Hivi Hiki kijigazeti bado kipo ?Niliwahi kujuta hela yangu niliyotoa kukinunua.Hakina maana kabisa
Unakuta Ukurasa wa Kwanza kinaanza na headline kali kama hii ila ukikisoma ni majungu matupu.Ukurasa wa Pili unakutana na Makala kuhusu Elimu ya Nyota ,Unajimu na jinsi ya kumuita au kuishi na jini,Ukurasa wa 3 na 4 unakuta makala ndefu juu ya Freemason na alama za Illuminati,Ukurasa wa Tano Tangazo la Mganga wa Kienyeji kutoka Sumbawanga anayetibu Kisukari,Mvuto wa mapenzi,Pesa za majini,Kujiunga Freemason,Akili za Darasani,kupandishwa cheo kazini ,kuepuka kutumbuliwa jipu na dawa ya kumsahaulisha anayekudai halafu Ukurasa wa Sita Michezo unakutana na makala jinsi Mourinho alivyowahi kuoa jini.