Magufuli apinga muswada wa haki za kijinsia wa EALA

Rais JPM apinga muswada wa haki za kijinsia unaojadiliwa Bunge la Afrika Mashariki

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amezindua barabara ya Bagamoyo-Msata na kutumia nafasi hiyo kuwakejeli wanaharakati wanaopigania haki za kijinsia miongoni mwa wanafunzi wa kike.



Miongoni mwa wanafunzi hawa kuna wanaolazimishwa kufanya ngono bila ridhaa yao na hatimaye kubeba mimba.

Pia wamo wanafunzi wanaoamua kukubali kufanya ngono kwa hiari yao lakini bila dhamira ya kubeba mimba, kwani nkuchagua kufanya ngono sio kuchagua kubeba mimba.

Sasa JPM anasema kuwa mwanafunzi yeyote atakayebeba mimba katika mazingira haya atakuwa amepoteza haki yake ya kupata elimu.

Pia, amesema kuwa mwanafunzi yeyote wa kiume atakaye sababisha mwanafunzi mwenzake wa kike kubeba mimba aondolewe shuleni na kufungwa jela miaka 30. Naye atakuwa amepoteza haki yake ya kupata elimu kwa sababu hiyo.

JPM ametoa maagizo hayo kwa sababu kuu mbili. Kwanza, anadai kuwa endapo msichana aliyejifungua tayari atarudi shuleni atawafundisha maadili mabaya wasichana wenzake.

Kwamba, wenzake wataona kuwa jambo la mwanafunzi kufanya ngono, kubeba mimba na kujifungua ni suala dogo, na hivyo kuwafanya wawe na wepesi wa kufanya ngono holela kabla ya kufikia uti uzima.

Pili, JPM anasema kuwa kwa kumruhusu mwanafunzi mzazi kurudi shuleni tutakuwa tumempa ruhusa ya kuendeleza mchezo wake wa kufanya ngono ya utotoni.

Kwamba, ataona kuwa kitendo chake hakikuwa na adhabu ya kutosha. Hapa adhabu ya kutosha, kwa mujibu wa JPM, ni kufutiwa haki yake ya kusoma.

Rais JPM anayasema haya wakati ambapo mambo yafuatayo katika Afrika Mashariki:

1. Bunge la Afrika Mashariki linajadili Muswada wa Sheria ya Haki za Kijinsia. Ulichapishwa katika gazeti la kiserikali la EAC Na. 2 la 20 january 2017. Muswada huu unapigania haki ya msichana kurudi shuleni baada ya kujifungua. Katika muswada huu, kifungu cha 9 kinasomeaka hivi:

“9(1) The partner states shall ensure that pregnant girls have a right to access free and compulsory primary and secondary education.

(2) A child shall not be expelled from scholl or any learning institution as a result of pregnancy.

(3) Subject to subsection (
1) the partner states shall ensure that girls who have become pregnant before completing their primary and secondary education are given the opportunity and facilities during pregnancy and after delivery, to continue with their education.

(4) The partner states shall, for the purposes of this section maintain records of all pregnancies occurring among adolescents in schools.

(5) The partner states shall introduce measures to protect children from any forms of abuse or related stigma or discrimination in the instances of early pregnancies by affording sexual and reproductive health information and where to access services to prevent early pregnancies.

(6) Partner states shall put in place systems to identify, manage, and refer children, adolescents and young persons, who have been victims of sexual abuse and are coming to health facilities and communities for psychological, health care, and legal support.

2. Tanzania ni muongoni mwa nchi nyingi za Afrika ambazo hazina mtaala wa elimu ya ujinsia kama somo linalo jitegemea.

3. Kwa mila na desturi za Kitanzania mchakato wa ujumuisho (socialisation) unajenga mtazamo uliosheheni mawazo hasi katika vichwa vya watoto (negative stereotypes) kuhusu suala zima la ujinsia wa bindamu.

4. Mtazamo wa dunia kuhusu masuala ya ujinsia ulio na wafuasi wengi (dominant sexual worldview) hautambui uwepo wa walemavu wa kijinsia (people with sexual disabilities) kama vile mwanaharakati aitwaye Mwamba Nyanda (pichani).

Katika kundi hili kuna watu wenye jinsia mbili na wale wenye jinsia tata (hermaphrodites and intersexed persons). Hivyo, jamii yetu haina utaratibu wa kuwatimizia mahitaji yao mashuleni, mahospitalini, magerezani na majumbani.

pic+mtanzania+mwenye+utata.jpg


5. Mpaka sasa, Wanateolojia wetu hawana teolojia makini ya ulemavu (personalistic theology of disability). Walemavu wa aina zote wanaambiwa kuwa wamekuwa hivyo kwa sababu ya dhambi zao.

