Magufuli akumbwa na kashfa nzito!

Magufuli akumbwa na kashfa nzito!

Status
Not open for further replies.
Magufuli ni JEMBE, mtapoteza muda bure kudunduliza skandali dhidi ya huyu jamaa, mbona mawaziri vilaza cc wako wengi tu, nendeni huko mkafunge magoli!
Akiiba asisemwe? Nafikiri upinzani unafanya vizuri haumwonei mtu kwao rafiki ni mtu mwadilifu ukiwa fisadi lazima utamulikwa tu ,
 
  • Thanks
Reactions: why
Huyu mwizi wa kutaja takwimu za uongo kila siku sasa kakutana na visiki chadema wananaenda mpaka field kuhakiki we chezea CHADEMA. MAGUFULI SIO ISHU JAMANI MANA UKUANGALIA JINSI ALIVYO JASIRI KUTAJA MLOLONGO WA TAKWIMU UNAWEZA FIKIRI MKWELI, MWAKA JANA AALITAJA FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA ZA DSM PEMBEZONI KWA KUTAJA FEDHA KWA MAMILIONI LAKINI LEO HAKUNA BARABARA ILIYOJENGWA MPAKA SASA, HIVO WATANZANIA TUWE MAKINI KWA KUWA MASOMAJI WA UTEKELEZAJI WA AHADI ZA SERIKALI, MIMI SITAKI KUAMINI DAIMA BILA KUHAKIKI UHALISIA HIVO NAOMBENI TUWE MAKINI SANA NA PROPAGANDA ZA MAGUFULI, UTAFITI WANGU UNANIAMBIA NI ASILIMIA 90 YA ANAYOSEMA MAGUFULI NI UONGO TUPU ILA ANAAMINI WOTE HUAKAA NA KUAMINI HAYO.
 
Hii imetoka kwenye hotuba ya kambi ya upinzani. Sehemu hii inaonyesha ubadhirifu wa fedha kwenye wizara iliyooko chini ya Dr John Pombe Magufuli. Mheshimiwa Spika,baada ya fedha hizi kupunguzwa kiasi cha shilingi bilioni 95 na kupelekwa wizara ya uchukuzi zilibakia kiasi cha shilingi bilioni 252.975 katika kifungu hiki, leo tumelazimika kulikumbusha Bunge kuhusiana na suala hili kwani kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka husika wa fedha kuhusiana na kifungu hiki alisema, naomba kunukuu ¡°malipo ya madeni ya mwaka wa nyuma yaliyolipwa kwa fedha za 2011/2012 kwa kutumia jina la mradi usiohalisi hs.252,975,000,000. Miradi katika wizara ilipewa namba 4168 kwa ajili ya kupitisha malipo ya madeni ya miaka ya nyuma kwa miradi inayotekelezwa na TANROADS. Namba hii sio halisi¡± (chanzo: taarifa ya CAG uk.160,fungu 98) Mheshimiwa Spika,fedha hizi ¡°zilizopotea¡±au ¡°kulipwa kifungu hewa¡± ni sawa na fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya barabara ifuatazo kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014; i. Barabara ya Usagara-Geita-Kyamyorwa (KM 422) ii. Barabara ya Kigoma-Kidahwe-Uvinza- Kaliua-Tabora (KM 443) iii. Barabara ya Nangurukuru-Mbwemkulu (KM 95) iv. Barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port (KM 112) v. Barabara ya Manyoni-Itigi-Tabora (KM264) vi. Barabara ya Tabora-Ipole-Konga-Mpanda (KM 359) vii. Barabara ya Kidatu-Ifakara-Lupilo-Malinyi- Londo-Lumecha/Songea(KM- 396) viii. Kuondoa msongamano barabara za Dar (KM- 102.15) Aidha, ni sawa na kusema kuwa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 316.218 imepotea kwa kutumia mahesabu ya wizara ya ujenzi kuwa kilomita moja ya lami inajengwa kwa kiasi cha shilingi milioni mia nane (800,000,000), hii ni sawa na kusema kuwa barabara ya kutoka Manyoni-Itigi-Tabora (KM 264) Changanya na barabara ya kutoka Chunya ¨C Makongorosi (KM 43) na Barabara ya Tangi Bovu ¨CGoba (KM 9), zimepotea kutokana na ufisadi huu. Chanzo: hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa msaada Marcossy Albane. Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
narudia tena na tena kuwa ndani ya CCM hakuna alie msafi!
 
