Magazeti yanayomsafisha Lowassa haya hapa!

Jamhuri halijaanza kutoka unathibitishaje? Kama unahiyo Pay roll ya wanaolipwa na Lowassa scan weka wazi kama huwezi kaa kimya.
 
Akisafishwa utakufa? Unafaidi nini akiwa mchafu?

Mchafu ni mchafu tu na atabaki mchafu. Lowassa ni mchafu wa maadili, hata Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alijua hilo na alituonya tuepukane na huyu mtu. Ni kama nguruwe amezoea kuchea kwenye matope, hata umuogeshe vipi halisi yake ni kuchafuka tu na ataendelea kuwa mchafu tu come what may.
 
Duh, mbona hasira hivyo kaka? Ni dalili ya kupakatwa na mafisadi hayo, sasa ukiona mtu anampiga vita anayekupakata lazima uwe mbogo. Natamani Mwalimu Nyerere angekuwa hai na kuona jinsi mafisadi walivyoshika hatamu.. Tanzania ni nchi yangu, naipenda Tanzania!

nimetukana coz wanaweka thread bila kueleza ufisadi wa mtu,wekeni basi kama upo siyo kubana pua tu,mtu anajiandikia eti mwananchi limenunuliwa,nyie vijana be carefull
 
wanajf mwenye ushaidi kuwa lowasa ni fisadi atujuze,kwani tnaweza hukumiwa bila sababu,tmechoka na tetesi jaman u thinkers,juzi nec ddma kaeleza wazi khsu richmond,ni upi ufisadi wake mwingine????
 
Waulize Barare Limited ni ya nani? Ni ya Lowassa na Regina Mumba Lowassa kama ilivyo ANBEM... More to come

tengeneza thread humu jf na andika kichwa cha habari MBALI NA RICHMOND HUU HAPA UFISADI WA LOWASA,ili umma ujue
 
wanajf mwenye ushaidi kuwa lowasa ni fisadi atujuze,kwani tnaweza hukumiwa bila sababu,tmechoka na tetesi jaman u thinkers,juzi nec ddma kaeleza wazi khsu richmond,ni upi ufisadi wake mwingine????

Muulize kwanza Lowassa kama yupo tayari kwa hili. Tutaanza na file alilomsomea Hayati Mwl. Nyerere, na kuendelea na mengine. Ktk kikao cha NEC alisema kuwa yeye alitaka kuvunja mkataba wa Richmond akamshauri JK akiwa nje ya nchi, JK akamwambia asivunje, hivi huoni hapa kuwa kuna usanii mkubwa sana?
 
Kama ameweza kuwanunua wote hao basi hakuna jinsi lazima eelekee jumba jeupe!! Ina maana wahariri wote hao wamenunuliwa hakuna hata mmoja anayesema ukweli?

Hivi ana tuhuma gani vile? Richmond ilikuwa ajali ya kisiasa tu kama iliyompata Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi wakati ule akiwa waziri wa Mambo ya Ndani!

EL songa hatua kwa hatua
 
wanajf mwenye ushaidi kuwa lowasa ni fisadi atujuze,kwani tnaweza hukumiwa bila sababu,tmechoka na tetesi jaman u thinkers,juzi nec ddma kaeleza wazi khsu richmond,ni upi ufisadi wake mwingine????

Ufisadi wa Lowassa huu hapa:

1. Kununua jumba la kifahari London, Uingereza, lenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 1 za Tanzania

Metropolitan police wa Uingereza wanachunguza suala hili. Wamewasiliana na anti-money laundering unit ya Tanzania kuchunguza suala hili.

2. Ufisadi wa Nyumba ya Sanaa

Lowassa ni mhusika mkuu wa kufanya uporaji wa ardhi ya Nyumba ya Sanaa iliyopo karibu na Serena Hotel (zamani Movenpik Hotel). Nyaraka zinaonesha yeye ni mmiliki wa kampuni inayojenga gorofa kubwa kwenye eneo hilo la Nyumba ya Sanaa.

3. Utajiri usioelezeka (unexplained wealth)

Akiwa kama kiongozi wa umma, Lowassa amejilimbikizia mali nyingi sana za thamani ya mabilioni ya shilingi. Mali alizo nazo haziendani na kipato chake kama kiongozi wa umma. Sheria ya kupambana na rushwa Tanzania iko wazi kuwa kiongozi wowote wa umma mwenye utajiri usioendana na mapato yake halali anastahili kufikishwa mahakamani. Kutokana na sera za kulindana na kuogopana, Lowassa, Andrew Chenge, na viongozi wengine wa umma hawajafikishwa mahakamani kwa kosa hili na PCCB. Pia kwenye fomu za kila mwaka za kutaja mali, Lowassa haja declare assets zake zote. Ana miliki Alphatel, Alpha Schools, Alpha House, apartment blocks Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi.

4. Land grabbing

Alipokuwa Waziri wa Ardhi enzi za utawala wa Mwinyi alihusika na uporaji mkubwa wa ardhi sehemu mbali mbali nchini.

5. Richmond

Lowassa ndiye aliyeagiza TANESCO waporwe madaraka ya kusimamia tenda ya umeme kinyume na sheria ya manunuzi, PPRA. Aliunda kamati ya makatibu wakuu na kusimamia kwa karibu majadiliano ya kamati hii na nRichmond na kuagiza wapewe tenda wakati Tanesco waliikataa Richmond kuwa haifai. Lowassa ndiye mhusika mkuu wa kashfa ya ufisadi ya Richmond ndio maana alilazimika kujiuzulu.

