Mwizukulu jilala
JF-Expert Member
- Jun 11, 2016
- 1,094
- 942
Pole sana bro, nawahurumia sana wadogo zako kwakuwa na kaka mpumbavuHuu mchakato usiutazame kwa jicho la kizembe-zembe. Utizame na ufuatilie kikamanda
Huu mchakato ni copy and paste kutoka kwa Paulo Kagame. Huu mchakato uko hatua za awali usidhani umefifia,nooo ndio kwanza kuni za kuwasha moto zinasanywa. Ninakupa experience ya ilikuwaje Kagame akabadilisha katiba kutoka miaka mitano mitano mpaka saba? Ilikuwa hivihivi anakataa-kataa, halafu wanyonge feki wanamlazimisha.
Mh. Juma Mkamia anajua anachokifanya, badala ya kumkebehi na kumdharau mnapaswa kumuandalia tuzo,zawadi ya ushindi. Subirini hoja yake ipewe nafasi ya kujadiliwa bungeni.
Mjadala huo utatumbuizwa na maandamano ya kumuunga mkono kutoka kwa "watanzania wanyonge". Kwanza itaanzia Dodoma. Wanyonge wa Dodoma wataandamano kumshinikiza rais akubali maombi yao. Halafu sauti zitapazwa na kuitikiwa na wanyonge kila mahali.
Hatima yake Rais ataheshimu kilio cha watanzania wanyonge waliokombolewa na John Pombe Joseph Magufuli toka mikononi mwa wapiga dili. Kwamba watanzania wanyonge wana nia njema na rasilimali za nchi.
Haaaaaaaa haaaaaaa. Msidhani kila mtu mshamba wengine tuna akili zetu na tutabaki kuona mbali siku zote. Msiseme sikusema