Magazeti yanayomsafisha Lowassa haya hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti yanayomsafisha Lowassa haya hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DOUBLE AGENT, Dec 4, 2011.

 1. D

  DOUBLE AGENT Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ifuatayo ni orodha ya magazeti ya Tanzania ambayo wamiliki wake au wahariri wake au wote wamiliki na wahariri wamekuwa wakitumika kumsafisha Edward Lowassa katika mradi wake wa kutaka kwenda Ikulu 2015 kwa gharama yoyote ile. Magazeti haya yalitumiwa sana kupotosha umma kuhusu matokeo ya vikao vya NEC na Kamati Kuu ya CCM Dodoma juzi na kutoa habari na picha za kumpamba Lowassa kila mara akitumia viongozi wa dini njaa kujisafisha:

  1. Mtanzania na RAI

  Ingawaje hayasomwi tena na Watanzania makini, magazeti haya yanamilikiwa na Rostam Aziz, kingmaker wa viongozi mafisadi Tanzania na chief financier wa Lowassa.

  2. MwanaHalisi

  Gazeti linalomilikiwa na Saeed Kubenea ambaye sasa amefika bei kwa mafisadi na anawatumikia kama kibarua wao kuwasafisha na kuwatukana maadui wao, hususan Waziri Samuel Sitta.

  4. Tanzania Daima

  Gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ambalo mhariri wake mkuu, Absalam Kibanda, yuko kwenye payroll ya Lowassa na Rostam kwa miaka mingi sana

  5. Jamhuri (soon-to-be launched)

  Gazeti la Lowassa ambalo litazinduka hivi karibuni, wahariri wake wakiwa ni vijana wa Lowassa wa siku nyingi -- Deodatus Balile na Manyerere Jackton -- ambao amewaazima kutoka kwenye magazeti ya rafiki yake Rostam. Hii ni baada ya jarida la Lowassa la Umoja linaloendeshwa na Absalom Kibanda wa Tanzania Daima kufeli na mpaka kufikia hatua ya kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.

  6. Mwananchi

  Kuna "mdudu" ameingia hivi karibuni kwenye gazeti pendwa la kila siku la Tanzania ambalo na gazeti hili nalo sasa linatumiwa kwenye mradi wa kumsafisha Lowassa. Hii ilijidhihirisha kwenye mkutanon wa juzi wa NEC ambapo habari kuu iliyotoka kwenye kikao cha NEC iliandikwa na mtu mmoja na kuchapishwa kwenye magazeti matatu -- Mwananchi, Tanzania Daima na Mtanzania -- neno kwa neno.

  7. Daily News

  Kaimu Mhariri Mkuu wa Daily News, Mkumbwa Ally, amejisalimisha kambi ya Lowassa ili athibitishwe na kupewa cheo kama Mhariri Mkuu wa magazeti ya serikali, TSN. Wakati huo huo, gazeti la Habari Leo lililo chini ya TSN limekuwa likipambana kuleta habari za ukweli kuhusu mafisadi. Hii imesababisha habari za Daily News na Habari Leo kuhusu kujivua gamba kutofautiana kabisa wakati yote ni magazeti ya serikali chini ya kampuni moja.

  • Mpaka hivi sasa, genge la kina Lowassa limejaribu na kushindwa kufanikiwa kwenye kila jitihada za kuyaingia au kuyamaliza kabisa magazeti mawili pekee yaliyosimama kidete kuueleza umma wa Tanzania ukweli. Nayo ni RAIA MWEMA na DIRA.
   
 2. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Na wewe uko kwenye mradi wa kumsafisha nani? Isije ikawa kuna habari ikiandikwa tofauti na mtizamo wa kambi yako halafu unasema yamenunuliwa? Je kama yangekuwa yanaandika unavyotaka wewe na kambi yako ungetaka sisi watanzania tuaminije?
  Ushauri kwako: Siyo wote wenye mtizamo hasi ktk hayo magazeti kama unavyotaka wewe na hao waliokutuma. Na kwa taarifa yako; hayo ndiyo magazeti yanayonunuliwa na watanzania kuliko hayo mengine unayofikiri yanaandika tofauti na unavyotaka wewe.
  Halafu lazima ujue kwamba hatuwezi kufikiria sawa unavyotaka wewe!
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Nitaona EL hafai ikiwa utatuthibitishia wahariri wote wa magazeti hayo yote ni wajinga.
   
 4. T

  The Informer Senior Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii orodha si sahihi. Mwananchi halitumiwi na mtu, ni gazeti huru kabisa. Kwani Aga Khan akijua tu wahariri wake wanatumiwa anawafukuza kazi, na Lowassa hawezi kumnunua Aga Khan. Ataishia kuwanunua wahariri wa Bongo kama Kibanda na Kubenea tu!
   
 5. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kama Edward Ngoyai Lowassa Mchafu,Basi Jakaya Mrisho Kikwete ndio Uchafu wenyewe("Kila nilichokuwa nafanya nilikujulisha,Unakumbuka vyema nilivyotaka kuuvunja mkataba ule,nilipokupigia simu ukiwa nje ya nchi...."EL ndani ya NEC,Novemba 26, 2011).Sasa wanasafisha nini mtu bado yupo Magogoni?
   
