Neno Fupi La Usiku Huu: Utamjua Mwafrika Anapohama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno Fupi La Usiku Huu: Utamjua Mwafrika Anapohama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, May 6, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,
  Ukitaka kumjua Mwafrika, basi, mwangalie siku anapohama. Ndivyo tulivyo. Hata kwenye uongozi, ni hivyo hivyo. Mwangalie kiongozi wa Afrika anapoingia
  na anapotoka kwenye madaraka.

  Ndio, hana tofauti sana na Mswahili anayehama kutoka Mwananyamala kwenda Magomeni. Mswahili wa
  Mwananyamala, hata kama atahakikishiswa, kuwa anakohamia Magomeni vyumba
  vyote vina taa za balbu na pazia za madirishani na milangoni, bado,
  Mswahili huyu atahakikisha, kabla ya kuhama, anang’oa balbu na pazia
  zote kutoka nyumba anayohama. Mpangaji mpya atakayekuja atajua mwenyewe!
  Huyo ndio Mwafrika, ingawa si wote, hata ukimchanja kwenye damu yake,
  utakuta chembe chembe za ushamba uliochanganyika na hila.

  Hakika, hizo ni hulka za Mwafrika, hata azaliwe na kukulia Ulaya au Marekani.

  Na hilo ni Neno Fupi la Usiku Huu.
  Maggid Mjengwa,
  Iringa
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Kaka mjengwa,
  Mie nataka tu nione wakati Chami anahama ,je atamuachia madudu Kigoda au ataondoka nayo? najua Ekelege atamuazima chami ile pickup yake kusomba madudu yake ya TBS
   
 3. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweli mwel...halafu leo nimehama...yani kama ulivyosema....kila kitu kidogo ning'oe na komeo la mlango kama si mwenye nyumba kukoroma....
   
 4. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  ila mbona wanapohama wanawaachia wengine madudu waliyofanya?
   
 5. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  ni kweli kabisaa. halafu umesahau kuwa harufu ya choo hufanana kwa kunuka!
   
 6. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Maggid mbona hata White House kila akiingia Rais mpya anafanya mabadiliko ya samani na vitu vingine?
   
 7. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Maggid,Nilkuandikia SMS lakini sasa nimepata mtandao wa uhakika.
  Umeandika kweli kabisa na karibuni kuna Mganga Mkuu wa Mkoa ambaye aling'oa mpaka komeo za milango.Mtu huyu ana uhakika wa kukuta nyumba ya serikali aendapo na pia atapata fungu la ukarabati lakini tamaa imekuwa kubwa mno na ubinafsi unatutafuna mno.
  Ulipotaja ya kuwa waafrika ndivyo tulivyo nilkuwa na wasiwasi mkubwa kwa kuwa mwenza si mwafrika inawezekana ukashukiwa na kila aina ya maneno ya ovyo lakini naona mpaka sasa kumetulia.Na iendelee hivyo.
   
 8. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kwa mswahili ni vigumu kuacha mbachao..............
   
 9. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tatizo wamiliki wa nyumba wengi wao hukwepa majukumu. Nyumba inahitaji walau kwa kila baada ya miaka miwili ifanyiwe matengenezo madogo madogo lakini likija suala hilo huwa wabishi na kuwaambia wapangaji kuwa nyumba walikuta ikiwa safi, hapo unategemea nini? Kumbuka leo hii kuna vitasa vinauzwa hadi elfu hamsini kwa kimoja na unasema nikiache! Thubutu!
   
 10. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unamsema Masha aliyeng'oa vitasa vya office,ili Wenje akija ajijue mwenyewe?
   
 11. I

  Iramba Junior Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu! The same thing also happned when Marsha alipokuwa anachukua vitu vyake na kumpisha Wenje! Aling'oa vitasa,n.k.
   
 12. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  hii generalisation za waafrika sizikubali. Kwani majid yeye kafanya research kwenye nchi ngapi za kiafrika mpaka afikie conclusion hii? Hivi tukienda botswana, Moroco, Shelisheli, misri kote tutakuta uhamaji wa namna hii??? Hizi ni kasumba alizoaminishwa na mkewe mzungu. Waafrika tuachane na mitazamo hasi ya uafrika wetu. Kwanini usitoe mfano mzuri ukasema huu ndiyo Uafrika? Mambo mabaya uafrika, mazuri uzungu. Elimu haitusaidii tuabadilike.
   
 13. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mkuu si wa AFRICA tu,niliwahi kukaa na mmarekani mwenye mchanganyiko wa puerto rico (black) na latino siku anaondoka alikomba malapa ya kuoga ,sikuamini alipoyapakia kwenye ndege kuelekea zake dubai!
   
Loading...