jamaa huwa msanii mbele ya vyombo vya habari lakini hakunaga mrejesho.... naweza kukuaibisha mbele ya media badae anakuomba msamaha. anakwambia its politics...

Huwa anaongeza kilometer zake za uongo alafu anachota billions of money.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kwenye vivuko amesema hivi,

1. Shilingi bilioni 3 kununua kivuko kitakachofanya kazi kati ya Dar ES Salaam -Bagamoyo

2. Ujenzi wa maegesho mwambao mwa Bahari ya HIndi katika maeneo ya Magogoni na RUngwe oceanic shilingi bilioni 2.5

fedha zote hizi zipo kwenye fungu 4125 na jumla kwenye kifungu hiki zimetengwa bilioni 5.990.....tafakarini

Magufuli amehakikisha JK na famalia yake inanyonya uchumi wa tanzania mpaka tone la mwisho.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
mi tangia jamaa alivyogawa nyumba za umma kwa bei ya kashata ndipo nilipoanza kumdoubt magufuli hakika aliifirisi taifa yeye na ben hadi moja ben kageuza ofisi yake ya ben hiv foundation masaki maskini tanzania.
 
huu ni uzushi, hakuna ukweli wowote hapo...hizi ni takwimu za kupakana matope na hazitafanikiwa

Mkuu, Jinsi Ulivyo na Mapenzi na CCM, huambiwi wala husikii, Naamini siku ukiambiwa kuwa Mkeo ana Mimba ya Mwigulu/Magufuli ama Nape ama Aden Rage kama sio Kinana, still Bado utabisha Mwanzo Mwisho
 
Hii ni wizara ambayo kwa miaka minne mfululizo imekuwa ikitengewa zaidi ya shilingi trilioni moja nuka tatu kila mwaka, hivyo watu wakiona makandarasi wanafikiri ni Magufuli, mbona alipokuwa kule samaki aliishia kukamata meli ya uvuvi na hakuweza hata kuboresha chuo cha uvuvi? Simply alikuwa hana fedha,

leo akisemwa ni haki maana anajisahau na kufikiri kuwa fedha za barabara hazina mwenyewe .....,
 
mtahangaika sana kumchafua pombe lakini itawamwagikia tu na mtanuka wenyewe

Huku si kumchafua.... mtu akisemwa ... muhimu ni je linalosemwa lina ukweli au la.... tuache unazi kwenye mambo ya umma... tupe taarifa za kama anasingiziwa au la... ndo tunataka tusikie hapa..... hakuna aliye MALAIKA...
 
Barabara anazojenga Magufuli zote hazina viwango, mashimo baada ya miezi miwili huku gharama za kujenga ziko juu (800,000,000 kwa kilomita moja). Huyu jamaa utasikia anapigiwa chapuo la kuwa rais kwa huu ubabaishaji na maCCM wenzie. CCM hakuna mwenye afadhali jamani, ngoja tusubiri utetezi wake kwa hizo hela alizokwapua

Nani kapita barabara ya Bwanga Chato hivi karibuni.....!!!!!
 
