Magu: Watoto wawili wauawa na fisi wakienda shule

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,899
Haya yanatokea leo karne ya 21.

Screenshot_20230429-094146~2.jpg


Tunaweza vipi kuwa na huruma na wezi na wabadhirifu au matumizi mabaya (yasiyokuwa na ridhaa ya watu) ya mali za umma?

--------
Mwanza. Wanafunzi wawili wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ilumya wilaya ya Magu mkoani Mwanza wamefariki katika matukio mawili tofauti baada ya kushambuliwa na fisi wakati wakiwa njiani kwenda shuleni.

Matukio hayo yametokea Aprili 27 na 28, 2023 kati ya Saa 12 na Saa 1 asubuhi katika kijiji cha Ilumya wilayani humo, ambapo waliofariki ni Saraha Ncheye (7) mkazi wa kitongozi cha Sanganyika kijiji cha Nsola na Elizabeth Emmanuel wa kijiji cha Ilumya –Busega.

Sarah Ncheye ameuawa leo Aprili 28, 2023 katika kitongoji cha Kilulu baada ya kushambuliwa na fisi Saa 1 asubuhi wakati akienda shuleni ambapo alikuwa akisoma shule iliyo jirani na kijiji cha Ilumya wilayani Busega.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema Sarah alikutana na fisi huyo na kabla ya kushambuliwa alisikika akipiga kelele za kuomba msaada ndipo wakawahi eneo hilo na kumkuta fisi ameshamshambulia na kukimbia naye akiwa amemng’ata kichwani ananing’inia.

Kaka wa marehemu, Jackson Ncheye amesema alikuwa njiani anakwenda shambani kulinda mpunga dhidi ya ndege waharibifu ndipo akasikia mayowe kisha kumuona fisi anakimbia.

“Nilianza kumfukuza nikidhani amechukua mifugo, lakini baadaye nikaitwa na kukuta mdogo wangu ameshauawa baada ya kujeruhiwa vibaya kichwani na mikono,”amesema
Shuhuda mwingine, Mariam Leonard amesema “Nilikuwa nakwenda shambani kuchimba viazi nikakutana na fisi akiwa na mtoto anakimbia analia nikamkimbiza lakini akaanza kunifuata mimi nikakimbia kwenda kwa watu kuomba msaada wa kumuokoa, tulivyorudi tukakuta mtoto ameshafariki,”

Mwalimu wa shule ya msingi Ilumya, Stephano Mangilima amesema matukio hayo ya mara kwa mara yanasikitisha nakuwaomba wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule ili wasidhurike huku akiitaka Serikali ya kijiji kuwawinda wanyama hao.

“Ni tukio la kuhuzunisha na kushangaza, mtoto alikuwa na maendeleo mazuri darasani, wito wangu kwa wazazi kwakuwa matukio haya yanajirudia tuombe wanaoishi maeneo ya mbali watu wazima wawe wanawasindikiza watoto shuleni na viongozi wa vijiji watafute njia mbadala za kumaliza tatizo hili kwani tutaendelea kupoteza watoto,” amesema Mangilima
Mwenyekiti wa kijiji cha Nsola, Damian Kabudu amesema baada ya kupata taarifa za kushambuliwa kwa mtoto huyo aliyekuwa amejeruhiwa vibaya kichwani huku kiganja chake cha mkono wa kushoto kimekatwa, aliwajulisha idara ya wanyamapori ambao walifika na kutoa msaada wakishirikiana na wananchi.

Diwani wa kata ya Lubugu, Lucas Ntingi amesema matukio ya fisi kuwashambulia watoto yameongezeka katika vijiji vya Nsola na Ilumya ambapo Aprili 24 mtoto, Paul Elias (5) alishambuliwa na fisi katika Kijiji cha Nsola na anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Magu, huku akizitaka mamlaka kuwawinda fisi hao ambao wamegeuka tishio kwa watu.

Jeshi la Polisi Wilaya ya Busega lilifika katika tukio hilo na kushughulikia taratibu mbalimbali kisha mwili wa marehemu kukakabidhiwa kwa familia kwa ajili mazishi.

Source: Mwananchi
 
Hivi yuko wapi yule Mbunge wa CCM Kishapu aliyekutwa na Bunduki za kuwindia 20 na nyama ya pori tani kumi?

Sasa hawa Fisi wale nini kama hadi vitoewo vyao na tozo zetu na kodi zetu hazipati Amani?
 
Lakini pia hawa wasukuma waache kufuga fisi! Fisi ni nyara za serikali na pia sio mfugo!
Ileje fisi hao hawafugwi. Infact hii imani na kusema kuna fisi wanafugwa ndiyo imefanya watu waendelee kuamini imani potofu na hatua hazichukuliwi. Hivi FFU na wanajeshi tulionao wanafanya nini? Wanasubiri vita au kupiga watu tu? Serikali inashindwaje kuchukuwa patuni kadhaa ziende kupiga kambi hayo maeneo ili kuua fisi wote?
 
Moyo wangu huwa wahuzunika sana nikisikia au kusoma visa vinavyohusiana na vifo vya watoto wadogo kama hao...

Huwa najaribu kupata picha jinsi walivyokuwa wanapigania maisha yao, Mungu awatie nguvu wazazi wao katika wakati huu mgumu...
 
Suluhisho, wazazi wawasindikize watoto shule sisi tunanunua magoli kwanza.
Wapumzike kwa aman marehemu wote! Ila hii post yako ni ya kijinga na imejaa chuki tu! Kwa hyo ulitaka rais afanyeje kuhusu hao fisi? Mafisi mnafuga wenyewe wasukuma halaf yakidhuru watu lawama kwa samia! Upumbavu tu! Mbona hizi lawama hamkupost wakati magu na kina sabaya wanaua ben, mawazo na azory na kuwaumiza kina lisu na kabendera?
 
So sad kwa kweli...
Je, n8 matokeo ya watu kusogelea maeneo ya Wanyama au wanyama kuvamia makaazi ya watu?
 
Wapumzike kwa aman marehemu wote! Ila hii post yako ni ya kijinga na imejaa chuki tu! Kwa hyo ulitaka rais afanyeje kuhusu hao fisi? Mafisi mnafuga wenyewe wasukuma halaf yakidhuru watu lawama kwa samia! Upumbavu tu! Mbona hizi lawama hamkupost wakati magu na kina sabaya wanaua ben, mawazo na azory na kuwaumiza kina lisu na kabendera?
Ongezea na Chacha Wangwe
 
Back
Top Bottom