 6. D

  Dark es Salaam Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio maana Benjamin Mkapa (Rais wa ukweli) aliwahi kusema kuwa waandishi wa habari wa Tanzania ni UCHWARA. Hao kina Kubenea am bao baadhi ya wana JF waliogizani bado wanamuona ni shujaa wao, ni watu wenye roho nyepesi kama kuku. Wote wamefika bei kwa mafisadi. Hii siyo siri, ni jambo linalofahamika sana.
   
 7. REBEL

  REBEL Senior Member

  #7
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mijitu mingine mipumbavu!Duniani hakuna mtu mbaya tu wote ni wa uvuguvugu.Lowassa ana mabaya yake na mazuri yake.Na hata yule mnafiki SAMWEL Sitta ana mabaya yake na mazuri yake!Wewe unataka ukweli uandikwe unaotaka wa mabaya tu ya mtu,hata kama ni ya kutungwa.kazi kwelikweli.
   
 8. N

  Ngao One Member

  #8
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mimi niliacha kusoma MWANA HALISI na Tanzania Daima muda mrefu sasa baada ya kuona jinsi walivyonyea mavi kambi ya kuandika ukweli daima na kupambana na ufisadi na kuhamia kambi ya mafisadi. Waandishi wa Tanzania wenye roho za kuku wanachangia kuliteketeza taifa kama waandishi wa habari wa Rwanda walivyohusika na mauaji ya kimbari ya 1994 nchini mwao.
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Huyu nae yupo kwenye huo mtandao wakumsafisha EL
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kivipi?
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tuthibitishie kama hawezi kuwamtumia
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wote wezi hakuna aliye safi ndani ya ccm
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  we kama mtu ni mwizi alafu anakana na ukweli unaonekana wazi kabisa tumfanyeje? Kubali usikubali Jk na EL wote ni wezi na wote ni magamba
   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nikusahihishe,
  mwananchi si GAZET PENDWA,
  WACHA NIKUTAJIE MFANO WA MAGAZET PENDWA
  RISASI,SANI,TUNU,KIU,UWAZI,HAMU, NA MENGINE YA AINA HIYO
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inaonyesha Tz yote kuanzia kwa wanasiasa hadi vyombo vya habari na usalama wote wananuka rushwa tupu na hili ni janga lingine kwa Taifa
   
 16. E

  EL+RA=UFISADI Member

  #16
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa mtu yoyote makini, ukisoma magazeti ya Tanzania unaona kabisa yako upande gani. Uweledi kwenye uandishi wa habari Tanzania na kufanya kazi bila woga wala upendeleo hakuna kutokana na njaa kali ya waandishi wa habari na wengi wao kutokwenda shule.

  Ndiyo maana magazeti haya mengi yalitumika kujenga hisia kuwa fisadi Lowassa ni victim wa vita ya Urais ya 2015, kumbe ukweli unabaki palepale kuwa huyu ni mtuhumiwa mkubwa wa rushwa. Lazima afukuzwe kwenye chama na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zake.
   
 17. E

  EL+RA=UFISADI Member

  #17
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hali ni mbaya kaka, rushwa imepenya kila mahali. Watu wanajisalimisha kwa mafisadi baada ya kuona upepo unaonesha nguvu yao ya pesa ni kubwa kuliko mfano.
   
 18. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Aliyesema hili ni janga la Taifa yuko sahihi, maana haoa wengine bora tutangulie kaburini tusione haya mauzauza, hakuna amani, hakuna uaminifu, unafiki, Tamaa, ubinafsi na uzandiki ndio sifa kuu ya Mtanzania katika kila tasnia. Tutakutana huko AHERA
   
 19. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #19
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sasa kama anasafishwa na wewe hutaki asafishwe si mchafue. Sasa unataka nani amchafue.
   
 20. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Unatakiwa kupiga kura na kuchagua kiongozi anayekufaa na siyo kwa kuchaguliwa na magazeti.

  Baada ya kusema hivyo hivyo inafaa tusirudie makosa kwa kuchagua wale tulioambiwa kuwa ni WASAFI hapo siku za nyuma.
  Kwa mfano Ilisemwa kwamba
  - Mkapa ni Mr. Msafi, lakini alinunua rada kwa dili, kufanya biashara ikulu, kuanzisha benki, kujiuzia migodi na madudu kibao.
  - Unamjua aliyeitwa askari wa mwamvuli asilia? Ni J. Pombe Magufuli, alibuni wazo la kuuza nyumba zote za serikali mpaka za walimu na kuuza baadhi kwa familia yake.
  - Dr, Kigoda ilitajwa kwamba hamna mtu msafi kama yeye, lakini alijiuzia mwambao wote wa Tanga wenye mikoko yenye utajiri.
  - Akaja Prof. Kapuya, nani asiyejua mafyongo yake, akaishia kuanzisha bendi za muziku wa dansi.
  Na wengine wengi ambao tuliambiwa ni WASAFI, kumbe ni wachafu kuliko computer keyboard.

  BORA ZIMWI LIKUJUALO.
   
Loading...