"dr magufuli aagiza makandarasi kukamatwa
na john maduhu
mwanza
waziri wa ujenzi,dr john magufuli ameagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuwaweka ndani mkandarasi wazembe wanaopewa kazi na kushindwa kuzifanya kwa wakati.
amesema kwa kuwa makandarasi hao wanaonekana kuwa kikwazo njia pekee ya kurejeshaheshima katika kazi ni kuwaweka ndani japo kwa saa sita kwa kuwa wanajenga barabara chini ya kiwango."
mtanzania,januari 5,2011
the gentleman is at it again, cheap populist soft targets.
katika mikataba ya ujenzi inayotayarishwa na serikali, mkandarasi mzembe anavifungu vinavyombana kutekeleza kazi kwa viwango vinavyotakiwa.
Sasa hili la kuwaweka ndani wakandarasi ni la kushangaza!
Tunategemea dr magufuli aanza yeye kwa kuwaweka ndani wasimamizi na wakandarasi wa kilwa rd.kazi imefanywa chini ya viwango wakati wahandisi wa wizara walikuwepo na hata leo wapo, hawajafa.
Dr magufuli awaweke ndani hawa.
Sakata la mrema linaishaje, dr magufuli atayarishi lupango ya kumweka mrema wa tanroads, ama sivyo hataeleweka.
Msata-bagamoyo je?
Dr magufuli atayarishe selo ya mkandarasi aliyepewa kazi hiyo,takopa, wa kikorea ili tuweze kumwelewa.
Udhaifu wa mikataba mingi ya ujenzi msingi wake uko katika watayarishaji na wasimamizi wenyewe ndani ya wizara husika za ujenzi na halmashauri.
Suala la rushwa ndio usiseme.
Mchawi wa matatizo ya ujenzi iko huko huko mawizarani ikiwa ni pamoja na ni ukosefu wa usimamizi imara wa miradi yenyewe.
Zaidi ya yote namshauri dr magufuli kusoma mikataba ya ujenzi, kitu ambacho inaelekea hakielewi vema.