6. Need I say more?

Lowassa ni mchafu wa maadili. Anapenda sana mali, amejilimbikizia utajiri kuliko kipato chake halisi. Wafuasi wake wanamfanananisha na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Tofauti ya Zuma na Lowassa ni kuwa Zuma alifikishwa mahakamani na kusafishwa na mahakama. Lowassa apelekwe kortini kujibu shutuma za ufisadi, akishinda kesi ndio atakuwa amesafishwa kweli. Si kwa kutumia vyombo vya habari na waandishi wa habari wenye njaa.
 
Mchafu ni mchafu tu na atabaki mchafu. Lowassa ni mchafu wa maadili, hata Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alijua hilo na alituonya tuepukane na huyu mtu. Ni kama nguruwe amezoea kuchea kwenye matope, hata umuogeshe vipi halisi yake ni kuchafuka tu na ataendelea kuwa mchafu tu come what may.

Mpeleke mahakamani kama unao ushaihidi vinginevyo ni msafi ww ndo mchafu.
 
Hivi katika hizi kukuru kakara za kusafishana,ni lini haswa tutasema EL sasa ni msafi na hivyo "akumbatiwe"?

Pls pls, let me know akishakuwa msafi, kwasababu ni almost two years nasikia tu bado yuko anasafishwa.
 
Hakuna ushindani hapa huo ndio ukweli wenyewe, MUMENUNULIWA na Fisadi LOWASA. Njaa zenu mbaya sana
 
na wewe unamsafisha nani? wewe kwa nafasi yako na uelewa wangu kamwe HUWEZI kuniambia nini cha kufanya hata kama nitakuwa mbali na kambi yako. Na kwa taarifa yako sina kambi isipokuwa ninachokataa ni kutaka kutuaminisha jinsi wewe na kambi yako, hasa wanaokutuma kutaka kutufanya tuamini ktk mawazo yenu yenye chuki kwenye biashara zenu.
Unapoongelea kikao cha NEC kwenye Mtanzania, kwani Viongozi wa CCM wamesemaje? -"SIRI ZA VIKAO VYA NEC ZIMEVUJA", sasa nini kosa la magazeti hayo? tuache ushabiki usiokuwa na mwelekeo chanya kwa nchi yetu na badala yake tuelekeze nguvu zetu ktk kukemea maovu ambayo kwa mwelekeo wako, katu huwezi kuyakemea.

Ni kweli wewe ni miongoni mwao.
 
Ufisadi wa Lowassa huu hapa:

1. Kununua jumba la kifahari London, Uingereza, lenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 1 za Tanzania.

Metropolitan police wa Uingereza wanachunguza suala hili. Wamewasiliana na anti-money laundering unit ya Tanzania kuchunguza suala hili.

2. Ufisadi wa Nyumba ya Sanaa

Lowassa amehisika kufanya uporaji wa ardhi ya Nyumba ya Sanaa iliyopo karibu na Movenpik Hotel (zamani Serena Hotel). Nyaraka zinaonesha yeye ni mmiliki wa kampuni inayojenga gorofa kubwa kwenye eneo hilo la Nyumba ya Sanaa.

3. Utajiri usioelezeka (unexplained wealth)

Akiwa kama kiongozi wa umma, Lowassa amejilimbikizia mali nyingi sana za thamani ya mabilioni ya shilingi. Mali alizo nazo haziendani na kipato chake kama kiongozi wa umma. Sheria ya kupambana na rushwa Tanzania iko wazi kuwa kiongozi wowote wa umma mwenye utajiri usioendana na mapato yake halali anastahili kufikishwa mahakamani. Kutokana na sera za kulindana na kuogopana, Lowassa, Andrew Chenge, na viongozi wengine wa umma hawajafikishwa mahakamani kwa kosa hili na PCCB. Pia kwenye fomu za kila mwaka za kutaja mali, Lowassa haja declare assets zake zote. Ana miliki Alphatel, Alpha Schools, Alpha House, apartment blocks Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi.

4. Land grabbing

Alipokuwa Waziri wa Ardhi enzi za utawala wa Mwinyi alihusika na uporaji mkubwa wa ardhi sehemu mbali mbali nchini.

5. Richmond

Lowassa ndiye aliyeagiza TANESCO waporwe madaraka ya kusimamia tenda ya umeme kinyume na sheria ya manunuzi, PPRA. Aliunda kamati ya makatibu wakuu na kusimamia kwa karibu majadiliano ya kamati hii na nRichmond na kuagiza wapewe tenda wakati Tanesco waliikataa Richmond kuwa haifai. Lowassa ndiye mhusika mkuu wa kashfa ya ufisadi ya Richmond ndio maana alilazimika kujiuzulu.

6. Need I say more?

Lowassa ni mchafu wa maadili. Anapenda sana mali, amejilimbikizia utajiri kuliko kipato chake halisi. Wafuasi wake wanamfanananisha na Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Tofauti ya Zuma na Lowassa ni kuwa Zuma alifikishwa mahakamani na kusafishwa na mahakama. Lowassa apelekwe kortini kujibu shutuma za ufisadi, akishinda kesi ndio atakuwa amesafishwa kweli. Si kwa kutumia vyombo vya habari na waandishi wa habari wenye njaa.

Mkuu hapo umemaliza, tungekuwa na TAKUKURU huru na jasiri ingewapeleka Lowassa na Chenge mahakamani leo. Watu kama hawa wala huwashitaki kwa corruption au bribery kwani ngumu kuthibitisha ingawa sote tunajua ni mafisadi. Wakipelekwa kwa criminal offences za abuse of public office na unexplained wealth WALLAHI hawachomoi hawa lazima wahukumiwe tu!
 
Back
Top Bottom