Magufuli aanza kulewa madaraka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli aanza kulewa madaraka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, Jan 5, 2011.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  "Dr Magufuli aagiza makandarasi kukamatwa
  Na John Maduhu
  Mwanza
  Waziri wa Ujenzi,Dr John Magufuli ameagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwaweka ndani mkandarasi wazembe wanaopewa kazi na kushindwa kuzifanya kwa wakati.
  Amesema kwa kuwa makandarasi hao wanaonekana kuwa kikwazo njia pekee ya kurejeshaheshima katika kazi ni kuwaweka ndani japo kwa saa sita kwa kuwa wanajenga barabara chini ya kiwango."
  MTANZANIA,Januari 5,2011

  The gentleman is at it again, cheap populist soft targets.
  Katika mikataba ya ujenzi inayotayarishwa na serikali, mkandarasi mzembe anavifungu vinavyombana kutekeleza kazi kwa viwango vinavyotakiwa.
  Sasa hili la kuwaweka ndani wakandarasi ni la kushangaza!
  Tunategemea Dr Magufuli aanza yeye kwa kuwaweka ndani wasimamizi na wakandarasi wa Kilwa Rd.Kazi imefanywa chini ya viwango wakati wahandisi wa Wizara walikuwepo na hata leo wapo, hawajafa.
  Dr Magufuli awaweke ndani hawa.
  Sakata la Mrema linaishaje, Dr Magufuli atayarishi lupango ya kumweka Mrema wa TANROADS, ama sivyo hataeleweka.
  Msata-Bagamoyo je?
  Dr Magufuli atayarishe selo ya mkandarasi aliyepewa kazi hiyo,TAKOPA, wa Kikorea ili tuweze kumwelewa.
  Udhaifu wa mikataba mingi ya Ujenzi msingi wake uko katika watayarishaji na wasimamizi wenyewe ndani ya Wizara husika za Ujenzi na Halmashauri.
  Suala la rushwa ndio usiseme.
  Mchawi wa matatizo ya ujenzi iko huko huko mawizarani ikiwa ni pamoja na ni ukosefu wa usimamizi imara wa miradi yenyewe.
  Zaidi ya yote namshauri DR Magufuli KUSOMA mikataba ya Ujenzi, kitu ambacho inaelekea hakielewi vema.
   
 2. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135

  Sina uhakika kama unajua Magufuli alikuwa Waziri wa hiyo wizara in the 3rd phase. Sidhani kama amekurupuka. Otherwise, ibua issues za kuona ameingia kichwa kichwa. It sounds nawe ni kandarasi, sasa unahofia kukamatwa na kuwekwa ndani masaa sita.
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Tuseme ukweli wakandarasi wezi wa mchana!anapojenga chini ya kiwango au makubaliano si wizi huo?rushwa ipo sana katika barabara za wilayani vifusi tuu
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh!naona mkuu una chuki binafsi na huyu Dr Magufuli,kwa kabisa nimesikishwa na initial uliyoitumia Huyu anaitwa Dr Magufuli(PHD),na sio Magufuli.DR Magufuli ana uzoefu wa kutosha na makandalasi,yeye anajua kabisa makandalasi wengi ni wazembe,hivyo wakati mwingine hatua za kisheria uhitajika kuchukuliwa mara moja!!
   
 5. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  mughonile Gwakisa!!!! ughwe ghwa kyellaaaa ghwa tukuyu???
   
 6. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi namuunga mkono Magufuli, wakati mwingine tunawahitaji viongozi wa aina yake ili kuleta nidhamu katika kazi. Mkuu wa nchi alitakiwa awe mkali kiasi hiki na bila upendeleo mambo yetu yangekuwa shega sana
   
 7. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  no comment
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuuu,

  Me binafsi sidhani hata kidogo kuwa maghufuli kalewa madaraka, Kwani wizara nyingi humu nchini kwetu zina uchafu mwingi sana na pale anapotokea mtu jasili na kukemea basi kutakuwa na watu wa kukubeza au kukupinga kile ukifanyacho kwa ajili ya jamii kwa ujumla ile jamii kubwa ambayo mtetezi wake ndio mbunge wao.

