Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,952
- 10,037
kwa hiyo kashfa iko wapi hapo? si usubiri ufafanuzi wa waziri wakati wa majumuisho
Hapo nadhani kuna technicalities juu ya ulipaji wa madeni na wala si ubadhirifu. Nasikia miaka ya karibuni serikali imekuwa ikiingia katika madeni makubwa na wakandarasi. Nitapenda kusikia ufafanuzi toka kwa Waziri wa Ujenzi Dr. John Joseph Pombe Magufuli wakati anahitimisha uchangiaji kwenye hotuba yake pamoja na wakati wa kupitisha bajeti kifungu kwa kifungu! Magufuli kama amekula MUKU vile manake akisimama kuongea hata kama ulikuwa unataka kumkamata pabaya unalegea na kumuacha atiririke. Ataanza kuongea kwa taratibu huku akiwa kama anaonyesha kuonewa kisha atashuka na data na kutaja barabara ambazo zipo kwenye jimbo la mbunge husika na mwisho kuwaambia niacheni nifanye kazi; hapo tena kila mtu kimya na matokeo yake ni kumuomba aangalie na barabara zao.
Magufuli kiboko; leo mtamsikia atakavyopangua hayo yote!