Magufuli apinga muswada wa haki za kijinsia wa EALA

Rtbkazoba

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
261
250
Rais JPM apinga muswada wa haki za kijinsia unaojadiliwa Bunge la Afrika Mashariki

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amezindua barabara ya Bagamoyo-Msata na kutumia nafasi hiyo kuwakejeli wanaharakati wanaopigania haki za kijinsia miongoni mwa wanafunzi wa kike.


Miongoni mwa wanafunzi hawa kuna wanaolazimishwa kufanya ngono bila ridhaa yao na hatimaye kubeba mimba.

Pia wamo wanafunzi wanaoamua kukubali kufanya ngono kwa hiari yao lakini bila dhamira ya kubeba mimba, kwani nkuchagua kufanya ngono sio kuchagua kubeba mimba.

Sasa JPM anasema kuwa mwanafunzi yeyote atakayebeba mimba katika mazingira haya atakuwa amepoteza haki yake ya kupata elimu.

Pia, amesema kuwa mwanafunzi yeyote wa kiume atakaye sababisha mwanafunzi mwenzake wa kike kubeba mimba aondolewe shuleni na kufungwa jela miaka 30. Naye atakuwa amepoteza haki yake ya kupata elimu kwa sababu hiyo.

JPM ametoa maagizo hayo kwa sababu kuu mbili. Kwanza, anadai kuwa endapo msichana aliyejifungua tayari atarudi shuleni atawafundisha maadili mabaya wasichana wenzake.

Kwamba, wenzake wataona kuwa jambo la mwanafunzi kufanya ngono, kubeba mimba na kujifungua ni suala dogo, na hivyo kuwafanya wawe na wepesi wa kufanya ngono holela kabla ya kufikia uti uzima.

Pili, JPM anasema kuwa kwa kumruhusu mwanafunzi mzazi kurudi shuleni tutakuwa tumempa ruhusa ya kuendeleza mchezo wake wa kufanya ngono ya utotoni.

Kwamba, ataona kuwa kitendo chake hakikuwa na adhabu ya kutosha. Hapa adhabu ya kutosha, kwa mujibu wa JPM, ni kufutiwa haki yake ya kusoma.

Rais JPM anayasema haya wakati ambapo mambo yafuatayo katika Afrika Mashariki:

1. Bunge la Afrika Mashariki linajadili Muswada wa Sheria ya Haki za Kijinsia. Ulichapishwa katika gazeti la kiserikali la EAC Na. 2 la 20 january 2017. Muswada huu unapigania haki ya msichana kurudi shuleni baada ya kujifungua. Katika muswada huu, kifungu cha 9 kinasomeaka hivi:

“9(1) The partner states shall ensure that pregnant girls have a right to access free and compulsory primary and secondary education.

(2) A child shall not be expelled from scholl or any learning institution as a result of pregnancy.

(3) Subject to subsection (
1) the partner states shall ensure that girls who have become pregnant before completing their primary and secondary education are given the opportunity and facilities during pregnancy and after delivery, to continue with their education.

(4) The partner states shall, for the purposes of this section maintain records of all pregnancies occurring among adolescents in schools.

(5) The partner states shall introduce measures to protect children from any forms of abuse or related stigma or discrimination in the instances of early pregnancies by affording sexual and reproductive health information and where to access services to prevent early pregnancies.

(6) Partner states shall put in place systems to identify, manage, and refer children, adolescents and young persons, who have been victims of sexual abuse and are coming to health facilities and communities for psychological, health care, and legal support.

2. Tanzania ni muongoni mwa nchi nyingi za Afrika ambazo hazina mtaala wa elimu ya ujinsia kama somo linalo jitegemea.

3. Kwa mila na desturi za Kitanzania mchakato wa ujumuisho (socialisation) unajenga mtazamo uliosheheni mawazo hasi katika vichwa vya watoto (negative stereotypes) kuhusu suala zima la ujinsia wa bindamu.

4. Mtazamo wa dunia kuhusu masuala ya ujinsia ulio na wafuasi wengi (dominant sexual worldview) hautambui uwepo wa walemavu wa kijinsia (people with sexual disabilities) kama vile mwanaharakati aitwaye Mwamba Nyanda (pichani).

Katika kundi hili kuna watu wenye jinsia mbili na wale wenye jinsia tata (hermaphrodites and intersexed persons). Hivyo, jamii yetu haina utaratibu wa kuwatimizia mahitaji yao mashuleni, mahospitalini, magerezani na majumbani.5. Mpaka sasa, Wanateolojia wetu hawana teolojia makini ya ulemavu (personalistic theology of disability). Walemavu wa aina zote wanaambiwa kuwa wamekuwa hivyo kwa sababu ya dhambi zao.

Ni katika mazingira haya ambapo Rais JPM anasema wanaharakati wanaotaka wanafunzi wazazi warudi shuleni, basi wao watafute fedha na kuwajengea shule hizo. Yaani, wajenge shule maalum kwa ajili ya "wanafunzi wazazi."

Hakusema suala lolote kuhusu mitaala wa elimu ya ujinsia. hakujenga hoja kuonyesha dosari iliyomo katika muswada wa sheria ya ujinsia inayojadiliwa katika Bunge la Afrika Mashariki.

Hakufafanua rai kwamba kulazimishwa kufanya ngono shuruti sio kutoa ridhaa ya kubeba mimba. Aidha JPM hakusema kitu kuhusu hoja kwamba uamuzi wa kufanya ngono sio uamuzi wa kubeba mimba.

Kwa hakika Rais JPM amenzisha mjadala mkubwa na mkali. Tujadili.


SEHEMU YA HOTUBA INAYOHUSIKA HII HAPA KATIKA MAANDISHI
===============================================

“Tulipoingia madarakani ndugu zangu, tuliamua kutenga bilioni 18.77 kwa ajili ya kutoa elimu bure. Kwamba mtoto ataingia darasa la kwanza mpaka sekondari, asome bure.

“Na, serikali tunachukua bajeti katika fedha hizi kidogo tunazozikusanya, na kuzipeleka kwenye elimu bure, kwa sababu watoto wetu, watoto wa maskini, walikuwa wanapata shida. Akienda shuleni anaambiwa ‘huna ada,’ anarudi nyumbani. Baadaye hasomi. Tukasema hawa watoto wa maskini, watoto wa Watanzania, lazima wasome bure.

“Sasa pametokea maneno mengine. Siku hizi nawasikia watu wa ma-NGO wanazungumza sana, kwamba mtoto akienda kule akapata mimba, arudi nyumbani azae, akishatoka kuzaa arudi shuleni. Sijui hao wanaozungumza haya walipata mimba wakiwa shuleni?

“Nataka niwaeleze, tukienda kwa mzaha wa namna hiyo, kwa kusikiliza ma-NGO yanakotupeleka yanalimaliza Taifa.

“Fikiria mtu ametoka pale amepata mimba, amezaa mtoto. Iwe kwa makusudi, iwe kwa raha yake, iwe kwa bahati mbaya, akienda shuleni ameishazaa, hawa wengine ambao hawajazaa atawafndisha.

“Halafu akipata mimba ya pili, anaenda nyumbani, akizaa tena anarudi shuleni. Anapata mimba ya tatu anaenda nyumbani, akizaa anarudi shuleni. Yaani tusomeshe wazazi?

“Nataka niwambie, na hizo NGO na ninyi wote mnaosikia, ndani ya utawala wangu, kama Rais, hakuna mwanafunzi mwenye mimba atakayerudi shuleni. Narudia, hakuna mtu mwenye mtoto, katika elimu ya darasa la kwanza mpaka sekondari, atakayerudi shuleni. Amechagua maisha hayo ya mtoto, akalee vizuri mtoto.

“Lakini, hata kama amepata mimba kwa bahati mbaya, yapo mambo mengi ya kufanya, ambayo yanaruhusu watu waliojifungua kushiriki. Anaweza kwenda VETA, anaweza akajifunza kushona kwa cherehani, anaweza akaenda kukopa akaanza kilimo cha kisasa, au akafanya shughuli nyingine.

“Lakini ukishazaa waranti ya kwenda shule ya msingi au sekondari hakuna tena. Labda ukazalie Chuo Kikuu. Wanaruhusiwa. Uwe mwaka wa kwanza, mwaka wa pili we zaa tu ukitaka.

“Lakini kama darasa la kwanza mpaka sekondari, tunapeleka watu walio na watoto, tunapoteza maadili yetu. Watazaa mno. Itafika baada ya miaka kadhaa, mtajikuta darasa la kwanza wote wana watoto, wanawahi kwenda kunyonyesha.

“Mchezo huo ni mzuri, na kila mmoja angependa aufanye. Halafu wanatokea watetezi wa mchezo huu kufanyika katika utaratibu wa hovyo wa kulipeleka Taifa mahali pabaya. Narudia, katika kipindi changu, kama Rais, ukishapata mimba ni kwa heri.

“Lakini nitoe wito kwa vyombo vya dola. Kwa sababu watakuja wengine watauliza, Je wanaowapa mimba wanafunzi vipi? Wanaowapa mimba kama ni mwanafunzi au mtu wa nje, sheria ipo. Kuna miaka 30 inawasubiri.

“Kama ni mwanafunzi, huyu atakwenda kulea mtoto wake, hutu atakwenda kutumikia miaka 30. Na mashamba tumeyafungua mengi. Zile nguvu alizozitumia kuzaa mtoto akazitumie kulima. Akitoka kule baada ya miaka 30, sisi tumepata mpunga wetu na yeye nguvu zimeishapungua, inawezekana atabaki na huyo huyo mtoto.

“Lakini kusema mtu amezaa, arudi shuleni, halafu awe anawahubiria wenzake, ‘unajua ilikuwa hivi, nilijaribu hivi hivi tu, na kuzaa ni rahisi tu,’ wenzake nao watatamani nao wakazae, halafu baadae warudi shuleni. Watu wa ajabu sana. Hatuwezi tukalipeleka Taifa hili katika maadili ambayo hayapo. Never (haiwezekani).

“Lakini, hao wanaowatetea wazazi, hawazuiliwi kuanzisha shule zao. Hizi NGO wanajilipa hela nyingi kutoka kwa hao wanaowafadhili. Wakafungue shule za wazazi kwa kutumia fedha hizo. Kwani wakifungua shule hapo ya private (shule binafsi), kwa ajili ya wanafunzi wote wenye watoto wakasomesha tutawazuia?

“Wakijaribu, ndipo watagundua kuwa, mwanafunzi mwenye mtoto akishaanza kufanya hesabu mbili mara mbili, hata kabla hajajibu, atamwambia mwalimu, ‘nakwenda kunyonyesha mtoto wangu namsikia huko analia.’

“Hizi NGO zikafungue shule za wazazi. Sio zilazimishe serikali. Ninatoa pesa ya bure hapa, kwa ajili ya kusomesha watoto, wanafunzi ambao wameamua kwenda kusoma, halafu nikasomeshe na wazazi?

“Kwa hiyo Mama Salma nakupongeza. Ulisimama na kulizungumza Bungeni. Endelea hivyo hivyo. Sisi sote tuna watoto. Hata kama mimi nina mtoto wangu wa kike, akapate mimba huko halafu tena nimpiganie kurudi shuleni? Waende wakafanye halafu wataona kama nitawarudisha shuleni.

“Ni lazima tufike mahali ndugu zangu Watanzania tushtuke. Hawa wanaotuletea haya mambo msifikiri wanatupenda sana. Wametuletea madawa wa kulevya, watoto wetu unawakuta wanatoa makamasi tu. Hawawezi wakalima, hawawezi wakafanya nini, wao wanashangilia.

“Wametuletea watu kubakana, wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake, wakati hata ng’ombe na hata mbuzi haziwahi kukosea huo mtindo. Huwezi ukamwona mbuzi, anafanya hivyo.

“Nyie wachungaji mmeshawahi kuchunga. Mmeshawahi kuona hata ng’ombe anakosea? Au mbuzi? Au kondoo? Hata nguruwe au mnyama yeyote? Lakini tunaambiwa sisi Watanzania tuwe tunakosea mahali penyewe. Ni ujinga ni upumbavu.