  Kwa hiyo nadhani unatakiwa kurudi nyuma na kuangalia kuwa huyu jamaa alikuwa hiyo wizara na alipo ongoka ndio hiyo wizara ika dimbwi la wala rushwa na kujiamulia watakavyo karudi tuu watu wakaanza hoo maghufuli hawatendei haki wafanyakazi wake katika wizara ame jaaawa sana na uzalendo sasa mlitakanini nyie sindio mlio omba kazi wizarani huko maaana yake ni kujitolea na kuwa mzalendoo.

   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Wanapowekeana mikataba na wakandarasi kuna kipengele cha kuwaweka ndani kama hawajatimizima masharti yaliyowekwa?

  Na mkuu wa mkoa atamjuaje mkandarasi aliyefanya kazi chini ya viwango?

  Kama kazi haijatendwa kama inavyotakiwa basi sheria ifuate mkondo wake na adhabu stahili zitolewe na sio kuwaweka watu ndani kama hakuna vyombo vya sheria.
   
 10. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hata hao anaotaka kuwaweka ndani walianza kazi kabla ya awamu hii (aliyoteuliwa kuwa waziri wa wizara hii)!
   
 11. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ehe! mshutueni kabla hajaanza kulia na kukumbuka rafiki zake walio kufa !
   
 12. RR

  RR JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Blah blah blah......hivi bado mnasikiliza huyu mpiga tumba?
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu basi ingekuwa vema makandarasi waongozwe na Idara ya Polisi ili kieleweke!!
   
 14. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  unamaanisha kitu gani?
   
 15. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu kuwa mkali bila kuelewa sheriana mikataba yenyewe ni kama unguided missile!
  Mie nampa changamoto Dr Magufuli awaweke ndani TAKOPA na KAJIMA.
  Na Mrema Vipi mbona bado anapeta?
   
 16. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Magufuli kakurupuka siyo anayefanya mkataba na mkandarasi ni tanroads akishirikiana na wizara so wanaojua ubora wa hiyo kazi ni wizara na tanroards. Na hiyo mikataba sidhani kama ina maandishi ya ukishindwa kufanya kazi vizuri ntakuweka ndani kitu nachoamini kamwe hakuna mkataba wa namna hiyo. Navyojua mimi kazi ikiisha kuna kipindi cha uangalizi kabla ya makabidhiano ambacho huwa 12Month to 18 month na pia kuna kitu kinaitwa Construction Bond au Performance Bond inayotakiwa kila Contructor anunue ili apewe kazi na iwapo itafanyika ndivyo sivyo hapo kazi ya bond inatakiwa kul;ipa gharama zote alizoingia principal.

  Ukweli ni kwamba hapa ni kutafuta sababu za kupelekana ICC kisha tuje kulipa ya Dowans,.
  Tunataka Magufuli aende mbali zaidi amshtaki Mrema, atuonyeshe na nnani alikula pesa ya msata bagamoyo, kama ulikuwa hujui hii pesa imeliwa na CCM kupitia SUMA JKT walilipwa wao kinyume na taratibu maana wao hawakuwa mkandarasi kiongozi badala ya TAKOPA.
  Kukuhakikishia hilo wakati TAKOPA wanalalamikia kitendo hicho walipewa barabara nyingine wakae kimya na kuacha msata bagamoyo pasipo majibu.

  Sheria na kanuni zipo wazi kama mkandarasi afanyi kazi mnyang'anye kazi na usimpe tena kazi FULL STOP
   
 17. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Polisi wapo kwa manufaa ya chama na sio taifa.
   
 18. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Nchi hii bila kuwekana ndani mambo hayaendi, so kweli wawekwe tu ndani ili nidhamu ya kazi irudi.
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  'BARABARA HII IMEJENGWA KWA MSAADA WA WALIPAKODI WA JAPANI'ni moja ya matangazo nilokua nayaona along kilwa road,na mkandaras ni mjapani,so utamuwekaje ndani?nauliza
   
 20. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,769
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Ata mie nimehisi ivoivo atakua mkandarasi na yy ndio maana imemtouch sana!hii nchi haiendi bila viboko!wacha watiwe ndani tushachoka ss na upuuzi kila kukicha!watu wako sbb yao na familia zao tu!tia ndani hao asap!
   
Loading...