Magufuli aanza kulewa madaraka?

Magufuli aanza kulewa madaraka?

"Dr Magufuli aagiza makandarasi kukamatwa
Na John Maduhu
Mwanza
Waziri wa Ujenzi,Dr John Magufuli ameagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwaweka ndani mkandarasi wazembe wanaopewa kazi na kushindwa kuzifanya kwa wakati.
Amesema kwa kuwa makandarasi hao wanaonekana kuwa kikwazo njia pekee ya kurejeshaheshima katika kazi ni kuwaweka ndani japo kwa saa sita kwa kuwa wanajenga barabara chini ya kiwango."
MTANZANIA,Januari 5,2011

The gentleman is at it again, cheap populist soft targets.
Katika mikataba ya ujenzi inayotayarishwa na serikali, mkandarasi mzembe anavifungu vinavyombana kutekeleza kazi kwa viwango vinavyotakiwa.
Sasa hili la kuwaweka ndani wakandarasi ni la kushangaza!
Tunategemea Dr Magufuli aanza yeye kwa kuwaweka ndani wasimamizi na wakandarasi wa Kilwa Rd.Kazi imefanywa chini ya viwango wakati wahandisi wa Wizara walikuwepo na hata leo wapo, hawajafa.
Dr Magufuli awaweke ndani hawa.
Sakata la Mrema linaishaje, Dr Magufuli atayarishi lupango ya kumweka Mrema wa TANROADS, ama sivyo hataeleweka.
Msata-Bagamoyo je?
Dr Magufuli atayarishe selo ya mkandarasi aliyepewa kazi hiyo,TAKOPA, wa Kikorea ili tuweze kumwelewa.
Udhaifu wa mikataba mingi ya Ujenzi msingi wake uko katika watayarishaji na wasimamizi wenyewe ndani ya Wizara husika za Ujenzi na Halmashauri.
Suala la rushwa ndio usiseme.
Mchawi wa matatizo ya ujenzi iko huko huko mawizarani ikiwa ni pamoja na ni ukosefu wa usimamizi imara wa miradi yenyewe.
Zaidi ya yote namshauri DR Magufuli KUSOMA mikataba ya Ujenzi, kitu ambacho inaelekea hakielewi vema.

Hapa mkuu nakubaliana na wewe kuwa Magufuli anataka kuvuka mipaka!

Magufuli anaelewa vyema masuala ya ukandarasi, anajua sheria zinazotawala biashara ya ukandarasi. Haya ya kuweka watu ndani ni matumizi mabaya ya madaraka.

Katika utendaji mbovu wa wakandarasi si tu chanzo ni wakandarasi saa nyingine ni viongozi wa serikali wanaochuka rushwa na kupitisha makandarasi wasio na uwezo!

Hivi tujiulize Mkandarasi kama Richmond alivyoshidwa kuperform, je njia sahihi ilikuwa kuwaweka ndani Richmond au ni kuwaweka ndani wale walioipa kazi huku wakijua wazi ni wababaishaji?????
 
..ubabe wake kule Mwanza ulisababisha hasara ya shilingi bilioni 14.

..hiyo ni hasara kubwa kuliko ile ambayo ilimtia matatizoni Nalaila Kiula.
 
Nakwambia Magufuli hajawahi kuwa na akili, kama angekuwa nazo asingekubali kuongozwa na watu wenye akili ndogo kama JK, angechukua fomu siku nyingi!!!!! Lakini yeye anaona Jk bonge la raisi anamnyenyekea na kujikomba kwake ili apewe viuwaziri........
siachi kusema,.....kajigawia nyumba ya NHC Boko kififadi yeye pamoja na mafisadi wengine mnao wajua...
 
Inaelekea huyu muanzisha thread alifurahia 'utendaji' (more so the lack of it) wa Shukuru Kawambwa.

Sasa upele umepata mkunaji.

Kama ww ni mkandarasi, sasa hakuna kulala. Fanya kazi vizuri mambo yatakuwa super tu.