“Kwa hiyo, ni lazima tufike mahali Watanzania tujitambue. Tumwogope Mungu. Tujirekebishe. Haya mambo ya ku-copy copy (kuigaiga) tutakuja ku-copy (kuiga) na mambo ya ajabu. Na saa nyingine wanaleta mambo haya kwa njia ya michango michango na misaada. Wanasema tutakusaidia hiki. Kumbe na hayo wanayotusaidia ni mali zetu zimetoka huku.

“Unajua ni lazima tujanjaruke, tujitambue basi ndugu zangu Watanzania. Tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe. Tanzania imebarikiwa na mwenyezi Mungu, ni tajiri mno. Tajiri! Na ndio maana napongeza watendaji na viongozi wa chama changu ambao wamekuwa wasimamizi wazuri wa maadili ya Watanzania.

“Niwaombe ndugu zangu wa Bagamoyo tuendelee kusimama hivyo.Tutafika na Mungu atatusaidia. Saa nyingine tunapata laana ya ajabu kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume cha maumbile yetu. Yaani unang’ang’ania tu mahali ambapo hapastahili! Tabu sana, baghosha!

“Ninazungumza haya kwa sababu niko kwa watani zangu. Maana ningezumza haya mahali pengine wangesema, ‘mnamwona huyu Rais na kauli zake!’ Lakini, ni nafuu kuongelea aibu ili kuondoa aibu. Tukiichekea aibu itatumaliza.

“Na hapa kwa sababu kuna vijana ni lazima tuwaenzi, tuwaeleze. Na niwaombe vijana, wa maeneo haya Bagamoyo, tuchape kazi. Vya bure havipo. Nafasi imeishapatikana ya kuwa na viwanda vingi. Serikali inatengeneza mazingira mazuri ya kuwa na umeme, maji, ili tuvitumie hivi kwa ajili ya kujenga Tanzania yetu. Sisi wazee tutaondoka mtabaki nyinyi.

“Mjipange kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya. Tanzania yenye mwelekeo. Tanzania yenye maendeleo. Mimi urais huu ni wa temporary (urais unapita).

“Pamekuwepo na marais wangapi? Alikuwepo Nyerere, amekuka Mwingi, amekuja Mkapa, amekuja mzee Kikwete, na mimi baadaye nitakuwa mzee, watakuja wengine. Lakini, katika kipindi hiki lazima niwaeleze yale ambayo nina wajibu wa kuyaeleza.

“Bagamoyo oyee! Jamani nilikuja hapa kuzindua mradi. Lakini nafikri message sent and delivered (ujumbe umetumwa na umefika).”


 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,387
2,000
Ila Rais anatakiwa aweke akiba ya Maneno. Kuna kesho tusiyoijua.
 

COPPER

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
2,117
2,000
Rais JPM apinga muswada wa haki za kijinsia unaojadiliwa Bunge la Afrika Mashariki

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amezindua barabara ya Bagamoyo-Msata na kutumia nafasi hiyo kuwakejeli wanaharakati wanaopigania haki za kijinsia miongoni mwa wanafunzi wa kike.


Miongoni mwa wanafunzi hawa kuna wanaolazimishwa kufanya ngono bila ridhaa yao na hatimaye kubeba mimba.

Pia wamo wanafunzi wanaoamua kukubali kufanya ngono kwa hiari yao lakini bila dhamira ya kubeba mimba, kwani nkuchagua kufanya ngono sio kuchagua kubeba mimba.

Sasa JPM anasema kuwa mwanafunzi yeyote atakayebeba mimba katika mazingira haya atakuwa amepoteza haki yake ya kupata elimu.

Pia, amesema kuwa mwanafunzi yeyote wa kiume atakaye sababisha mwanafunzi mwenzake wa kike kubeba mimba aondolewe shuleni na kufungwa jela miaka 30. Naye atakuwa amepoteza haki yake ya kupata elimu kwa sababu hiyo.

JPM ametoa maagizo hayo kwa sababu kuu mbili. Kwanza, anadai kuwa endapo msichana aliyejifungua tayari atarudi shuleni atawafundisha maadili mabaya wasichana wenzake.

Kwamba, wenzake wataona kuwa jambo la mwanafunzi kufanya ngono, kubeba mimba na kujifungua ni suala dogo, na hivyo kuwafanya wawe na wepesi wa kufanya ngono holela kabla ya kufikia uti uzima.

