Magazeti yanayomsafisha Lowassa haya hapa!

Magazeti yanayomsafisha Lowassa haya hapa!

Kila nikitizama uozo wa kwenye halmashauri zetu namkumbuka el

Uozo huu ambao sasa una nafuu ulikuwa umeshamiri sana enzi za Lowassa. Mtu huwezi kuishi kwa kutegemea sifa za kuunga unga wakati tunajua kwamba sifa hizo zinamezwa na sifa mbaya ya kukosa uadilifu na kuendesha hujuma na uasi.
 
Mkuu nakumbuka wakati ule alizuia viwanja vya Mnazi Mmoja visiporwe.

Ni baada ya kukataliwa kupewa kitu kidogo na Baghdad mpaka akamzulia kesi iliyomfunga jela. Wakati anazuia Mnazi mmoja, kule maskai alikuwa akigawa open space kama njugu! Mnafiki mkubwa huyu!
 
........ndugu! kama umetumwa ishia huko huko, RAIA MWEMA na DIRA na MEMBE wenu, hamuwezi tena kutuaminisha ujinga mnaoamini, unataka tutumie lugha ngumu afu useme hekima zimeturuka? mpuuzi kweli wewe, sisi sio wajinga tena kama unavyofikiri, upuuzi wako ufanyie huko huko! ....ck u! upuuzi hauhalalishwi kwa upuuzi, lakininkwa hili la kwako, hamna mwenye akili timamu wa kukuvumilia, kwa sababu utakuwa umetufanya wote wajinga kama wewe!!!!

Tulichoshuhudia kwenye post yako hii ni ukweli wa kwamba wewe ni mtoto uliyekulia katika mazingira magumu ambaye kwake yeye ustaarabu ni idadi ya matusi anayoyajua. Halafu unajiuliza kama kweli Lowassa anastahili kuwa rais kama company yake ni ni midomo ya vyoo vya uswahilini kama wewe! Lowassa alishaandika political orbituary yake yeye mwenyewe na sas tunasubiri tu memorial service. Zuma mnayejifananisha naye alikuwa kipenzi cha watu, walalahoi. Huyu bwana hawezi hata kufanya mkutano manzese Bakhresa au Karume Mchikichini.

Nyerere alipomnadi Mkapa hakukuwa na rekodi yoyote mbaya kuhusu Mkapa na kwa hilo mwalimu alikuwa sahihi. Huyu jamaa alishahukumiwa na attempts zozote sasa haziwezi kufua dafu maana mahakamani (Court of Public opinion) hakuna reverse gear.

Kama mnafanya postmortem mlitakiwa kujiuliza kwamba kwa miaka yote ya kununua kila chombo cha habari, kwa nini hakujawa na improvement katika approval ratings zake? Go back to the drawing board men!
 
Swali la msingi ni kuwa na huyu mleta mada na ANATUMIWA na nani?

Imefikiwa wakati tumeacha kufikiri kwa vichwa na kuendekeza matumbo yetu. Kama humpendi au hutaki EL awe rais basi ujue kuna unayempenda.

Kwa wakristo Yesu aliwahi kusema ASIYE NA DHAMBI AANZE KUMRUSHIA JIWE YULE MAMA ALIYEKAMATWA AKIZINI, Nini matokeo? wote wakaanza kuondoka mmoja mmoja.

Hilo ndo lilopo. Mwisho wa siku kila mtu ana mapungufu yake, tunachojali ni UCHAPA KAZI. EL ni bora kwa uchapa kazi.
 
Tulichoshuhudia kwenye post yako hii ni ukweli wa kwamba wewe ni mtoto uliyekulia katika mazingira magumu ambaye kwake yeye ustaarabu ni idadi ya matusi anayoyajua. Halafu unajiuliza kama kweli Lowassa anastahili kuwa rais kama company yake ni ni midomo ya vyoo vya uswahilini kama wewe! Lowassa alishaandika political orbituary yake yeye mwenyewe na sas tunasubiri tu memorial service. Zuma mnayejifananisha naye alikuwa kipenzi cha watu, walalahoi. Huyu bwana hawezi hata kufanya mkutano manzese Bakhresa au Karume Mchikichini.

Nyerere alipomnadi Mkapa hakukuwa na rekodi yoyote mbaya kuhusu Mkapa na kwa hilo mwalimu alikuwa sahihi. Huyu jamaa alishahukumiwa na attempts zozote sasa haziwezi kufua dafu maana mahakamani (Court of Public opinion) hakuna reverse gear.

Kama mnafanya postmortem mlitakiwa kujiuliza kwamba kwa miaka yote ya kununua kila chombo cha habari, kwa nini hakujawa na improvement katika approval ratings zake? Go back to the drawing board men!