Au ndiyo mambo ya RA kuelekea 2015?

Keep it up Dr Magufuli (PhD)!
 
"Dr Magufuli aagiza makandarasi kukamatwa
Na John Maduhu
Mwanza
Waziri wa Ujenzi,Dr John Magufuli ameagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwaweka ndani mkandarasi wazembe wanaopewa kazi na kushindwa kuzifanya kwa wakati.
Amesema kwa kuwa makandarasi hao wanaonekana kuwa kikwazo njia pekee ya kurejeshaheshima katika kazi ni kuwaweka ndani japo kwa saa sita kwa kuwa wanajenga barabara chini ya kiwango."
MTANZANIA,Januari 5,2011

The gentleman is at it again, cheap populist soft targets.
Katika mikataba ya ujenzi inayotayarishwa na serikali, mkandarasi mzembe anavifungu vinavyombana kutekeleza kazi kwa viwango vinavyotakiwa.
Sasa hili la kuwaweka ndani wakandarasi ni la kushangaza!
Tunategemea Dr Magufuli aanza yeye kwa kuwaweka ndani wasimamizi na wakandarasi wa Kilwa Rd.Kazi imefanywa chini ya viwango wakati wahandisi wa Wizara walikuwepo na hata leo wapo, hawajafa.
Dr Magufuli awaweke ndani hawa.
Sakata la Mrema linaishaje, Dr Magufuli atayarishi lupango ya kumweka Mrema wa TANROADS, ama sivyo hataeleweka.
Msata-Bagamoyo je?
Dr Magufuli atayarishe selo ya mkandarasi aliyepewa kazi hiyo,TAKOPA, wa Kikorea ili tuweze kumwelewa.
Udhaifu wa mikataba mingi ya Ujenzi msingi wake uko katika watayarishaji na wasimamizi wenyewe ndani ya Wizara husika za Ujenzi na Halmashauri.
Suala la rushwa ndio usiseme.
Mchawi wa matatizo ya ujenzi iko huko huko mawizarani ikiwa ni pamoja na ni ukosefu wa usimamizi imara wa miradi yenyewe.
Zaidi ya yote namshauri DR Magufuli KUSOMA mikataba ya Ujenzi, kitu ambacho inaelekea hakielewi vema.

Siwezi kumsamehe Magufuri kwa kuuza nyumba za serikali tena kwa bei ya kutupa
 
Magufuli ni mlevi wa madaraka siku zote, na ameingizia nchi kwenye matatizo makubwa. Alivunja Nyumba Mwanza na serikali ikaamriwa kulipa. Alitoa nyumba na kumuuzia mtu asiyestahili, aktetea sehemu ya wazi kumilikiwa na mtu binafsi-Rose \garden- hivyo kuilazimish serikali kulipa fidia pale itakapo dhamiria kupanua barabara, na hivi karribuni ametutia kwenye matumizi makubwa na samaki wake. Wakati wote huu sisi tunampongeza na kusifu utendaji wake!!!
 
does Lole Gwakisa have to say more...?
 
does Lole Gwakisa have to say more...?

Ha ha ha Mkuu LAT!
It is quite obvious now that Dr Magufuli-the chemical don, is polishing his apple the wrong way.
From contributors in this thread the pros and cons of locking away "makansdarasi" and refreshing their liberty after six hours is a cheap ploy at self popularity gratification.
My challenge to the self styled Dr Pombe is to ahead and lock up TAKOPA, Mrema and KAJIMA.
I doubt if he has the balls to do just that, and if he does I will be the first chap to congratulate him.
 
This Magufuli guy is a bomb; bomb; bomb. He is disaster to the road construction industry bin Tanzania!
 
Mkuu kuwa mkali bila kuelewa sheriana mikataba yenyewe ni kama unguided missile!
Mie nampa changamoto Dr Magufuli awaweke ndani TAKOPA na KAJIMA.
Na Mrema Vipi mbona bado anapeta?

Kama mnajua sheria za mikataba tusaidieni tusilipe sh. bilioni 185 kwa Dowans. Acheni sound!!!!!
Shida ya watanzania ni barabara zenye kiwango, sasa kama contractors watawekwa ndani ili wajenge hizo barabara kwa ubora na wakati, sitojali sana.
Kwa katiba (mbovu) ya sasa mkuu wa mkoa anaweza kukutia ndani bila kukupa maelezo yoyote.
 
aktetea sehemu ya wazi kumilikiwa na mtu binafsi-Rose \garden- hivyo kuilazimish serikali kulipa fidia pale itakapo dhamiria kupanua barabara,

Rose garden kuna structure gani ya maana pale ukilinganisha na mijumba ilojengwa mita chache toka barabarani.

Rose Garden road ni barabara kuu au ya mtaa?? So future plans ni kuifanya dual carriage, right??

Rose Garden ni sehemu ya wazi toka lini???

Think twice maaaaaaaaan!!
 
Inaelekea huyu muanzisha thread alifurahia 'utendaji' (more so the lack of it) wa Shukuru Kawambwa.

Sasa upele umepata mkunaji.

Kama ww ni mkandarasi, sasa hakuna kulala. Fanya kazi vizuri mambo yatakuwa super tu.

Au ndiyo mambo ya RA kuelekea 2015?

Keep it up Dr Magufuli (PhD)!

Nimekwisha sema mimi si mkandarasi bali mdau wa mikataba ya ujenzi
Na nukuu my post no 52 kwa faida yako:

Mimi si mkandarasi lakini Law of Contract naifahamu vizuri sana.
Kwa jinsi Law of Contract kwa minajili ya ujenzi inavyoendeshwa nchi hii mkataba standard upo wizara ya ujenzi na ndio unaotumika katika miradi yote ya ujenzi, iwe Halmashauri au Serikali Kuu.

Nimefarijika kuona michango iliyoenda shule, kama vile Gaijin anavyohoji.
Contract au Mkataba wa Ujenzi una sehemu kuu nne:
-Conditions of contract-mazingira ya nayohusu utekelezaji wa mradi
-Specifications-viwango vya utekelezaji kazi
-Drawings- michoro yote ya ujenzi
-Bills of Quantities-gharama ya kazi pamoja na hesabu ya vifaa vyote.
Kunaweza kuwa na kipengere cha Specific Conditions ambazo ni mahsusi kwa mradi husika.

Mkandarasi hapo anabanwa tena vipengele viko wazi kabisa juu ya adhabu za kuchukuliwa asipotekeleza kufuatana na viwango vya kazi.
Adhabu hizi ziko katika Conditions of Contract ambazo Mwenye kazi na Mkandarasi wanaekeana sahihi.

Pengine Dr Magufuli hajui kwamba vifungu hivi vipo ndani ya mikataba hii, lakini vipo wazi.
La msingi hapa ni usimamizi mbaya na usioridhisha katika mikataba karibu yote ya ujenzi.Mkandarasi si malaika usipomsimamia lazima atatumia mwanya kimkatabakukuibia.
Mbaya zaidi kama mtoa kazi hajui mkataba wenyewe unasema nini.
Tumemsifia sana Dr Magufuli kwa kuanza kuisafisha TANROADS lakini uozo uliopo katika mikataba yake wizarani pamoja na kukosa kabisa usimamizi AU rushwa ndio tunaona matokeo yake.

Sasa mkuu ujenzi sio politics, aidha unaijua au huijui.
Dr Magufuli anatakiwa kuonyesha usomi kwa kutumuia taratibu za ujenzi zilizopo na zinazijitosheleza kiutendaji.
Matatizo anayoyaona ni sehemu tu ya rushwa,ukosefu wa usimamizi na uvivu tu wa watendaji wake.
Hii ya kukurupuka kuwaweka ndani makandarasi ndo inaleta changamoto ya yeye kuwa wa kwanza kurusha jiwe-kwa kuwaweka ndani TAKOPA,KAJIMA na Mrema wa TANROADS.
 
Back
Top Bottom