Ni katika mazingira haya ambapo Rais JPM anasema wanaharakati wanaotaka wanafunzi wazazi warudi shuleni, basi wao watafute fedha na kuwajengea shule hizo. Yaani, wajenge shule maalum kwa ajili ya "wanafunzi wazazi."

Hakusema suala lolote kuhusu mitaala wa elimu ya ujinsia. hakujenga hoja kuonyesha dosari iliyomo katika muswada wa sheria ya ujinsia inayojadiliwa katika Bunge la Afrika Mashariki.

Hakufafanua rai kwamba kulazimishwa kufanya ngono shuruti sio kutoa ridhaa ya kubeba mimba. Aidha JPM hakusema kitu kuhusu hoja kwamba uamuzi wa kufanya ngono sio uamuzi wa kubeba mimba.

Kwa hakika Rais JPM amenzisha mjadala mkubwa na mkali. Tujadili.


SEHEMU YA HOTUBA INAYOHUSIKA HII HAPA KATIKA MAANDISHI
===============================================

“Tulipoingia madarakani ndugu zangu, tuliamua kutenga bilioni 18.77 kwa ajili ya kutoa elimu bure. Kwamba mtoto ataingia darasa la kwanza mpaka sekondari, asome bure.

“Na, serikali tunachukua bajeti katika fedha hizi kidogo tunazozikusanya, na kuzipeleka kwenye elimu bure, kwa sababu watoto wetu, watoto wa maskini, walikuwa wanapata shida. Akienda shuleni anaambiwa ‘huna ada,’ anarudi nyumbani. Baadaye hasomi. Tukasema hawa watoto wa maskini, watoto wa Watanzania, lazima wasome bure.

“Sasa pametokea maneno mengine. Siku hizi nawasikia watu wa ma-NGO wanazungumza sana, kwamba mtoto akienda kule akapata mimba, arudi nyumbani azae, akishatoka kuzaa arudi shuleni. Sijui hao wanaozungumza haya walipata mimba wakiwa shuleni?

“Nataka niwaeleze, tukienda kwa mzaha wa namna hiyo, kwa kusikiliza ma-NGO yanakotupeleka yanalimaliza Taifa.

“Fikiria mtu ametoka pale amepata mimba, amezaa mtoto. Iwe kwa makusudi, iwe kwa raha yake, iwe kwa bahati mbaya, akienda shuleni ameishazaa, hawa wengine ambao hawajazaa atawafndisha.

“Halafu akipata mimba ya pili, anaenda nyumbani, akizaa tena anarudi shuleni. Anapata mimba ya tatu anaenda nyumbani, akizaa anarudi shuleni. Yaani tusomeshe wazazi?

“Nataka niwambie, na hizo NGO na ninyi wote mnaosikia, ndani ya utawala wangu, kama Rais, hakuna mwanafunzi mwenye mimba atakayerudi shuleni. Narudia, hakuna mtu mwenye mtoto, katika elimu ya darasa la kwanza mpaka sekondari, atakayerudi shuleni. Amechagua maisha hayo ya mtoto, akalee vizuri mtoto.

“Lakini, hata kama amepata mimba kwa bahati mbaya, yapo mambo mengi ya kufanya, ambayo yanaruhusu watu waliojifungua kushiriki. Anaweza kwenda VETA, anaweza akajifunza kushona kwa cherehani, anaweza akaenda kukopa akaanza kilimo cha kisasa, au akafanya shughuli nyingine.

“Lakini ukishazaa waranti ya kwenda shule ya msingi au sekondari hakuna tena. Labda ukazalie Chuo Kikuu. Wanaruhusiwa. Uwe mwaka wa kwanza, mwaka wa pili we zaa tu ukitaka.

“Lakini kama darasa la kwanza mpaka sekondari, tunapeleka watu walio na watoto, tunapoteza maadili yetu. Watazaa mno. Itafika baada ya miaka kadhaa, mtajikuta darasa la kwanza wote wana watoto, wanawahi kwenda kunyonyesha.

“Mchezo huo ni mzuri, na kila mmoja angependa aufanye. Halafu wanatokea watetezi wa mchezo huu kufanyika katika utaratibu wa hovyo wa kulipeleka Taifa mahali pabaya. Narudia, katika kipindi changu, kama Rais, ukishapata mimba ni kwa heri.

