Magufuli apinga muswada wa haki za kijinsia wa EALA

Hamia kenya. Huko ni ruksa kutia mimba watoto wa shule kama utakavyo. Na wakitiwa mimba wanaendelea masomo kwa baraka za rais wao.
Na haya ndio aina ya majibu ya "wafuasi" wake. Mambo magumu na very sensitive yenye wider impacts kwa nchi wao wanakuja na majibu rahisi yasiyo na logic yoyote. Dunia ingekuwa rahisi kuhama nchi kama unavyoshauri, unadhani Africa ingebaki na watu kwa jinsi ilivyo na viongozi wenye IQ ndogo kila kona.
 
Na haya ndio aina ya majibu ya "wafuasi" wake. Mambo magumu na very sensitive yenye wider impacts kwa nchi wao wanakuja na majibu rahisi yasiyo na logic yoyote. Dunia ingekuwa rahisi kuhama nchi kama unavyoshauri, unadhani Africa ingebaki na watu kwa jinsi ilivyo na viongozi wenye IQ ndogo kila kona.
What is "very sensitive" here; if I may ask?
 
Sheria hii ipo tangu zamani, unless wewe ni dot com. Ukiwa mzazi mtoto akakuharibikia nyumbani hujui malezi bora. JK aliwahi sema wanafunzi akipata mimba mzazi afungwe.

Hamia kenya. Huko ni ruksa kutia mimba watoto wa shule kama utakavyo. Na wakitiwa mimba wanaendelea masomo kwa baraka za rais wao.
Tuacheni ushabiki wa sheria zilizopitwa na wakati au kwa Rais. Mimi ni mzazi mwenye watoto wa jinsia tofauti na nisingependa mwanangu akwame eti kwa sababu tu kuna mhuni amembaka, au kuna lizee limemlaghai na hata kama ni mihemuko ya ujana imemsukuma kufanya kosa hilo. Utakuwa umemmaliza mtoto huyu na ataishi kwa shida na kuendelea kuwa tegemezi kwako.

Kwa huyu anaependekeza kuhamia Kenya kwa sababu tu ya tofauti ya mawazo huna hoja na pengine hukuwahi kulinganisha maisha yako na mataifa mengine halafu ukagundua kuwa WaTz tuko nyuma sana kulinganisha na hata hao wa Kenya!!!
 
Isije ikawa njia ya kuwaondosha watu kwenye mjadala wa makinikia ( maana kule mambo ni magumu kuliko tunavyodhani, mziki ule ni mnene MTU anaweza umbuka at the end of the day) Ili tuje kujadili mimba za vijisichana vya shule ambavyo hata 20 havifikii kwa idadi.After all so kila msichana wa while anapata mimba!
 
Sio hoja kuitolea mapovu ni hoja mjadala....kwa maslahi Taifa na ipatikane suluhu kwa mijadala....hata Bungeni walikataa...kwa sasa kuna binti anarudi shule za serikali baada kujifungua?? Mmepipenda wenyewe!!!
Kama hoja ni wanafunzi wanaopata mimba kufukuzwa shule basi japo sikumpigia kura Magu lakin namuunga mkono 100%.
 
Magu ni kisu. Watz tunamuunga mkono na tupo nyuma yake 100%
Wewe ni zaidi ya nyumbu! Jaribu kuongeza na zako japo kidogo
Rais JPM apinga muswada wa haki za kijinsia unaojadiliwa Bunge la Afrika Mashariki

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amezindua barabara ya Bagamoyo-Msata na kutumia nafasi hiyo kuwakejeli wanaharakati wanaopigania haki za kijinsia miongoni mwa wanafunzi wa kike.



Miongoni mwa wanafunzi hawa kuna wanaolazimishwa kufanya ngono bila ridhaa yao na hatimaye kubeba mimba.

Pia wamo wanafunzi wanaoamua kukubali kufanya ngono kwa hiari yao lakini bila dhamira ya kubeba mimba, kwani nkuchagua kufanya ngono sio kuchagua kubeba mimba.

Sasa JPM anasema kuwa mwanafunzi yeyote atakayebeba mimba katika mazingira haya atakuwa amepoteza haki yake ya kupata elimu.

Pia, amesema kuwa mwanafunzi yeyote wa kiume atakaye sababisha mwanafunzi mwenzake wa kike kubeba mimba aondolewe shuleni na kufungwa jela miaka 30. Naye atakuwa amepoteza haki yake ya kupata elimu kwa sababu hiyo.

