Maggid ana nini na CDM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maggid ana nini na CDM?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by issenye, Feb 10, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Wana JF naomba tumjadili majid Mjengwa kutokana na hizi makala zake dhidi ya CDM. Alianza na maandamano ya Arusha sasa amekuja na hili la wabunge kutoka nje kupinga ukandamizaji wa CCM dhidi ya demmokrasia

  Wabunge CHADEMA Kutoka Nje Ya Bunge: Tafsiri Yangu
  Ndugu Zangu,

  SASA ni dhahiri shahiri kuwa CHADEMA inapoteza mwelekeo. Hili si jambo jema kwa demokrasia yetu changa tunayotaka kuijenga.

  Nimesoma kwa makini magazetini habari kuhusu sakata la wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge jana jioni. Hakika sikuona mantiki wa walichokifanya mbali ya CHADEMA kuanza kutengeneza ombwe la upinzani wenye maana uliotarajiwa na Watanzania wengi.

  Miezi mitano imepita tangu tumalize uchaguzi, CHADEMA bado hawaonekani kufunga ukurasa wa siasa za wakati wa kampeni za uchaguzi. CHADEMA wana lazima ya kuingia kwenye maisha magumu na ya kawaida ya kisiasa.

  Maisha ya kisiasa yenye changamoto zake. Migogoro ya ndani ya Chama ikiwamo kutofautiana kimawazo. Uimarishaji wa chama mikoani na wilayani, kwa nchi nzima na mengine mengi. Ni ukweli CHADEMA bado haijaimarika katika ngazi za chini.

  Na changamoto za kisiasa hazikimbiwi, hukabiliwa kwenye majukwaa ya kisiasa. Wabunge wa CHADEMA hawakuwa na sababu za msingi za kutoka nje ya bunge. Badala yake, wangepambana kwa hoja ndani ya Bunge. CHADEMA si wanajua, kuwa hatma ya jambo lile lilikuwa ni kupigiwa kura. Kwamba wangeshindwa. Ni sehemu ya mapambano ya kisiasa.

  Watanzania tuna matatizo haya mawili; Mosi, tu mahodari sana wa kuukana ukweli. Pili, tu mahodari sana wa kuupotosha ukweli. Ukichanganya na kukimbilia kushabikia mambo na kutofikiri kwa kina, basi, tunashindwa kabisa kuambizana ukweli hata kama tunauona. Kwa kitendo cha jana, Wabunge wa CHADEMA hawakuwa sahihi. Kuwaambia vinginevyo si kuwasaidia.

  Wakati mwingine kukimbilia kutoka nje ya Bunge hakupelekei kupata huruma ya kisiasa bali hasira za kisiasa kutoka kwa wapiga kura. Ndio, kuna gharama zake. Mtatotaka nje bungeni mara ngapi? Na CHADEMA kutoka nje bungeni kulikuwa na hasara zaidi kuliko faida. Huku mitaani, kuna watu wanaoanza kuiangalia CHADEMA kwa miwani mingine. Kwa staili hii, itafika mahali Wabunge hao wakaja kuzomewa Kibaigwa, Msamvu na kwengineko.


  Na David yule wa Kafulila kausema ukweli wake; kuwa. "Tunashinda kwa asilimia 20 tunakataa mseto, tukipata asilimia 60 hali itakuwaje, ukipata kidogo uoneshe una busara ya kufanya kazi pamoja, kwa hali hiyo ukipewa kikubwa huwezi kuaminika." Anasema David Kafulila wa NCCR Mageuzi.

  Sikilizeni, enyi ndugu zangu wa CHADEMA, yale tuliokuwa tukiwashutumu CCM, CHADEMA sasa mnayafanya mara mbili yake! Tumeilaumu, na bado tunailaumu sana CCM kuwa chama kisichokubali mabadiliko. Chama ambacho hakitaki kujenga misingi ya kugawana madaraka na wengine.

  Leo CHADEMA hamjaingia madarakani mnaanza mapema kuwachagua wa kukaa meza moja na nyinyi. Mnavikebei vyama vingine ikiwamo CUF. Tuchukue mfano wa CUF, badala ya kuwakebei, busara ingekuwa kuwapa heshima yao stahiki kwa mchango wao wa kuleta mageuzi ya kisiasa hapa nchini.

  Inapofika mahali idadi ya wapiga kura wote wa wabunge wa Zanzibar inapofananishwa na idadi ya wapiga kura wa jimbo la John Mnyika la Ubungo, na kuwa kigezo cha mbunge wa kutoka Zanzibar asiwe Mwenyekiti wa Kamati ya bunge, basi, hapo kuna tatizo maana, tutakuja kuambiwa Rais wa nchi hii hawezi kutoka Zanzibar maana huko watu wake hawazidi milioni moja!

  Hakika, huu ni wakati wa CHADEMA na wabunge wake kutanguliza busara. Huko tunakokwenda tungependa tuwe na serikali za mseto. Na CHADEMA wana nafasi ya kuonyesha mfano wa kunyosha mkono wa ushirikiano na vyama vingine vya upinzani bungeni, hata viwe vidogo kiasi gani. Waonyesha utayari wa kushirikiana na kuvishirikisha vyama vingine vya upinzani badala ya kuvipa mgongo. Inawezekana.

  Maggid
  Iringa,
  Jumatano, Februari 9, 2011
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tulia tunabalance mambo , Asante mkuu Maggid:clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280

  Sawasawa mkuu tumekuelewa, sasa msimlipe Maggid peke yake, hebu niPM na mimi hiyo kazi ya kuwa kinyonga naimudu vilevile, maana watu tumeshapigika vya kutosha, tuwasiliane na mimi nitakuwa naingia humu kwa ID nyingine. nasubili msg mkuu.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,471
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Maggid ni kigeugeu....na yupo humu...kimya baada ya kushindwa hoja juu ya Arusha
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hamumtendei haki Maggid nadhani yeye ni mtu anaeona kwa jicho la tatu kuna vitu vingine haihitaji kufanya ili kuwafurahisha watu fulani, napenda watu wanaochambua mambo na adhari zake za muda mfupi na muda mrefu hizi analysis huwasaidia watu kujua tulipo na tuendako.

  Usife moyo Magid nice article.
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Very Good Shossit
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Mkuu twende taratibu kidogo, kusema kwamba Majjid anaona kwa jicho la tatu ni kututukani sisi kwamba ni mambumbu hatuoni mbali, na unamweka Maggid kwenye hadhi ya umungu kwamba yeye hawezi kukosea, hapana mkuu wote humu tuna akili timamu na hatutompa mtu yeyote au niseme sitompa mtu yeyote nafasi ya kufikiri kwa niaba yangu. Maggid ni binadamu na huwa anakosea na ananunulika vilevile ushahidi upo japo hapa sio mahakamani na kama anabisha ajitoze sasa hivi kwenye hii thread nilimlipuwe sasa hivi
  ONYO: KAMA UNAISHI NYUMBA YA VIOO USIMCHOKOZE KICHAA. TUMO HUMU KWA SURA MBALIMBALI. KARIBU MAGGID.
   
 8. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Maggid Mjengwa is extremely chameleonic. Ni Maggid huyu huyu wakati wa campaign alikua anatumia blog yake kumpigia campaign JK wazi wazi. Na hata yeye mwenyewe alitoa msimamo wake kwamba ni kwa nn atampigia JK kura. Ni huyo huyo baada ya matokeo alianza usifia upinzani kwa kazi nzuri. Ni huyu huyu Maggid baada ya mauaji ya kule kwao Mbarali. Ukimuuliza chanzo cha mauaji hayo na ya Arusha ni nini atakuambia ni AR ni upinzani, mbeya ni CCM na serikali yake. Ukimuuliza ni kwanini unatumia nafasi yako kuwahadaa watu waipigie CCM hakupi jina. Angalia jinsi anavyojadili kuhusiana na maozo ya Richmond, Dowans, etc. The man is a pitiable CCM puppet who's using the pen kudhoofisha upinzani. It's too late. He needs to get back to school and acquaint himself with the international politics to establish the truth behind wabunge kutoka nje. Maggid needs to know that changes are bound to come, come what may.
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,471
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Posee...

  [​IMG]
   
 10. kichomeo

  kichomeo Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bro pamoja na kuoa mzungu bodo hastaarabiki tu,ndo matatizoya wahehe,shule ndogo brain haipo smart thats y,ngoja ntampa taarifa mzungu anyang'anye laptop,lkn sometimes tuvumilie coz hata mke wake kamzidi umri so ni kama anambemenda,mwambi rostamhatampa chochote zaidi ya kumpotezea amani kwenye jamii hii ya wenye hasira
   
 11. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 740
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Hahahahahaaaa..sasa ndiyo nimekuona mbumbumbu kutona na hayo majibu yako.kuona kwa jicho la tatu haimaanishi kama ulivyofahamu wewe hapo.uchuie kuna mtenda,mtendewa na mtu wa tatu ni mtazamaji.sasa kamahao watu wawili yaani mtenda na mtendewa wakigombana muono wao kwenye hiyo issue ni tofauti na muono wa mtazamaji.na uwezekano wa mtazamaji kuwa bias ni mdogo sana kwani tunajaalia ya kuwa hana self interest ya kile wanachokigombania.na hapo ndiyo tunasema mtazamaji ameangalia kwa jicho la tatu.pindipo akitoa mchango wake kuhusu issue ile. shule ni muhimu na siyo jazba.
  PS kama wafuasi wa chichiem ni myopic basi wa cha-dem ni blind.kumbuka wote wana maradhi!!!!
   