Hapo nadhani kuna technicalities juu ya ulipaji wa madeni na wala si ubadhirifu. Nasikia miaka ya karibuni serikali imekuwa ikiingia katika madeni makubwa na wakandarasi. Nitapenda kusikia ufafanuzi toka kwa Waziri wa Ujenzi Dr. John Joseph Pombe Magufuli wakati anahitimisha uchangiaji kwenye hotuba yake pamoja na wakati wa kupitisha bajeti kifungu kwa kifungu! Magufuli kama amekula MUKU vile manake akisimama kuongea hata kama ulikuwa unataka kumkamata pabaya unalegea na kumuacha atiririke. Ataanza kuongea kwa taratibu huku akiwa kama anaonyesha kuonewa kisha atashuka na data na kutaja barabara ambazo zipo kwenye jimbo la mbunge husika na mwisho kuwaambia niacheni nifanye kazi; hapo tena kila mtu kimya na matokeo yake ni kumuomba aangalie na barabara zao.

Magufuli kiboko; leo mtamsikia atakavyopangua hayo yote!

Hata kama unampenda mtu kiasi gani sifa lazima ziwe na reservation. Kama kweli anazo data mbona hata siku moja hajawahi kutushawishi kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali? Mbona ndugu yake na nyumba ndogo waliingizwa kwenye mgao hajawahi kukanusha with such cooked data. Wlatini wana msemo "qui omne dict nihil excludit" anayeongea kila kitu hatofautishi kitu. Sio kila mashahiri yake yana maslahi kwa taifa
 
Hata kama unampenda mtu kiasi gani sifa lazima ziwe na reservation. Kama kweli anazo data mbona hata siku moja hajawahi kutushawishi kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali? Mbona ndugu yake na nyumba ndogo waliingizwa kwenye mgao hajawahi kukanusha with such cooked data. Wlatini wana msemo "qui omne dict nihil excludit" anayeongea kila kitu hatofautishi kitu. Sio kila mashahiri yake yana maslahi kwa taifa

Kuhusu kuuza nyumba za serikali Magufuli alilishawishi Baraza la Mawaziri na wakaridhia kwa sababu ambazo alizitoa.
 
Kuhusu kuuza nyumba za serikali Magufuli alilishawishi Baraza la Mawaziri na wakaridhia kwa sababu ambazo alizitoa.
Na wewe umeshawahi kushawishika kuhusiana na uuzwaji ule? Sababu zake zimewahi kukushawishi wewe au kwa vile walikuwa kundi la walaji wakakubaliana pamoja? Kana kwamba wakiondoka na Ben ndio mwisho wa uwepo wa serikali na viongozi wake , wakauza mpaka nyumba za OCD ndani ya vituo vya polisi kana kwamba ndio mwisho wa kuwa na OCD kwenye vituo hivyo, wameuza mpaka makazi ya SPika , kana kwamba hatakuwepo mwingine leo tunajenga kwa mabilioni wakkati waliuziana kwa bei chee......
 
Baada ya kuuziana nyumba leo ameomba kutengewa kiasi cha shilingi bilioni 2.245 kwenye bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya kujenga nyumba za viongozi wa serikali , baada ya kuuziana zile za awali leo anaomba fedha ambayo ingeelekezwa kwenye miradi ya maji.....
 
Na wewe umeshawahi kushawishika kuhusiana na uuzwaji ule? Sababu zake zimewahi kukushawishi wewe au kwa vile walikuwa kundi la walaji wakakubaliana pamoja? Kana kwamba wakiondoka na Ben ndio mwisho wa uwepo wa serikali na viongozi wake , wakauza mpaka nyumba za OCD ndani ya vituo vya polisi kana kwamba ndio mwisho wa kuwa na OCD kwenye vituo hivyo, wameuza mpaka makazi ya SPika , kana kwamba hatakuwepo mwingine leo tunajenga kwa mabilioni wakkati waliuziana kwa bei chee......

Kwenye uuzaji wa nyumba nina reservation kadhaa hasa linapokuja eneo la location. Hata kama nyumba zilikuwa mbovu lakini wasingekubali kuuza locations ambazo zilikuwa strategically kwa ajili ya makazi ya viongozi. Kwangu mimi tatizo si kuuziana nyumba tatizo ni maeneo ambayo nyumba hizo zilikuwepo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom