ufupi. Huyu bwana alipoingia bungeni ulikuwa wakati wa Msekwa ambapo bunge lilikuwa mhuri tu na haikuwa rahisi sana kujua wapiganaji kwa uwazi hasa ukiwa ndani ya chama. Halafu akawa waziri jambo lililombana zaidi.

Kurudi kwake bungeni tena bila kupingwa ni ishara ya kuwa wapiga kura wake walikubali kazi yake, na hiyo inamjengea hoja kuwa japo si msemaji ni mtendaji. Kama ni kweli au si kweli wananchi wa Chato wanamajibu sahihi.

J.P Magufuli ni kiongozi ambaye ametuonyesha mengi yaliyowashinda wenzake.mambo. Anaifahamu vizuri kazi yake na yupo tayari kusimamia sheria zetu wenyewe hata kama ni za kurithi kutoka kwa mkoloni.
Kukubalika kwake kunatokana na kufuata kanuni, sheria na mipango. Kwanfano aliposimamia ujenzi wa bara bara, ile ni sehemu ya kutumia na kuendeleza rasilimali za taifa. Alipotuonyesha kuwa tumelala na watu wanavua samaki karibu na kigamboni alisimamia rasilimali za taifa.

J.P.M anaposema ujenzi haramu ndani ya hifadhi za bara bara anasimamia matumizi ya kile kidogo tulicho nacho kwa manufaa yetu sote,kwa kuzingatia sheria tulizozikubali sisi wenyewe na kumkabidhi azisimamie.

Kitendo cha viongozi wa juu kumsema mbele ya mikutano ni ukiukaji wa kanuni za uwajibikaji wa pamoja 'collective responsibility'. Sijui kama PM au Rais wameshindwa kuwasiliana naye faragha hadi kusimanga hadharani.

Viongozi wanajali kura zaidi na si sheria walizoapa kuzisimamia ' cheap popularity'. Utamaduni uliotufikisha mahali wizi, ubadhirifu na ufujaji ni sehemu ya uongozi.

La kushangaza,ni kitendo cha J.P kutojiuzulu. Kanuni za utawala bora zinasema kunapokuwa na tofauti za mitazamo wazi kiongozi anatakiwa ajiuzulu.
Magufuli anaweza kuwa kiongozi mzuri hata kama si msemaji wa wazi kama
mbunge, sijui anasubiri nini na kama anataka kuwa malaika ndani ya kundi la wahalifu.

Kiongozi anayeamini katika kanuni na sheria tunamhitaji katika nchi hii kwa sasa. Nchi yetu haihitaji kiongozi wa kuwafurahisha watu bali mwenye 'discipline, vision, goals and action'.
Dah mkuu umemaliza kila kitu.
 
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?

Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?

Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?

Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?

Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?

Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:

a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.

b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.

Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:

a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.

b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

my two cents plus the other fifty
Njaa mbaya sana, huyu mtu sasa hivi sijui atasema nn baada ya uzi huu.
 
during this time, M.M Mwanakijiji was at the peak of great thinking.

Indeed he who breaks the principle, the principle will find the way to revenge and it will eventually break him as well!
 
Tuangalie kwa ufupi. Huyu bwana alipoingia bungeni ulikuwa wakati wa Msekwa ambapo bunge lilikuwa mhuri tu na haikuwa rahisi sana kujua wapiganaji kwa uwazi hasa ukiwa ndani ya chama. Halafu akawa waziri jambo lililombana zaidi.

Kurudi kwake bungeni tena bila kupingwa ni ishara ya kuwa wapiga kura wake walikubali kazi yake, na hiyo inamjengea hoja kuwa japo si msemaji ni mtendaji. Kama ni kweli au si kweli wananchi wa Chato wanamajibu sahihi.

J.P Magufuli ni kiongozi ambaye ametuonyesha mengi yaliyowashinda wenzake.mambo. Anaifahamu vizuri kazi yake na yupo tayari kusimamia sheria zetu wenyewe hata kama ni za kurithi kutoka kwa mkoloni.
Kukubalika kwake kunatokana na kufuata kanuni, sheria na mipango. Kwanfano aliposimamia ujenzi wa bara bara, ile ni sehemu ya kutumia na kuendeleza rasilimali za taifa. Alipotuonyesha kuwa tumelala na watu wanavua samaki karibu na kigamboni alisimamia rasilimali za taifa.

J.P.M anaposema ujenzi haramu ndani ya hifadhi za bara bara anasimamia matumizi ya kile kidogo tulicho nacho kwa manufaa yetu sote,kwa kuzingatia sheria tulizozikubali sisi wenyewe na kumkabidhi azisimamie.

Kitendo cha viongozi wa juu kumsema mbele ya mikutano ni ukiukaji wa kanuni za uwajibikaji wa pamoja 'collective responsibility'. Sijui kama PM au Rais wameshindwa kuwasiliana naye faragha hadi kusimanga hadharani.