 12. s

  shosti JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  sikuwa najua kumbe ukioa au kuolewa na mzungu unastaarabika,tembea uone:coffee:
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  huyu maggid mjengwa alilelewa katika kituo cha kulelea yatima baadae akachukuliwa na kuanza kulelewa na mzungu baadae alivojua goodmorning akamchakachua mzungu,akapelekwa sweeden kusomea uandishi wa habari aliporudi akarubuniwa na CHAMA CHA MAUAJI,ana watoto wa4 wawili mapacha,kwa ufupi anitwa baba gustav,alikua na akili na misimamo baada ya kunyoa rasta ndo akawehuka.....katika gazeti la mme wao RAI ana kona ya maggid...................kwa kifupi anakaa Iringa gangilonga,pambaaaf sake
   
 14. s

  shosti JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  majungu hayo,na yule mdogo wake naye alilelewa na nani:sick:
   
 15. Mwangaza

  Mwangaza Senior Member

  #15
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Majid mwandishi maarufu kama wewe unapokuwa unatoa habari za kuposha unakuwa ni MPUUZI (Na sio mjinga, maana mjinga hutibiwa kwa kuelimishwa, lkn mpuuzi hatibiki) na MROHO (Uroho upo wa iana nyingi, kuna wa madaraka,pesa,kuuza sura nk sijui huu wa kwako ni wa nini sasa). Uroho hupeleka watu kama nyinyi the HEGUES. Naamini hakika unajua kwamba wabunge wa CHADEMA walichangia mada saana mpaka walipoona kuna hujuma flan kulazimisha kubadirishwa kanuni ndipo walitoka nje, kunyesha ukomavu wa kidemokrasia wa kutounga mkono uhuni huu.Na sikwamba hawakuchangia mada. Majid hata ITV na TBC walionyesha haya kwenye taarifa ya habari wewe ulikuwa unakunywa ulanzi??

  CHADEMA kama alivyosema Mh.Mbowe ni kwamba sio kwamba hawataki ushirikiano na vyama vingine .ila pawepo na makubaliano madhubuti na mazungumzo ya mda mrefu pamoja na kuwashirikisha wanchama wao.

  Majjid usiwe kama mtoto, elewa kuunganisha CHADEMA na CUF sio kazi ya viongoz tu! kuna mamilion ya wanachama wanahusika hapo. CUF ikiwa ni CCM-B, kuiunganisha na CHADEMA ni sawa na kuinganisha CHADEMA na CCM..na hapo upinzani umekufa TZ.Tutakuwa hatuja watendea haki waTz wanodai mabadiriko, Tutakuwa hatuja zitendea haki roho za watu waliokufa wakidai mabadiriko.

  Majjid, Sio kwamba waTZ ni wakolofi na tunapenda kupingana pingana,kugoma na kuandaman..la hasha! Tunatamani sana migongano hii, wote tufaidi rasilimali za nchi yetu kwa usawa na tufanye maendeleao. Lkn huwez kuungana hivi hivi bila kumaliza madai ya msingi ya wananchi, hapo ndipo unapoona nguvu ya UMMA inafanya kazi. Lazima NGUVU ya UMMA ifanye kazi sana tufika tunapotaka kufika. Angalia kenya nguvu ya UMMA ilifanya kazi sana mpaka serikali ya umoja ikapatina na sasa wote wanafaidi rasilimali za Taifa lao kiusawa. ZNZ pia NGUVU ya UMMA ilifanya kazi sana ndio huo muafaka ulipatikana huko ZNZ huku kwetu bara bado sana...watu wachache ndio wameiweka nchi mifukoni. CHADEMA hatutorudi nyuma ktk hili na tutazid kutumia NGUVU ya UMMA mpaka kieleweke.


  Majjid, ilitakiwa ujiulize kabla huaandika huu upuuzi, kwanini CCM wanalazimisha CHADEMA waungane na vyama vingine(hasa hasa CUF maana vingne vimeunganishwa kwa mkumbo tu)?? Kwa nini CCM wasiache vyama vya upinzani viamue vyenyewe?? ulishaona wapi duniani chama tawala kikalazimisha vyama vya upinzani viongane??...hapo lazima ujua kuna kitu! Jiulize vizuri sio unakurupuka kurupuka tu.

  USHAURI WA BURE KWA MAJJID,

  Jitahid uwe na ushirikia mzuri na milango yako ya fahamu ikiwemo akili kabla hujaandika vitu vinavyogusa jamii. ukiendelea kuandika kwa kushirikisha vidole vyako tu...itakuja kukughalimu sana.
   
 16. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Aisee ni sura ngapi hizo ulizonazo, mimi nimependa beat lako tu!
   
 17. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #17
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  jamani hebu tupeni habari kamili kwani huyu mjengwa haswa ni nani? na anamaslahi gani na ccm lazima kuna kitu hapo yawezekana anaogopa mke wake asijerudishwa kwao kama yeye atakuwa kinyume na matakwa ya ccm

  msema ukwelii hapendwiiiii daimaaaa:A S thumbs_down:
   
 18. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Punguza jazba mikatafeki isije kuwa na post yako feki. Kifupi post sijaipenda mimi nimeiona kupitia http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/wabunge-chadema-kutoka-nje-ya. Nilisoma nikaona kidogo kama yupo biased na alichokuwa anakiongea lakini nikaona ni mtazamo wake.
   
 19. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mwambieni huku siyo sehemu ya mahubiri...akafungue kanisa.
  Mgomo ni moja ya suluhu ya matatizo.
   
 20. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyo kaolewa na mzungu hajaoa mzungu ndio mana anakosa misimamo kashazoea kuhongwa hongwa......
   
Loading...