JPM ametoa maagizo hayo kwa sababu kuu mbili. Kwanza, anadai kuwa endapo msichana aliyejifungua tayari atarudi shuleni atawafundisha maadili mabaya wasichana wenzake.

Kwamba, wenzake wataona kuwa jambo la mwanafunzi kufanya ngono, kubeba mimba na kujifungua ni suala dogo, na hivyo kuwafanya wawe na wepesi wa kufanya ngono holela kabla ya kufikia uti uzima.

Pili, JPM anasema kuwa kwa kumruhusu mwanafunzi mzazi kurudi shuleni tutakuwa tumempa ruhusa ya kuendeleza mchezo wake wa kufanya ngono ya utotoni.

Kwamba, ataona kuwa kitendo chake hakikuwa na adhabu ya kutosha. Hapa adhabu ya kutosha, kwa mujibu wa JPM, ni kufutiwa haki yake ya kusoma.

Rais JPM anayasema haya wakati ambapo mambo yafuatayo katika Afrika Mashariki:

1. Bunge la Afrika Mashariki linajadili Muswada wa Sheria ya Haki za Kijinsia. Ulichapishwa katika gazeti la kiserikali la EAC Na. 2 la 20 january 2017. Muswada huu unapigania haki ya msichana kurudi shuleni baada ya kujifungua. Katika muswada huu, kifungu cha 9 kinasomeaka hivi:

“9(1) The partner states shall ensure that pregnant girls have a right to access free and compulsory primary and secondary education.

(2) A child shall not be expelled from scholl or any learning institution as a result of pregnancy.

(3) Subject to subsection (
1) the partner states shall ensure that girls who have become pregnant before completing their primary and secondary education are given the opportunity and facilities during pregnancy and after delivery, to continue with their education.

(4) The partner states shall, for the purposes of this section maintain records of all pregnancies occurring among adolescents in schools.

(5) The partner states shall introduce measures to protect children from any forms of abuse or related stigma or discrimination in the instances of early pregnancies by affording sexual and reproductive health information and where to access services to prevent early pregnancies.

(6) Partner states shall put in place systems to identify, manage, and refer children, adolescents and young persons, who have been victims of sexual abuse and are coming to health facilities and communities for psychological, health care, and legal support.

2. Tanzania ni muongoni mwa nchi nyingi za Afrika ambazo hazina mtaala wa elimu ya ujinsia kama somo linalo jitegemea.

3. Kwa mila na desturi za Kitanzania mchakato wa ujumuisho (socialisation) unajenga mtazamo uliosheheni mawazo hasi katika vichwa vya watoto (negative stereotypes) kuhusu suala zima la ujinsia wa bindamu.

4. Mtazamo wa dunia kuhusu masuala ya ujinsia ulio na wafuasi wengi (dominant sexual worldview) hautambui uwepo wa walemavu wa kijinsia (people with sexual disabilities) kama vile mwanaharakati aitwaye Mwamba Nyanda (pichani).

Katika kundi hili kuna watu wenye jinsia mbili na wale wenye jinsia tata (hermaphrodites and intersexed persons). Hivyo, jamii yetu haina utaratibu wa kuwatimizia mahitaji yao mashuleni, mahospitalini, magerezani na majumbani.

pic+mtanzania+mwenye+utata.jpg


5. Mpaka sasa, Wanateolojia wetu hawana teolojia makini ya ulemavu (personalistic theology of disability). Walemavu wa aina zote wanaambiwa kuwa wamekuwa hivyo kwa sababu ya dhambi zao.

Ni katika mazingira haya ambapo Rais JPM anasema wanaharakati wanaotaka wanafunzi wazazi warudi shuleni, basi wao watafute fedha na kuwajengea shule hizo. Yaani, wajenge shule maalum kwa ajili ya "wanafunzi wazazi."

Hakusema suala lolote kuhusu mitaala wa elimu ya ujinsia. hakujenga hoja kuonyesha dosari iliyomo katika muswada wa sheria ya ujinsia inayojadiliwa katika Bunge la Afrika Mashariki.

Hakufafanua rai kwamba kulazimishwa kufanya ngono shuruti sio kutoa ridhaa ya kubeba mimba. Aidha JPM hakusema kitu kuhusu hoja kwamba uamuzi wa kufanya ngono sio uamuzi wa kubeba mimba.

