Maharagande: Tunataka Ratiba ya Utekelezaji wa Mageuzi ya Kisiasa Nchini

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Utangulizi.
Chama cha ACT Wazalendo kupitia Kamati ya Kuisimamia Serikali ya Wasemaji wa Kisekta (Baraza Kivuli la Mawaziri) imekuwa ikifuatilia kwa karibu maoni na majadiliano juu ya madai ya wadau mbalimbali kuhusu mageuzi ya kidemokrasia nchini. Mnamo tarehe 22 na 23 Agosti 2023, wadau wa siasa kupitia jukwaa la Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) walikuwa na majadaliano yaliyowezesha kupata mwafaka kwenye masuala kadhaa kuhusu mageuzi yanayopaswa kufanyika katika uendeshaji wa siasa zetu nchini.

Kufuatiwa na mjadala huo, tumeona kwa sasa upo mwafaka kwa wadau wote juu ya madai ya kuwa na Tume huru ya uchaguzi, kuanza kwa mchakato wa katiba mpya, mabadiliko ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa; Na mabadiliko ya vyombo vinavyohusika na usimamizi wa siasa (Sheria ya Jeshi la Polisi).

Sisi, ACT Wazalendo tunapata wasiwasi kwenye utaratibu wa utekelezaji wa maoni na maeneo yaliyofikiwa mwafaka na wadau tangu mijadala hii ianze. Tunaona mijadala inachukua muda mrefu bila ya kuwa na kalenda ya utekelezaji katika kukamilisha madai na malengo ya mageuzi ya siasa zetu. Tangu mwaka jana, tumekuwa tukitoa wito kwa Serikali kuweka ratiba ya kila jambo na namna utekelezaji wake.

Hivyo basi, tunarudia tena wito wetu kuwa tunaitaka Serikali iweke wazi ratiba ya utekelezaji wa maazimio ya wadau kutoka majukwaa mbalimbali ili kuwa na Sheria Mpya ya vyama vya siasa Sheria mpya ya uchaguzi na marekebisho ya Sheria ya mchakato wa Katiba mpya.

Aidha, tunaitaka Serikali katika vikao vijavyo vyote vya wadau iletwe kalenda ya utekelezaji badala ya kufanya kama majukwaa ya kuendelea kutoa maoni pekee.

Mwisho, tunatoa wito kwa wadau wengine ni wakati wa kushirikiana na kushikamana kuitaka Serikali kuanza kutekeleza maazimio yatakayoleta mageuzi ya uendeshaji wa siasa zetu nchini kwa kuweka ratiba ya utekelezaji wake sasa.

Hitimisho
Ni matumaini yetu kuwa dhamira, nia na utayari wa kisiasa wa viongozi wa Serikali unapaswa kutafsiriwa kwa vitendo. Hivyo basi ni wakati sasa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Nchi kama Mkuu wa Shughuli za kiserikali Bungeni, Mkuu wa kisera na Mkuu wa shughuli za kisiasa kwa kuwa Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa ilichukue jambo hili kwa uzito ili lianze kutekelezwa.

Imetolewa na;
Ndg. Mbarala Abdallah Maharagande,
Twitter: @Mbaralagande
Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria
ACT Wazalendo.
28 Agosti, 2023.
 
Tatizo la wanasiasa wa bongo mna njaa sana! Halafu ni wanafiki. Na hapa ndipo ccm inapowakamata kwa urahisi. Mkizidiwa tu kidogo na njaa, mnalambishwa asali.

Ona Kiongozi wenu mkuu Zitto! Baada ya kulambishwa asali, hata hajulikani alipo! Na ikitokea amejitokeza kutoka huko mafichoni alipo, basi utamsikia tu anasifia kila kilichopo mbele yake! Kwa namna hii ccm itakuja itoke kweli madarakani!! Kuweni na msimamo bahana!
 
Tatizo la wanasiasa wa bongo mna njaa sana! Halafu ni wanafiki. Na hapa ndipo ccm inapowakamata kwa urahisi. Mkizidiwa tu kidogo na njaa, mnalambishwa asali.

Ona Kiongozi wenu mkuu Zitto! Baada ya kulambishwa asali, hata hajulikani alipo! Na ikitokea amejitokeza kutoka huko mafichoni alipo, basi utamsikia tu anasifia kila kilichopo mbele yake! Kwa namna hii ccm itakuja itoke kweli madarakani!! Kuweni na msimamo bahana!
Wanasiasa bongo wanafki sana

Ova
 
Back
Top Bottom