Maggid amchana Lau Masha live..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maggid amchana Lau Masha live.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Leornado, Dec 28, 2010.

 1. L

  Leornado JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Na Maggid Mjengwa,
  UKITAKA kumjua Mwafrika, basi, mwangalie siku anapohama. Ndivyo tulivyo. Hata kwenye uongozi, ni hivyo hivyo. Mwangalie kiongozi wa Afrika anapoingia
  na anapotoka kwenye madaraka.

  Ndio, hana tofauti sana na Mswahili anayehama kutoka Mwananyamala kwenda Magomeni. Mswahili wa
  Mwananyamala, hata kama atahakikishiswa, kuwa anakohamia Magomeni vyumba
  vyote vina taa za balbu na pazia za madirishani na milangoni, bado,
  Mswahili huyu atahakikisha, kabla ya kuhama, anangÂ’oa balbu na pazia
  zote kutoka nyumba anayohama. Mpangaji mpya atakayekuja atajua mwenyewe!
  Huyo ndio Mwafrika, ingawa si wote, hata ukimchanja kwenye damu yake,
  utakuta chembe chembe za ushamba uliochanganyika na hila.

  Hakika, hizo ni hulka za Mwafrika, hata azaliwe na kukulia Ulaya au Marekani.
  Si tumesikia majuzi, Waziri aliyepoteza ubunge alihakikisha anahamisha
  mpaka pazia kutoka kwenye ofisi ya mbunge jimboni kwake. Naambiwa, kuwa
  Waziri huyo kakulia Marekani. Kumbe, kukulia Marekani hakumwondolei
  Mwafrika hulka zake! Na hilo Ni Neno La Leo.

   
 2. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  lau balaa
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ushamba mpaka kwenye chembechembe za damu hahaha!Kweli lakini kuna watu wengine hata wasome vipi..wasafiri na kuishi majuu bado ushamba hauwaishi!
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  ''Miafrika ndivyo ilivyo'' by Nyani Ngabu
   
 5. L

  Leornado JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Labda yalikuwa masharti ya mganga kubeba kila kitu... Lau umeliaibisha taifa. Still kwenye profile yake face book anajiita waziri wa mambo ya ndani, kivipi?
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Kweli Lau pale alipotoka kidogo alikuwa na hasira ushamba.....uliopitiliza...aibu fulani hivi...hadi mapazia...vitasa aahh
   
 7. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Heee kweli inachekesha. Huo ni umaskini wa roho.
   
 8. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Si ushamba kamwe bali ni choyo na tamaa iliyopita kiasi!! enzi za kuwa kongozi wa maisha zimepita!!
  Me nilipenda alivyojionyesha ni mtu wa namna gani, then utarajie mtu wa sampuli hii alete maendeleo? labda kama kalogwa.
   
 9. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  alinunua na pesa zake au?
   
 10. c

  carefree JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tatizo ni utaratibu mbovu unaotumiwa wa kuwapa wabunge fedha hizo kama sehemu ya mishahara hivyo hakuna marejesho zimetumikaje?
   
 11. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hiyo ndiyo athari ya kutojiandaa kushindwa. Kwa namna moja au nyingine Masha hakutegemea kama hali ingekuwa vile lakini hakustahili kufanya vile kwani ni vingapi yeye kama yeye amepata tena vya kifisadi hadi afikie kuja kung'oa vitasa na mapazia. Kifupi amejivunjia sana.
   
 12. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Baadhi ya viongozi wa nchi hii wana fikira mgando ambazo hazisaidii bali zinabomoa. Nani kasema utaendelea kuwa kiongozi daima milele? Ifikie mahali tukubali (Viongozi waroho wa madaraka) kushindwa. Tabia hii ndio inayotufanya tuzidi kuwa na maendeleo duni pamoja na kwamba tuna rasilimali za kutosha.
   
 13. m

  maarufu Member

  #13
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo inaonyesha kuwa hata uwaziri hakupaswa kupewa na labda tumuuliza s v nahodha kuwa masha hajaenda kuchukua kompyuta yake pale wizarani? maana tabia ni kama mimba huwezi kuficha
   
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Waingereza wana msemo kuwa " YOU CAN TAKE THE AFRICAN OUT OF THE BUSH BUT NOT THE BUSH OUT OF THE AFRICAN". Sasa hayo ndio mambo ya hao waheshimiwa ingawa wamekulia majuu lakini bado wana asili yao ya kung'oa pazia na vitasa wanapohama!!
   
 15. L

  Leornado JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kuna wengine huwa wanakunya ndani ii mpangaji mpya apate kazi ya kudeki uharo...
   
 16. N

  Nimrod Member

  #16
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio tunayo hiyo hulka, lakini mwenzetu na hasira ya kushindwa!! haaa haaa
   
 17. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Tulisha laaniwa
   
 18. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,838
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  hahahahahahah hili kweli ni neno la leo Mkulu,,,huko kulikuwa kuweweseka kwa kutokuamini matokeo papaaa
   
 19. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  The Birds of the same feather.........
  Character of Masha reflects the Character of His then Boss........
   
 20. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Nadhani kaoneysha uzungu halisi, wazungu wanathamini kitu chohcote walicho nunua na wanapo hama hutoa vitu vyao na kufanya yard sale , nadhani kukulia USA ndiokumemfanya afanye hivyo maana ana jua matumizi halisi ya pesa.

  Tuliishi na jirani na Mzungu Obay , yeye alipo ondoka alitoa hadi fence aliye weka yeye mwenyewe, huo ni uzungu jamani.
   
Loading...