“Lakini nitoe wito kwa vyombo vya dola. Kwa sababu watakuja wengine watauliza, Je wanaowapa mimba wanafunzi vipi? Wanaowapa mimba kama ni mwanafunzi au mtu wa nje, sheria ipo. Kuna miaka 30 inawasubiri.

“Kama ni mwanafunzi, huyu atakwenda kulea mtoto wake, hutu atakwenda kutumikia miaka 30. Na mashamba tumeyafungua mengi. Zile nguvu alizozitumia kuzaa mtoto akazitumie kulima. Akitoka kule baada ya miaka 30, sisi tumepata mpunga wetu na yeye nguvu zimeishapungua, inawezekana atabaki na huyo huyo mtoto.

“Lakini kusema mtu amezaa, arudi shuleni, halafu awe anawahubiria wenzake, ‘unajua ilikuwa hivi, nilijaribu hivi hivi tu, na kuzaa ni rahisi tu,’ wenzake nao watatamani nao wakazae, halafu baadae warudi shuleni. Watu wa ajabu sana. Hatuwezi tukalipeleka Taifa hili katika maadili ambayo hayapo. Never (haiwezekani).

“Lakini, hao wanaowatetea wazazi, hawazuiliwi kuanzisha shule zao. Hizi NGO wanajilipa hela nyingi kutoka kwa hao wanaowafadhili. Wakafungue shule za wazazi kwa kutumia fedha hizo. Kwani wakifungua shule hapo ya private (shule binafsi), kwa ajili ya wanafunzi wote wenye watoto wakasomesha tutawazuia?

“Wakijaribu, ndipo watagundua kuwa, mwanafunzi mwenye mtoto akishaanza kufanya hesabu mbili mara mbili, hata kabla hajajibu, atamwambia mwalimu, ‘nakwenda kunyonyesha mtoto wangu namsikia huko analia.’

“Hizi NGO zikafungue shule za wazazi. Sio zilazimishe serikali. Ninatoa pesa ya bure hapa, kwa ajili ya kusomesha watoto, wanafunzi ambao wameamua kwenda kusoma, halafu nikasomeshe na wazazi?

“Kwa hiyo Mama Salma nakupongeza. Ulisimama na kulizungumza Bungeni. Endelea hivyo hivyo. Sisi sote tuna watoto. Hata kama mimi nina mtoto wangu wa kike, akapate mimba huko halafu tena nimpiganie kurudi shuleni? Waende wakafanye halafu wataona kama nitawarudisha shuleni.

“Ni lazima tufike mahali ndugu zangu Watanzania tushtuke. Hawa wanaotuletea haya mambo msifikiri wanatupenda sana. Wametuletea madawa wa kulevya, watoto wetu unawakuta wanatoa makamasi tu. Hawawezi wakalima, hawawezi wakafanya nini, wao wanashangilia.

“Wametuletea watu kubakana, wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake, wakati hata ng’ombe na hata mbuzi haziwahi kukosea huo mtindo. Huwezi ukamwona mbuzi, anafanya hivyo.

“Nyie wachungaji mmeshawahi kuchunga. Mmeshawahi kuona hata ng’ombe anakosea? Au mbuzi? Au kondoo? Hata nguruwe au mnyama yeyote? Lakini tunaambiwa sisi Watanzania tuwe tunakosea mahali penyewe. Ni ujinga ni upumbavu.

“Kwa hiyo, ni lazima tufike mahali Watanzania tujitambue. Tumwogope Mungu. Tujirekebishe. Haya mambo ya ku-copy copy (kuigaiga) tutakuja ku-copy (kuiga) na mambo ya ajabu. Na saa nyingine wanaleta mambo haya kwa njia ya michango michango na misaada. Wanasema tutakusaidia hiki. Kumbe na hayo wanayotusaidia ni mali zetu zimetoka huku.

“Unajua ni lazima tujanjaruke, tujitambue basi ndugu zangu Watanzania. Tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe. Tanzania imebarikiwa na mwenyezi Mungu, ni tajiri mno. Tajiri! Na ndio maana napongeza watendaji na viongozi wa chama changu ambao wamekuwa wasimamizi wazuri wa maadili ya Watanzania.

“Niwaombe ndugu zangu wa Bagamoyo tuendelee kusimama hivyo.Tutafika na Mungu atatusaidia. Saa nyingine tunapata laana ya ajabu kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume cha maumbile yetu. Yaani unang’ang’ania tu mahali ambapo hapastahili! Tabu sana, baghosha!

“Ninazungumza haya kwa sababu niko kwa watani zangu. Maana ningezumza haya mahali pengine wangesema, ‘mnamwona huyu Rais na kauli zake!’ Lakini, ni nafuu kuongelea aibu ili kuondoa aibu. Tukiichekea aibu itatumaliza.

“Na hapa kwa sababu kuna vijana ni lazima tuwaenzi, tuwaeleze. Na niwaombe vijana, wa maeneo haya Bagamoyo, tuchape kazi. Vya bure havipo. Nafasi imeishapatikana ya kuwa na viwanda vingi. Serikali inatengeneza mazingira mazuri ya kuwa na umeme, maji, ili tuvitumie hivi kwa ajili ya kujenga Tanzania yetu. Sisi wazee tutaondoka mtabaki nyinyi.

“Mjipange kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya. Tanzania yenye mwelekeo. Tanzania yenye maendeleo. Mimi urais huu ni wa temporary (urais unapita).

“Pamekuwepo na marais wangapi? Alikuwepo Nyerere, amekuka Mwingi, amekuja Mkapa, amekuja mzee Kikwete, na mimi baadaye nitakuwa mzee, watakuja wengine. Lakini, katika kipindi hiki lazima niwaeleze yale ambayo nina wajibu wa kuyaeleza.

“Bagamoyo oyee! Jamani nilikuja hapa kuzindua mradi. Lakini nafikri message sent and delivered (ujumbe umetumwa na umefika).”



NYIE Hangaikeni na vipost post vyenu ila maamuzi haya hakuyafanya JPM yalishakuwepo na hata angeanzisha yeye it is a right move to make...shuleni ni mahala pa kwenda kusoma sio kujifunza ngono...ikikuuma fungua shule sebuleni kwako.
 
NYIE Hangaikeni na vipost post vyenu ila maamuzi haya hakuyafanya JPM yalishakuwepo na hata angeanzisha yeye it is a right move to make...shuleni ni mahala pa kwenda kusoma sio kujifunza ngono...ikikuuma fungua shule sebuleni kwako.
.
Kwani, wewe alianza kufanya ngono ukiwa na miaka mingapi? Ndani ya ndoa yako, umeshampa mimba mkeo mara ngapi bila kukusudia? Yeye JPM anao watoto wangapi nje ya ndoa na ambao hakukusudia wazaliwe? Think bing man....
 
Kwa upuuzi Kama huu sijui mnatetea mini?
.
Unachanganya maembe na machungwa. Ngoma hizo ni kipindi rasmi--extra curricular activities. It all depends on how it is supervised. Hiyo lakini sio mada hapa...
 
Mwenywe mwanzoni nilikuwa nampinga Magufuli lakn saiv namuunga...hao watoto watajifunza kusema nooo...pengine iangaliwe sheria ya incase under18 kabakwa...ila above wote hta kam yuko primary ni lwake anajua kutoa huyo
 
.
Kwani, wewe alianza kufanya ngono ukiwa na miaka mingapi? Ndani ya ndoa yako, umeshampa mimba mkeo mara ngapi bila kukusudia? Yeye JPM anao watoto wangapi nje ya ndoa na ambao hakukusudia wazaliwe? Think bing man....

Nabii Suleimani alikuwa na wanawake wangapi wa ndoa na nje ya ndoa?? na kitabu chako cha dini kinakwambia unatakiwa kuwa na wake wangapi?? wengi wa kikosea haifanyi kosa kuwa halali
 
Nabii Suleimani alikuwa na wanawake wangapi wa ndoa na nje ya ndoa?? na kitabu chako cha dini kinakwambia unatakiwa kuwa na wake wangapi?? wengi wa kikosea haifanyi kosa kuwa halali
.
Kumbuka:
  • Every verse in the Bible is inspired-Cathechism
  • Note even a single letter is mutable--Jesus
Hivo, nikimfuata Nabii Suleimani ni sawa
 
Nauliza.... hizo pesa za bajeti ni za mtu binafsi so anaamua cha kutumia na huyu apate na huyu asipate kisha? Na yeye pia anafurahia utamu wake kkuzila... na kama raia wamechukizwa na kitendo hicho kwani watoto wakikosa wanatakiwa waadhibiwe maisha yao yote? Imagine mtu huyu apewe Umungu atateketeza Wanadamu kwa Siku moja hana wema mtu huyu na hakuwahi kuwa mtu mwema
 
Back
Top Bottom