Mageuzi yanaanzia juu. Je, Waziri wa Mambo ya Ndani yupo tayari kwa mageuzi?

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
3,718
11,708
Kama kuna ajenda ambyo Mheshimiwa Rais wetu ameivalia njuga basi ni mageuzi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama pamoja ni mifumo ya utoaji haki!

Katika hilo wanao nyooshewa sana kidole hadharani ni Jeshi la polisi, magereza pamoja na kidogo mahakama. Na huko sirini inawezekana kuna wengine.

Vyombo hivi vina mapungufu makubwa ambayo yako ndani sana ya tamaduni zake kiasi kwamba ni vigumu kuamini kama kazi hiyo inawezekana bila ya kuvivunja kabisa baadhi ya vyombo hivyo na kuviunda upya kwa sheria mpya na ajira mpya.

Hapa majuzi tu katika ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa wa juu wa jeshi la polisi tumepata 'reminder' ya kazi ngumu iliyo mbele ya Rais, waziri wake wa mambo ya ndani amesimama na kuongea vitisho kwa umma na mambo mengine ya ajabu ajabu, kwenye kikao ambacho 'main theme' ni maboresho ya jeshi katika kutenda haki 🤣!

Sasa huyu bwana alikuwepo wakati wa awamu ile inayotuhumuwa kwa ukatili wa kutisha tangia nchi hii ipate uhuru, alikuwa naibu waziri, kwa lugha nyingine ni mtu wa falsafa kama za awamu ile, vitisho, ubabe na ukatili.

Kama mama anataka kurahisisha kazi ya kufanya mageuzi hayo, basi aanze juu kabisa, kwa waziri wa mambo ya ndani! Nafasi ile inapaswa kukaliwa na mtu ambaye ni muumini wa kweli wa haki na mageuzi. Kinyume na hapo atalalamika sana na hakuna cha maana kitakachobadilika
 
Back
Top Bottom