Pili, JPM anasema kuwa kwa kumruhusu mwanafunzi mzazi kurudi shuleni tutakuwa tumempa ruhusa ya kuendeleza mchezo wake wa kufanya ngono ya utotoni.

Kwamba, ataona kuwa kitendo chake hakikuwa na adhabu ya kutosha. Hapa adhabu ya kutosha, kwa mujibu wa JPM, ni kufutiwa haki yake ya kusoma.

Rais JPM anayasema haya wakati ambapo mambo yafuatayo katika Afrika Mashariki:

1. Bunge la Afrika Mashariki linajadili Muswada wa Sheria ya Haki za Kijinsia. Ulichapishwa katika gazeti la kiserikali la EAC Na. 2 la 20 january 2017. Muswada huu unapigania haki ya msichana kurudi shuleni baada ya kujifungua. Katika muswada huu, kifungu cha 9(1)-(4) kinasomeaka hivi:

“9(1) The partner states shall ensure that pregnant girls have a right to access free and compulsory primary and secondary education. (2) A child shall bot be expelled from scholl or any learning institution as a result of pregnancy. (3) Subject to subsection (1) the partner states shall ensure that girls who have become pregnant before completing their primary and secondary education are given the opportunity and facilities during pregnancy and after delivery, to continue with their education. (4) The partner states shall, for the purposes of this section maintain records of all pregnancies occurring among adolescents in schools.”

2. Tanzania ni muongoni mwa nchi nyingi za Afrika ambazo hazina mtaala wa elimu ya ujinsia kama somo linalo jitegemea.

3. Kwa mila na desturi za Kitanzania mchakato wa ujumuisho (socialisation) unajenga mtazamo uliosheheni mawazo hasi katika vichwa vya watoto (negative stereotypes) kuhusu suala zima la ujinsia wa bindamu.

4. Mtazamo wa dunia kuhusu masuala ya ujinsia ulio na wafuasi wengi (dominant sexual worldview) hautambui uwepo wa walemavu wa kijinsia (people with sexual disabilities) kama vile mwanaharakati aitwaye Nyanda. Katika kundi hili kuna watu wenye jinsia mbili na wale wenye jinsia tata (hermaphrodites and intersexed persons). Hivyo, jamii yetu haina utaratibu wa kuwatimizia mahitaji yao mashuleni, mahospitalini, magerezani na majumbani.

5. Mpaka sasa, Wanateolojia wetu hawana teolojia makini ya ulemavu (personalistic theology of disability). Walemavu wa aina zote wanaambiwa kuwa wamekuwa hivyo kwa sababu ya dhambi zao.

Ni katika mazingira haya ambapo Rais JPM anasema wanaharakati wanaotaka wanafunzi wazazi warudi shuleni, basi wao watafute fedha na kuwajengea shule hizo. Yaani, wajenge shule maalum kwa ajili ya "wanafunzi wazazi."

Hakusema suala lolote kuhusu mitaala wa elimu ya ujinsia. hakujenga hoja kuonyesha dosari iliyomo katika muswada wa sheria ya ujinsia inayojadiliwa katika Bunge la Afrika Mashariki.

Hakufafanua rai kwamba kulazimishwa kufanya ngono shuruti sio kutoa ridhaa ya kubeba mimba. Aidha JPM hakusema kitu kuhusu hoja kwamba uamuzi wa kufanya ngono sio uamuzi wa kubeba mimba.

Kwa hakika Rais JPM amenzisha mjadala mkubwa na mkali. Tujadili.

Ushoga hapana kabisa, la wanafunzi wazazi hata Bunge letu limekataa.
 

Rtbkazoba

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
261
250
Ushoga hapana kabisa, la wanafunzi wazazi hata Bunge letu limekataa.
.
Katika maelezo yangu ya msingi sijaongelea ushoga. Kifungu kinachohusika hiki hapa:

"4. Mtazamo wa dunia kuhusu masuala ya ujinsia ulio na wafuasi wengi (dominant sexual worldview) hautambui uwepo wa walemavu wa kijinsia (people with sexual disabilities) kama vile mwanaharakati aitwaye Nyanda. Katika kundi hili kuna watu wenye jinsia mbili na wale wenye jinsia tata (hermaphrodites and intersexed persons). Hivyo, jamii yetu haina utaratibu wa kuwatimizia mahitaji yao mashuleni, mahospitalini, magerezani na majumbani."