Viongozi wanajali kura zaidi na si sheria walizoapa kuzisimamia ' cheap popularity'. Utamaduni uliotufikisha mahali wizi, ubadhirifu na ufujaji ni sehemu ya uongozi.

La kushangaza,ni kitendo cha J.P kutojiuzulu. Kanuni za utawala bora zinasema kunapokuwa na tofauti za mitazamo wazi kiongozi anatakiwa ajiuzulu.
Magufuli anaweza kuwa kiongozi mzuri hata kama si msemaji wa wazi kama
mbunge, sijui anasubiri nini na kama anataka kuwa malaika ndani ya kundi la wahalifu.

Kiongozi anayeamini katika kanuni na sheria tunamhitaji katika nchi hii kwa sasa. Nchi yetu haihitaji kiongozi wa kuwafurahisha watu bali mwenye 'discipline, vision, goals and action'.
Will you still say the same today?
 
mr gentleman, kabla sijaendelea hii hapa chini ni sehemu ya maandishi ya Mzee Mwanakijiji humu JF tarehe 31/1/2007 akiwa amekipa kichwa cha habari kinachosema, ni lazima kuisifia serikali?

Ni lazima kuisifia serikali?
By Mzee Mwanakijiji
Kwanza, hakuna mahali popote katika Katiba yetu au sheria yetu panapomtaka mtu kuisifia serikali au kuikosoa serikali. Zaidi ya yote hakuna mahali panapomlazimisha mtu anapoikosoa serikali lazima pia aipe sifa. Kama mtu hataki kukupa sifa kwanini umlazimishe? Katiba yetu inapotambua haki ya raia kutoa maoni au mawazo haisemi hata chembe mawazo hayo yawe ya aina gani! Kitendo cha kulazimisha mtu au kikundi cha watu kutoa mawazo yanayoipendeza serikali na yenye kukubalika na serikali ni kitendo kinachopakana na utawala wa kiimla.

Ni nani aliyesema kuwa wananchi wa Tanzania ni lazima wacheze kila siku serikali ikipiga ngoma? Ni nani aliyesema kuwa kuipenda serikali ni lazima? Na ni nani aliyesema ni marufuku kuichukia serikali? Watu wakiipenda serikali wanaichagua kuwaongoza, wakiichukia wanaiondoa kwenye sanduku za kura. Wale wanaoipenda wana haki hiyo na wale wanaoichukia wana haki hiyo hiyo. Wale wananchi wanaoimwagia sifa serikali au viongozi wake wanafanya hivyo kwa haki kabisa, na wale wanaoikosoa na wanaokosoa viongozi wake wana haki hiyo hiyo pia.

Tatizo linakuja pale baadhi ya viongozi wanapofikiri wao ni wana wa mfalme ambao wanaweza kutawala kwa maneno yao na kulazimisha watu kuwasifia! Hilo halina nafasi katikaTanzania na tunapinga kwa nguvu zetu zote hadi pumzi ya mwisho. Tanzania ni nchi huru, na itaendelea kuwa huru, hatumtumikii mfalme au wana wa mfalme, mapenzi yetu ni kwa jamhuri yetu na utii wetu wa kwanza ni kwa Katiba yetu. Aneyehoji uzalendo wa watu kwa vile mawazo yao hayaendani na yale ya serikali au kwa vile wanaikosoa serikali amefilisika kifikra na siasa haziwezi, bora aachie ngazi.

Katika utawala wa demokrasia (kama tunaojaribu kujenga) uhuru wa mawazo na maoni haonekani pale tunaporuhusu mawazo kama ya kwetu kutolewa, bali pale tunaporuhusu mawazo yanayopingana na mawazo yetu kutolewa na kuitetea haki ya wanaofanya hivyo kulindwa! Kitendo cha serikali kujifanya kuwa ndiyo pekee iliyo kisima cha habari sahihi ni uongo mwingine ambao hatuko tayari kuununua.

Serikali ituachie tupate habari kokote tunakozipata, tuzilinganishe habari hizo, na tuzipime kama watu wenye akili, na tuzitolee maamuzi juu ya ukweli wake. Vinginevyo, serikali iamue kupitisha sheria mpya ya Habari Sahihi toka Serikalini Pekee ya Mwaka 2007 ili tujue kuwa hatimaye Tanzania tumeingia rasmi kwenye utawala wa kibabe wa serikali ya kiimla inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi.

mr gentleman, nyakati hizo JF ilikuwa JF (Jambo Forums) na Mzee Mwanakijiji alikuwa ni Mzee Mwanakijiji, sijui wewe wakati huo ulikuwa wapi. Lakini hayo tuyaache, tukianza kufukua JF, itabidi wazee wengine wachutame lakini huyu mwenzetu inaonekana hayuko tayari kuchutama.