Una evidence au magazeti yanafikiria kwa niaba yako? Maana kuna watu siku hizi magazeti yanafikiria kwa niaba yao.
Mkapa aliwahi kusema wa Tanzania tu mbilikimo wa mawazo na wavivu wa kufikiri.

Sisi tutaendelea kufikiri kwa AKILI zetu, nyie ONGEZENI idadi ya MAGAZETI yawasaidie kufikiri.
 
TBC nayo imehongwa, juzi wametoa issue ya Lowasa mpaka nikashangaa amefanya issue gani, eti anaelezea maonesho ya miaka 50 ya uhuru, sijui kama nanai wakati ni fisadi aliye fukuzwa kazi ya uwazi mkuu, lakini waandishi walio nununliwa wakitaja kuwa ni msaafu!!! shame of you TBC. Mi ntaingia msituni lowasa akiwa rais
 
Sasa kama anasafishwa na wewe hutaki asafishwe si mchafue. Sasa unataka nani amchafue.

Kama ccm wameshindwa kumvua Gamba basi mtu huyo ni safi acheni BLA-BLA za magamba za kufatilia watu kwa manufaa yao
 
wenzenu wanoteshwa vikombe watibu raia... we umeoteshwa huu upururu uwadanganye raia wema
 
Ufisadi wa Lowassa huu hapa:

1. Kununua jumba la kifahari London, Uingereza, lenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 1 za Tanzania

Metropolitan police wa Uingereza wanachunguza suala hili. Wamewasiliana na anti-money laundering unit ya Tanzania kuchunguza suala hili.

2. Ufisadi wa Nyumba ya Sanaa

Lowassa ni mhusika mkuu wa kufanya uporaji wa ardhi ya Nyumba ya Sanaa iliyopo karibu na Serena Hotel (zamani Movenpik Hotel). Nyaraka zinaonesha yeye ni mmiliki wa kampuni inayojenga gorofa kubwa kwenye eneo hilo la Nyumba ya Sanaa.

3. Utajiri usioelezeka (unexplained wealth)

Akiwa kama kiongozi wa umma, Lowassa amejilimbikizia mali nyingi sana za thamani ya mabilioni ya shilingi. Mali alizo nazo haziendani na kipato chake kama kiongozi wa umma. Sheria ya kupambana na rushwa Tanzania iko wazi kuwa kiongozi wowote wa umma mwenye utajiri usioendana na mapato yake halali anastahili kufikishwa mahakamani. Kutokana na sera za kulindana na kuogopana, Lowassa, Andrew Chenge, na viongozi wengine wa umma hawajafikishwa mahakamani kwa kosa hili na PCCB. Pia kwenye fomu za kila mwaka za kutaja mali, Lowassa haja declare assets zake zote. Ana miliki Alphatel, Alpha Schools, Alpha House, apartment blocks Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi.

4. Land grabbing

Alipokuwa Waziri wa Ardhi enzi za utawala wa Mwinyi alihusika na uporaji mkubwa wa ardhi sehemu mbali mbali nchini.

5. Richmond

Lowassa ndiye aliyeagiza TANESCO waporwe madaraka ya kusimamia tenda ya umeme kinyume na sheria ya manunuzi, PPRA. Aliunda kamati ya makatibu wakuu na kusimamia kwa karibu majadiliano ya kamati hii na nRichmond na kuagiza wapewe tenda wakati Tanesco waliikataa Richmond kuwa haifai. Lowassa ndiye mhusika mkuu wa kashfa ya ufisadi ya Richmond ndio maana alilazimika kujiuzulu.


6. Need I say more?

Lowassa ni mchafu wa maadili. Anapenda sana mali, amejilimbikizia utajiri kuliko kipato chake halisi. Wafuasi wake wanamfanananisha na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Tofauti ya Zuma na Lowassa ni kuwa Zuma alifikishwa mahakamani na kusafishwa na mahakama. Lowassa apelekwe kortini kujibu shutuma za ufisadi, akishinda kesi ndio atakuwa amesafishwa kweli. Si kwa kutumia vyombo vya habari na waandishi wa habari wenye njaa.

Asante kwa kuweka mambo wazi, watetezi wa fisadi Lowassa wote wamefyata sasa. Huyu mpenda mali za wizi ni lazima afikishwe mahakamani haraka aache kuivuruga hii nchi yetu ya amani na utulivu.
 