 

yoga

JF-Expert Member
Jan 6, 2013
1,452
2,000
Hahaha kama rais uyu tumepata sio kwa maneno hayo eti kamchezo ako ni katam kilamtu anapenda kukafanya
 

Rtbkazoba

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
261
250
Mkuu wa nchi ni kiongozi wa wote, wazima na walemavu kama vile kina Nyanda...
================================================================
Nyanda, Mtanzania mwenye utata wa jinsi

Na Florence Majani, Mwananchi

Jumanne, MARCH 28, 2017Kwa mara ya kwanza nilipomuona mwanaharakati wa masuala ya afya ya uzazi, Mwamba Nyanda maeneo ya Sinza, Dar es Salaam nilivutiwa na mwonekano wake, nikajawa shauku ya kutaka kukaa karibu naye. Nilifanya miadi nikafanikiwa kuonana naye.Hakika, Nyanda ni mwanamume anayejipenda.

Kama mwanamke atakuwa hajavutiwa na uvaaji wake basi anaweza kunaswa na mwendo wake au sauti au sura yake.“Mambo kaka,” nilimsalimia tulipokutana huku tukitafuta mahali pa kukaa. “Poa,” alinijibu.

Hiyo ndiyo siku nilipoifahamu historia ya maisha na shughuli zake za uanaharakati wa masuala ya afya ya uzazi, mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi (VVU) na anavyojihusisha na biashara na muziki.

Pamoja na utanashati, mvuto, uwezo wa kujenga hoja na sauti yenye ushawishi kuna kitu kinachomfanya akose raha maishani mwake. Kitu hicho si kingine bali utata wa jinsi yake.Kwamba ingawa sauti, muonekane, mavazi na mwendo wake vyote vinamtambulisha kuwa ni mwanamume, sura yake inamuonyesha kuwa ni mwanamke.

Kwamba ingawa yeye anajiona ni mwanamume kamili, jamii inayomzunguka hata baadhi ya ndugu zake wanamuona ni mwanamke.Maisha yake tangu utotoni yamesongwa na namna ya kukabili ukweli kuhusu utata wa jinsi yake.

Kwa Kiingereza Nyanda ni ‘intersex’ yaani hali ya kibaolojia, ambapo mtu huzaliwa akiwa na viungo vya uzazi, vichocheo, tabia au mwonekano wa nje ambao haumuweki katika kundi lolote la kuwa mwanamke au mwanamume au akiwa na sifa za kibaolojia zilizochanganyika kutoka jinsi zote mbili.

Jamii imweleweHivi sasa anataka jamii ikubaliane na hali halisi, kwamba yeye ni mwanamume. “Mimi ni mmoja, wapo wengi wanaopitia shida kama zangu ambazo ni ngumu zaidi, nataka niwe kioo cha jamii kwa kuwa jasiri katika mazingira haya,” anasema.

Alizaliwa miaka 26 iliyopita mkoani Morogoro akiwa mtoto wa pili kati ya wawili katika familia yao.

Kadri alivyozidi kukua alianza kujiona yeye si mwanamke kama wazazi wake walivyokuwa wanamweka na alijiona tofauti na jina walilompa hadi akiwa na umri wa miaka sita.“Nilianza kujisikia wa tofauti, yaani sipendi kucheza na watoto wa kike, sipendi mavazi ya kike waliyokuwa wananivalisha yaani sikujisikia mimi eti ni mtoto wa kike,” anasema.

Kadri siku zilivyokuwa zikisogea, ndivyo wasiwasi ulivyoongezeka na akijiuliza maswali, itakuwaje ukifika wakati akavunja ungo au akaota matiti? “Nilichelewa kuota matiti na hata yalipoota yalikuwa madogo sana, huwezi kuyaona, lakini nilikuwa nawaza, hivi nitabalehe?”

Hali hiyo ilimfanya awe mpenzi wa magazeti hivyo alitumia muda mwingi kusoma magazeti akidhani angesoma mahali maelezo ya dawa ya kutibu au kuzuia hedhi au kuota maziwa.