Kwa hakika Rais JPM amenzisha mjadala mkubwa na mkali. Tujadili.

 
.
Haki ya kufanya ngono unaanza lini (a) kwa mujibu wa physiolojua na (b) kwa mujibu wa sheria? Mambo haya mawili yanasikilizana? Kama hapana, hakuna tatizo?
Enhee! Endelea mbona unaishia njiani? Wakati ulianza vizuri?
 
...Mimi ni mzazi mwenye watoto...
Na mimi ni babu mwenye wajukuu wa jinsia tofauti, kwa hiyo ninaelewa ninazungumzia nini. Kama unataka jamii yenye uhuru wa kuwatia mimba watoto wa shule na kuwaacha waendelee na masomo hamia kenya nimeshakuambia. Huko wana rais ana mambo ya kizungu. Eti watanzania tuko nyuma sana; labda wewe uko nyuma, usitake kuwa msemaji wa wote.
 
Rais JPM apinga muswada wa haki za kijinsia unaojadiliwa Bunge la Afrika Mashariki
Mswada wa bunge la Afrika Mashariki?then what?hilo bunge haliwezi kutupangia masuala ya ndani.

By the way,mlengo wa ushirikiano ni maingiliano ya watu na uchumi,wamekosa changamoto za pande hizo mpaka kuingilia masuala ya ndani ya nchi zingine?
 
Yaani hata katika hili mnainua vichwa kumpinga rais! Was TZ wa ajabu sana. Kwa taarifa hata hao wasichana wanaopata mimba hawataki kurudi shule. Tusihalarishe dhambi kwa kumpinga rais, hiyo in mwiko. Km ni kuendelea mfumo unamruhusu kuendelea nje ya mfumo rasmi. After all that will be natural selection. Nimefunga mjadala, acheni kubeza dhamira ya kuitengeneza Tz.
 
.
Haki za kijinsia ziko pale pale hata kama Tanzania ikijitoa EAC....
Kama hizo haki zipo wewe tatizo lako nin?

Tanzania haitajitoa EAC na wakati wote haiwezi kuamuliwa mambo yake ya ndani na Bunge lolote lisilo bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
 
Suala la kurudi shule si zuri hata kidogo. Malezi yanahitaji mzazi au wazazi wote. Kwa kuwa ni mwanafunzi, yabidi ajifunze majukumu mapya pale anapokuwa mama, sio kigezo cha utoto, majukumu apewe bibi au babu.
Kumfunga au kumfukuza shule mwanaume chini ya miaka 18 haina tija.
Jambo la kutazamwa hapa ni je abortion iwe legal?. Kuhusu disabilities au abnormalities ni suala jipya na lina changamoto nyingi nchini Tanzania. Dini, tamaduni na hadithi ni baadhi ya vikwazo.
 
Mswada wa bunge la Afrika Mashariki?then what?hilo bunge haliwezi kutupangia masuala ya ndani.

By the way,mlengo wa ushirikiano ni maingiliano ya watu na uchumi,wamekosa changamoto za pande hizo mpaka kuingilia masuala ya ndani ya nchi zingine?
Elimu sio suala la ndani ya nchi pekee, haki za binaadam katika kupata elimu sio suala la ndani ya nchi. Millennium Development Goals ambapo nyie ni signatories inajumuisha jitihada katika kumpatia elimu ya lazima kila raia wa nchi yako.

Hata hivyo, hebu tafakari pale darasa la wanafunzi 45 kisha wasichana 10 kutiwa mimba na kugukuzwa shule pia wavulana 10 wametia mimba na kufungwa miaka 30. Trend hii ikiwa extended kwa 1/4 ya shule zote za serikali. Ni aina gani ya jamii ya watu unaoitengeneza katika taifa hili? Sio mambo yote yanahitaji kupayuka.
 
Kama unaona JPM hayuko sawa, waite wanaume wampe mimba binti yako (kama unaye) na uendelee na maisha yako. Shida iko wapi?

Hujui maana ya BINTI,ungekuwa unajua usingeandika huo upupu.Umeisha mtafutia bintiyo mwanaume wa kumpa mimba?
 
Hakuna cha kesho katika issue hiyo. Raid yuko sahihi. Kama ni wazungu wanatushinikiza wawajengee shule zao na kuwaletea waalimu na mitaala yao.

Hujui maana ya binti siku ukijajua utajutia maneno yako.
 
Back
Top Bottom