Kwa mwaka mzima baada ya Kikwete kula kiapo wapo walioshinda humu wakimsifia, lakini tupo wengine tulibahatika kutambua mapungufu yake hata kabla hajaapishwa. Zaidi ya hapo tupo tulioonya asipewe awamu nyingine mwaka 2010 lakini kama kawaida hatukusikilizwa.

Je unadhani ni sababu gani imemfanya Rais Magufuli kuahidi kuwalinda viongozi waliomtangulia? Tupo tulioona mapungufu ya Magufuli hata kabla ya kuapishwa kama tulivyoyaona mapungufu ya Kikwete mwaka 2005...kama Mzee Mwanakijiji ni nabii, je sisi ni akina nani?
 
Let freedom reign!
By Mzee Mwanakijiji, February 1, 2007
My fellow citizens, let freedom reign, from the sparkling snow-capped mount Kilimanjaro, to the green valleys of Southern Highlands, from the golden sands of the coast of the Indian ocean to the praised shores of Lake Tanganyika!

Let Freedom Ring! May our nation dare to rise to be all it can be, may we as a people and as a nation ascend to the heights that our forebearers never dreamed of, may we build a nation that is freer, modern, and yet very African!

Yes, may we one day, pass to the next generation of Tanzanians, a nation that has finally taken its rightful place among the nations of the world!

If our esteemed leaders won't lead now to fulfill such an ambition of ours, they'll find themselves following later! For Freedom never ceases to ring!

Huwezi kuamini kwamba haya maandishi yalielekezwa kwa awamu ya tano chini ya Jakaya Mrisho Kikwete! Leo wakosoaji wananyanyaswa wazi wazi, Mzee Mwanakijiji anasifia uongozi, uhuru (freedom)...where art thou gone?
 
Will you still say the same today?
Ahsante, nilikuwa nasubiri swali hili. Jibu ni yes nasimama na hayo niliyosema

Nikukumbushe msemo unaosema 'absolute power corrupts absolutely'

Kwa maana rahisi ya Kiswahili , nguvu zozote au nguvu za kiutawala, nguvu hizo huondoa uadilifu.

Je, tunahitaji kiongozi atakayeleta nidhamu, jibu ni yes
Tunahitaji kiongozi wa kupambana na uovu, wizi na ufisadi, jibu ni ndiyo

Nidhamu(discipline) huanza kwa mtu kabla ya kwenda nje. Nidhamu si woga au hofu, ni mpangilio, utaratibu, utii wa taratibu na kuzifanya kwa taratibu kwa kuzingatia utaratibu

Je, tuna nidhamu tunayohitaji, jibu ni hapana! Woga, kutisha, matumizi ya nguvu , matumizi mabaya ya nguvu (abuse of power) hayo si nidhamu. Tofauti ya nidhamu na woga au hofu ni nyembamba na mara nyingi watu hawawezi kutofautisha

Je, kuna mapambano ya uovu, yes yapo. Mapambano ya uovu ni across the board, kwamba hakuna anayepewa favor au kusalimika. Nidhamu ndiyo iongoze mapambano hayo bila kubagua au kuchagua nani mhalifu sana, nani mhalifu kidogo

Fisadi wa bilioni 36 na karushwa ka 5,000 huwezi kuweka katika madaraja. Mimba ni mimba tu hakuna ka mimba na li mimba.

Fisadi wa bilioni 36 anapoambia akamalizie kazi, huku fisadi wa mshahara hewa wa milioni 40 akiwekwa magereza, ni double standards na hiyo si nidhamu tunyaohitaji wala mapambano tunayotaka.

Kwanini tumefika hapo kinyume na matarajio tuliyoonyesha huko nyuma? Jibu ni rahisi absolute power corrupts absolutely na culture iliyojengeka ndani ya CCM miaka nenda rudi ya 'get away'

Ninasimama na kauli zangu 100% , sikubaliani na utekelezaji kwasababu haupo katika muktadha wa hoja yangu. Umekwenda kombo !

Judi wa Kishua mpwa nijaalie, za siku
 
Kuna mtu anadai kinachomsumbua Mzee Mwanakijiji ni uzalendo wake mkuu kwa "vatican", atamlinda na kumtetea "raia" mwenzie wa nchi hiyo iliyondani ya nchi nyingine.
 
Kuna mtu anadai kinachomsumbua Mzee Mwanakijiji ni uzalendo wake mkuu kwa "vatican", atamlinda na kumtetea "raia" mwenzie wa nchi hiyo iliyondani ya nchi nyingine.

you know better than that... ila kwa vile story za kijiweni ni stori tu basi ndiyo hivyo hivyo...
 
Back
Top Bottom