Lakini hakuwahi kupata tiba hiyo.Maisha yaliendelea huku mtihani ukizidi kuwa namna ya kutegua kitendawili cha jinsi yake na jamii ikamwelewa. Alipofikisha umri miaka 15-16, alizidi kuwa na mwonekano wa kiume, sura, sauti mpaka koromeo lake lilijitokeza kama ilivyo kwa wanamume.

Mabadiliko hayo pia yaliwapa changamoto wazazi wake. Hapo ndipo mama yake aliyefikiri mwanaye anakabiliwa na mapepo, aliamua kumchukua na kuanza kupita katika makanisa ili afanyiwe maombi.“Ilifikia mahali hata mimi nilidhani huenda kweli nina mapepo.

Ilinipa shida,” anaeleza.Mazingira mengine magumu yalikuwa shuleni. “Hali ya shuleni ilikuwa ngumu. Nilihisi shule nzima niko peke yangu. Nakumbuka nilishawahi kusimamishwa mbele na kuadhibiwa kisa muonekano wangu,” anasema.

Mwalimu wa zamu siku hiyo aliamua kumpa adhabu kwa madai ya kujiweka kiume licha ya kwamba alikuwa anavaa sare za shule za kike. Mbali ya kuadhibiwa na walimu mara kadhaa aliingia katika mzozo na wanafunzi wenzake.

Wapo waliomwita tomboy (msichana ambaye anaonyesha hulka na tabia zinazofikiriwa kuwa za kiume kama kuvaa nguo za kiume na kushiriki kazi na michezo ya aina hiyo ambayo kwa utamaduni inafikiriwa si ya kike).

Wengine walimwita dumejike na majina mengi ambayo hayakumfurahisha.Pia, wakati mwingine alikuwa anaingia katika mabishano mazito na wenzake kuhusu suala la jinsi. “Wao wanasema kuna jinsi mbili mke na mume, mimi najaribu kuwaelimisha kuwa zipo tatu; me, ke na jinsi tata ambao huitwa dume jike.

Na kuna dhana kwenye jamii kuwa wapo watu wanaozaliwa na jinsi mbili, kitu ambacho bado jamii inakosea,” anasema.“Wengine wanasema nawachanganya. Wengine eti nawaletea mambo ya Ulaya. Wanasema hakuna watu kama hawa katika jamii wakati tafiti zipo zinaonyesha kama tupo na jinsi tunavyopata shida,” anasema.Hata hivyo, Nyanda hakutaka kuweka wazi iwapo ana jinsi mbili.

Jamii haikumwelewa wakati ule na hadi sasa bado haimwelewi. Mara kadhaa amefukuzwa katika nyumba za kupanga kutokana na mwonekano wake na amekuwa akikosa ajira.“Yaani kutokana na jinsia na mwonekano hata kama nina elimu sipewi ajira, hii imenitokea mara kadhaa sitaki kutaja kampuni si vizuri, ila Mungu anawaona,” anaeleza.

Aliwahi kupeleka barua ya maombi ya kazi katika kampuni moja, akaitwa kwenye usaili, lakini baadaye wakaanza kumhoji kuhusu jinsi yake na wala si masuala ya kazi aliyoomba.

Baada ya hapo, hakuitwa tena.“Kwingine nikiomba kazi wanaishia kusema kweli ninafaa, nina vigezo vyote lakini hawawezi kuniajiri kutokana na utambulisho na muonekano wangu.“Hili la kukosa kazi halijanitokea mara moja, hali hiyo ilinipelekea kuninyanyapaa kisaikolojia juu ya ajira nchini,” anasema.

Kunyanyapaliwa na wenye nyumba, “Utakuta napokewa vizuri kwenye nyumba ya kupanga lakini sijui watu wanatokea wapi na kumletea mwenye nyumba maneno. Basi baada ya siku mbili tatu, nafukuzwa kwenye nyumba,” anasema.