TBC nayo imehongwa, juzi wametoa issue ya Lowasa mpaka nikashangaa amefanya issue gani, eti anaelezea maonesho ya miaka 50 ya uhuru, sijui kama nanai wakati ni fisadi aliye fukuzwa kazi ya uwazi mkuu, lakini waandishi walio nununliwa wakitaja kuwa ni msaafu!!! shame of you TBC. Mi ntaingia msituni lowasa akiwa rais

Tutakufata huko misituni tuikomboe nchi yetu, haiwezekani tukatawaliwa na fisadi mkubwa kama yeye ambaye dunia nzima inamjua kwa uhalifu wake. TBC kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakitumika kumpa Lowassa airtime kubwa sana kwenye TV hii inayoendeshwa na pesa za walipa kodi kwa lengo la kumsafisha na kumjenga.
 
propaganda za Lowassa anazowapa vibaraka wake;
1. wote wachafu ndani ya CCM (je kama wote ni wachafu hakuna wachafu zaidi?)
2. mchapa kazi (kazi ipi/zipi ambazo zilikua ni vision yake binafsi na akazifanikisha mwenyewe? na je hakuna watu wengine wanaotekeleza majukumu yao kwa ufanisi bila ya siasa wala kujinufaisha binafsi?)
3. wapinzani wake ni wanafiki mfano Sitta anayeshambuliwa na akina kubenea na kibanda (je si Lowassa alimuweka kikwete akijua kua rafiki yake hana uwezo wa kazi huku akampangia baraza la mawaziri la wasiokua na uwezo na vibaraka wake akijua yeye lowassa ndiyo atakua rais ajaye bila kujali ufanisi wa serikali hii sasa yuko nje anajidai ana huruma na wafanyakazi na vijana eti ni bomu la kitaifa,, huu ndiyo UNAFIKI)
4.maamuzi magumu (maamuzi magumu kujiuzulu ili kujiokoa na aibu zaidi kama uchunguzi ungeendelea na kununua pumzi zaidi ya kisiasa, kuvunja city water mkataba ambao ulikua mbovu ungevunjwa na yeyote yule mwenye mamlaka yake hususani katika huduma muhimu kama ya maji)
5.kuonewa kisiasa (wengi wengine wana haki ya kulalamika kuwa wameonewa kisiasa na haina umuhimu wowote kwetu sisi wananchi kwani siasa ni kukosa na kupata sasa kuendelea kulalamika ni kelele -Salim, Sitta, Malecela,Nape, Makamba, Rostam wote wangeendelea kutupigia kelele za kuonewa )
 
Kama ameweza kuwanunua wote hao basi hakuna jinsi lazima eelekee jumba jeupe!! Ina maana wahariri wote hao wamenunuliwa hakuna hata mmoja anayesema ukweli?

Hivi ana tuhuma gani vile? Richmond ilikuwa ajali ya kisiasa tu kama iliyompata Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi wakati ule akiwa waziri wa Mambo ya Ndani!

EL songa hatua kwa hatua


wewe jamaa uwa unanichefua sana na kumkumbatia lowassa ukiwa na avatar ya mpiganaji kama Tom...thats disgrace kama unapenda Africa, umemsoma Tom unajua historia unajua Tz imetoka wapi na inaelekea kwenye neema au shimo gani ikiwa na Rais huyu au yule basi Lowassa ni mtu wa mwisho kabisa kumpigia debe...fikiri otherwise una undugu nae
 
Usafi uanzie moyoni sio nje,hao mafisadi hata wangesafishwa na CNN,ALJAZEERA au hata BBC na magazeti kama Daily mirrow nk kama moyoni hawako safi ni sawa na nguruwe kumuosha na kumpiga mapowder soon atarejea kwenye tope
 
Usafi uanzie moyoni,sio nje na kwenye suti,hata wangesafishwa na BBC.CNN,PRESSTV au hata VOA na magazeti kama daily mirrow nk kama mioyoni ufisadi bado upo ni sawa na nguruwe kumuosha na kumpiga mapowder soon anarudi kwenye matope,wanaowasafisha kwa nje ipo siku uchafu utawarusia wenyewe,chroloquini iliyopakwa asali bado ni chungu tu,ukilamba asali ikiisha unakutana na uchungu halisi
 
Tutakufata huko misituni tuikomboe nchi yetu, haiwezekani tukatawaliwa na fisadi mkubwa kama yeye ambaye dunia nzima inamjua kwa uhalifu wake. TBC kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakitumika kumpa Lowassa airtime kubwa sana kwenye TV hii inayoendeshwa na pesa za walipa kodi kwa lengo la kumsafisha na kumjenga.

Yaani umeamua kuacha kutumia UBONGO wako kufikiri na kutumia magazeti kufikiria?

Duh! haya bana acha magazeti yaendelee kufikiri kwa niaba yako
 
wewe jamaa uwa unanichefua sana na kumkumbatia lowassa ukiwa na avatar ya mpiganaji kama Tom...thats disgrace kama unapenda Africa, umemsoma Tom unajua historia unajua Tz imetoka wapi na inaelekea kwenye neema au shimo gani ikiwa na Rais huyu au yule basi Lowassa ni mtu wa mwisho kabisa kumpigia debe...fikiri otherwise una undugu nae

Mkuu acha kubwabwaja bila EVIDENCE, tuletee evidence la sivyo kaa kimya> Tushachoka na watu ambao magazeti yanafikiri kwa niaba yao.
Amkeni nyie hizi ni kampeni. Think.
 
Wana jf acheni kupotosha umma,kinachoonekana hapa ni kwamba watu wanataka kila siku mwanahalisi liwe na habari ya kuponda lowassa na kumsifia sitta hata kama anafanya madudu.Mi napingana na wote wanaosema mwanahalisi limenunuliwa.Kwangu mimi bado naona ni gazeti lisilofungamana na upande wowote.kama ataharibu sitta watasema ukweli kwani nani asiyejua unafiki wa mzee sitta.Pia binafsi sijaona mwanahalisi likimpamba lowasa na sitegemei wafanye hivo kwa kuwa lowassa habebeki kwa vyovyote vile...kilichotokea kny habari za NEC ni kwamba magazeti yaliandika kile kilichotokea na burning issue muda ule ilikuwa na kujivua gamba...huwezi judge mwanahalis kwa habari moja.
 
Lowassa si anataka awashike masikio chadema kwani hujui hilo kamanda?anajua chadema ndio watakaombeba mpaka ikulu,si unasikia kila akipata nafasi analizungumzia kundi gani zaidi ya vijana???anajua huo ndio mtaji wa chadema hivyo anataka aukope ili akishinda awadanganye chadema na serikali ya mseto wa feki kwa kumtumia zitto!

romantic umejipanga sana unajua hili la Lowassa,CDM na Zitto kua kwenye cabinet ikiwezekana PM..hapa ndiyo unafiki wa CDM unakua nje nje
 
Ufisadi wa Lowassa huu hapa:

1. Kununua jumba la kifahari London, Uingereza, lenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 1 za Tanzania

Metropolitan police wa Uingereza wanachunguza suala hili. Wamewasiliana na anti-money laundering unit ya Tanzania kuchunguza suala hili.

2. Ufisadi wa Nyumba ya Sanaa

Lowassa ni mhusika mkuu wa kufanya uporaji wa ardhi ya Nyumba ya Sanaa iliyopo karibu na Serena Hotel (zamani Movenpik Hotel). Nyaraka zinaonesha yeye ni mmiliki wa kampuni inayojenga gorofa kubwa kwenye eneo hilo la Nyumba ya Sanaa.

3. Utajiri usioelezeka (unexplained wealth)

Akiwa kama kiongozi wa umma, Lowassa amejilimbikizia mali nyingi sana za thamani ya mabilioni ya shilingi. Mali alizo nazo haziendani na kipato chake kama kiongozi wa umma. Sheria ya kupambana na rushwa Tanzania iko wazi kuwa kiongozi wowote wa umma mwenye utajiri usioendana na mapato yake halali anastahili kufikishwa mahakamani. Kutokana na sera za kulindana na kuogopana, Lowassa, Andrew Chenge, na viongozi wengine wa umma hawajafikishwa mahakamani kwa kosa hili na PCCB. Pia kwenye fomu za kila mwaka za kutaja mali, Lowassa haja declare assets zake zote. Ana miliki Alphatel, Alpha Schools, Alpha House, apartment blocks Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi.

4. Land grabbing

Alipokuwa Waziri wa Ardhi enzi za utawala wa Mwinyi alihusika na uporaji mkubwa wa ardhi sehemu mbali mbali nchini.

5. Richmond

Lowassa ndiye aliyeagiza TANESCO waporwe madaraka ya kusimamia tenda ya umeme kinyume na sheria ya manunuzi, PPRA. Aliunda kamati ya makatibu wakuu na kusimamia kwa karibu majadiliano ya kamati hii na nRichmond na kuagiza wapewe tenda wakati Tanesco waliikataa Richmond kuwa haifai. Lowassa ndiye mhusika mkuu wa kashfa ya ufisadi ya Richmond ndio maana alilazimika kujiuzulu.


6. Need I say more?

Lowassa ni mchafu wa maadili. Anapenda sana mali, amejilimbikizia utajiri kuliko kipato chake halisi. Wafuasi wake wanamfanananisha na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Tofauti ya Zuma na Lowassa ni kuwa Zuma alifikishwa mahakamani na kusafishwa na mahakama. Lowassa apelekwe kortini kujibu shutuma za ufisadi, akishinda kesi ndio atakuwa amesafishwa kweli. Si kwa kutumia vyombo vya habari na waandishi wa habari wenye njaa.

kaka umesahau kujimilikisha ranch ya serikali kule Handeni
jengo la umoja wa vijana/UVCCM akiwa mlezi wake
Kuuzwa kwa TRC wakati akimweka mkurugenzi wa PSRC ili fungu lake liwe salama
 
Back
Top Bottom