Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,115
Watoto wawili ambao wanafahamika kwa majina Evance Kapinga (3) na Tabia Ngombele (17) wamefariki dunia baada ya kuacha jiko la mkaa likiwa linawaka ndani wakiwa wamelala nyakati za usiku.
Mwenyekiti wa mtaa wa Frelimo Bw. Jalala Mwinyimbegu amerhibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema watoto hao waliachwa peke yao na mzazi waliyekuwa wanaishi naye ambaye alikuwa safarini na aliporejea usiku na kugonga hodi bila mafanikio akawaita majirani waliovunja mlango na kukuta watoto tayari wamefariki.
EATV imezungumza na jirani wa familia hiyo Ibrahim Kitang’ala, ambaye anaiashi katika nyumba waliyokuwa wakiishi watoto hao na mzazi wao na amesema baada ya kuvunja mlango walikuta watoto hao wamefariki huku mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina Moline Mligo (7) akiwa amenusurika.
“Tulipovunja mlango tulimkuta mama mdogo wa watoto hao akiwa jirani na mlango kwahiyo tunadhani wakati anasonga ugali alipoona hali inakuwa mbaya alitaka kufungua mlango na yeye akaishiwa nguvu” amesema Ibrahim Kitang’ala, jirani.