Siku moja alipokuwa katika baa moja jijini alijikuta akifuatwa na watu alipoingia choo cha wanaume, ambacho kwake ni sahihi kwa sababu anaamini yeye ni mwanamme.Japokuwa mama yake hakuwa anaikubali hali aliyonayo, baba yake amekuwa akimtia moyo. “Usitetereke na wala usisikilize wanayosema mabaya juu yako. Usiogope, cha muhimu ishi na watu vizuri,” anasema akinukuu maneno ya baba yake.

Mazingira haya yamemfanya awe mwanaharakati wa masuala ya afya ya uzazi, virusi vya ukimwi nafasi inayompa fursa ya kufanya kampeni jamii imuelewe na isimnyanyapae pamoja na wengine wengi wa aina yake.Takwimu za Umoja wa Mataifa (UN) zinaonyesha kuwa idadi ya watu wenye jinsi tata duniani ni asilimia 1.7.

Kadhalika, Shirika la Afya Duniani (WHO) katika ripoti yake ya 2015 kuhusu miongozo ya afya ya jinsia, haki za binadamu na sheria limeeleza kuwatambua watu wenye jinsi tata.

“Jinsi tata ni kasoro za kimaumbile kama zilivyo nyingine na hivyo wasibaguliwe, wapewe huduma za afya wala wasitengwe,” inasema ripoti hiyo.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea afya kwa makundi maalumu nchini (CHESA), John Kashia anasema mtazamo hasi juu ya watu wa kundi hili ndiyo unaosababisha wakati mwingine wakose hata huduma za afya.“Wizara ya afya inatakiwa iwape elimu watu hawa, iwatengenezee mazingira rafiki wafikapo katika vituo vitoavyo huduma za afya,” anasema.

Kashia anasema kadri unyanyapaa unavyozidi ndivyo wanavyogeuka kuwa watu hatari au hata wanapata magonjwa.Pia, amewahi kuhubiriwa alipokwenda hospitali kupata huduma. Madaktari na washauri wanamuuliza maswali mengi ambayo lengo si kumsaidia bali kutaka kujua au kujifurahisha.

Semenya na Odiele: Utata wa jinsi alionao Nyanda ni kama ule wa mwanariadha Caster Semenya wa Afrika Kusini, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 800 kwenye Michezo ya Olimpiki 2016 na ubingwa wa dunia 2009.

Semenya mwenye mwonekano wa kiume na baadhi ya sifa za mwanamke, alianza kupata changamoto mwaka 2009 wakati huo akiwa na umri wa miaka 18, baada ya kushinda mbio za wanawake za mita 800.

Wanariadha wenzake walilalamika kuwa si mwanamke iweje ashiriki mbio za wanawake?Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), Pierre Weiss alisema; “Semenya ni mwanamke lakini inawezekana siyo kwa asilimia 100.”

Baadaye alizuiwa kushiriki mashindano hadi alipopimwa na kuonekana ana korodani kwa ndani, homoni za kike kwa kiasi fulani, nyumba ya uzazi lakini na uume mdogo.

Pia, Nyanda ni kama alivyo mwanamitindo wa Kibelgiji, Hanne Gaby Odiele ambaye amejitambulisha Januari mwaka huu.

Odiele ana baadhi ya sehemu za kiume, kama korodani zilizojificha kwa ndani na sehemu za kike kama matiti, lakini hana nyumba ya uzazi huku mwendo na sauti yake vyote ni vya kiume.
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,290
2,000
Waliowapa mimba kwa ridhaa yao wanafungwa gerezani miaka 30 halafu wao waendelee kudunda kama kawa!!! Tena adhabu yao hiyo ya kutorudi shuleni ni ndogo sana. Walitakiwa nao wafungwe miaka 30 kama wenzawao. Hapo wangeogopa kuruhusu pusy ovyo ovyo. Visichana hivi kupata mimba au ukimwi ni vihere here vyao tu. Wazungu wasitake kuvuruga mila na desturi zetu.

Hapa hatuongelei kwa waliobakwa. Na aliyebakwa hasubiri kuripoti polisi hadi amepata mimba. Hatutakiwi kutungiwa sheria na EALA ya namna ya kuwa care psyschologically ana humanitariarly wanafunzi wetu wakike waliobakwa na kupatwa au kutopatwa na mimba/ukimwi. Siyo kweli kwamba hawapewi elimu ya reproductive health ikwamo na matumizi ya protective sexual gears.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom