Mafuta ya Petroli na Dizeli yaadimika vituoni mkoani Katavi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Shughuli za usafirishaji wa abiria kupitia usafiri wa pikipiki na bajaji mkoani Katavi zimesimama kutokana na ukosefu wa mafuta ya petrol na dizeli kwenye vituo vya kuuzia mafuta, hali iliyowaathiri madereva wa vyombo hivyo kukosa mahitaji ya familia zao.

Wakizungumza na mwananchi leo Jumapili, Julai 30, 2023 baadhi ya madereva wa pikipiki na bajaji katika Manispaa ya Mpanda, wamesema zaidi ya siku nne sasa wamekumbwa na kadhia hiyo.

Dereva gari binafsi Masanja Salaganda, amesema kwasasa inawalazimu kupata mgawo wa lita moja moja ya mafuta kutokana na uhaba uliopo ili kila mwendesha chombo cha moto apate ambapo hayakidhi mahitaji.

“Tunajiuliza shida iko wapi labda kuna matatizo kati ya Serikali na wauza mafuta tunaumia sisi watumiaji, tunachoomba Serikali ilitatue suala hili kama dharura,” amesema.

John Shija dereva bajaji amesema takribani siku mbili amezunguka Mpanda nzima vituo vyote hakuna mafuta petrol na dizel na badala yake wananunua ya mgao.

“Unapewa bajaji bosi anataka Sh20,000 jioni kwa siku lakini tunashinda sheli kusubiri mafuta tunatoka saa nane, tunarundika madeni maana fedha ya kupeleka kwa bosi haifikii kwa siku," amesema na kuongeza;

“Tutaishije na familia wakati kula yetu ni sheli watoto wanalala njaa kwasababu shughuli zote zimesimama imepelekea bei kupanda, abiria sehemu ya kulipia Sh1000 wanalipa Sh3000,”

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Madema Ernest Madema, ambaye pia ni mmiliki wa kituo cha kuuzia mafuta cha Mwanone amekiri kuwepo hali hiyo akidai imemlazimu kuomba mafuta kutoka bohari za Serikali.

“Kweli changamoto ilikuwepo inatokana na uhitaji mkubwa, lakini mafuta tumepata imenibidi kuchukua kwenye bohari za Serikali mpaka sasa nimepakia magari manne.

“Mawili yameshaingia, moja liliingia jana usiku, lingine sasa hivi na kesho yataingia mengine mawili hivyo tatizo hili litaisha shida ilikuwa huko Dar es Salaam,” amesema.

Sanjari na hayo hali hiyo pia imesababisha bei ya usafiri kupanda kutoka Sh1000 kwa bajaji na pikipiki hadi kufikia Sh3000 huku wengine wakipaki vyombo vyao na abiria wakiathirika.

MWANANCHI
 
Spika atufanyie wepesi hapo Ewura 😂
Nyooo
20230604_124446.jpg
 
Kuna hizi tuhuma nzito hapa.. Nimeitoa kwenye kundi sogozi..

Kikao cha dharura kati EWURA na waagizaji wa mafuta hakijafua dafu baada ya kutawaliwa na shutuma dhidi ya mkurugenzi wa EWURA na waziri wa nishati na jinsi wanavyojaribu mfumo mzima wa bulk procurement na upendeleo na rushwa zinazofanywa kuwapa watu vibali

Wafanyabiashara hao wamemwambia Mkurugenzi wa EWURA hana uwezo wa kutatua mgogoro huo na mgomo huo kwa kuwa malalamiko yao yako kwake zaidi ya mwaka na hakuna kitu amefanya zaidi ya kutoa vitisho

Kikao hicho kilichosusiwa na wengi wa waagizaji mafuta kilikuwa kitoke na suluhu ya mgogoro uliopo wa kuadimika kwa mafuta na mgomo wa kimya kimya wa waagizaji mafuta.

Kwa mara ya kwanza waagizaji mafuta hao wamesema ndani ya kikao kuwa waziri January Makamba ni mtu asiyejua sekta ya mafuta inaendeshwaje na yeye anachowaza ni kupokea rushwa tu bila kufikiria hiyo ni biashara na watu wanataka kupata faida. Moja ya mjumbe alisema ni bora akatafuta biashara nyingine ya kufanya lakini hawezi kutoa $400,000 karibia 1bn TZS kwa ajili ya rushwa ili apewe kibali ambapo faida ya biashara hiyo haifiki hata hiyo 1bn TZS anayotaka apewe.

Tukiondoka kwenye kikao hicho ni wazi kuwa uhaba na kutokuwepo kwa mafuta na kuanza kuuzwa mafuta kwa magendo kumeanza kusambaa nchi nzima na hii ni dalili kuwa tatizo hili linakwenda kuwa sugu na linakwenda kuathiri sana uchumi wa taifa hili.

Waziri Makamba ndiye anayesababisha mgao wa umeme kimya kimya huku kila kukicha anatokea kwenye makamera anasaini mikataba ya kuzalisha umeme hewa. Lakini tunajua kwenye mikataba hii anachofuata na kukitafuta ni rushwa tu na hakuna kingine. Kwenye hili la mafuta kumedhihirisha jinsi ambavyo rushwa anazozitaka ili kutoa vibali vya kuagiza mafuta zinavyoathiri nchi na uchumi.

Swali je? Haya yote ndiyo ambayo mlikuwa mnataka kuwafanyia watanzania? Mlikuwa mnajenga uchumi kwa miaka miwili mitatu nyuma na ukawa imara sana lengo lenu ilikuwa kuja kuuharibu kwa kuwa na waziri wa hovyo kama huyu?

Tunajua Kinana na kundi lake wanamtetea sana kufa na kupona kwa sababu ni wanufaika wa hizi rushwa na ndiyo maana January Makamba hakauki nyumbani kwa Kinana hapo Masaki.

Kinana ni miongoni mwa wanaotisha mamlaka kuwa huyu akitolewa ataleta mpasuko. Hivi Lowassa alishindwa kuleta mpasuko ataleta mpasuko mtu aliyepata kura chache kuliko zote kwenye ujumbe wa NEC? Huyu alifukuzwa uwaziri na Magufuli alileta athari gani? CCM msitake kujibrand kuwa wizi na rushwa ni sifa ya kuwa mwana CCM. Huyu kijana wenu kashindwa kazi na uwezo hana. Dada yake ambaye ndiyo mficha hela za wizi mkuu anaishi maisha ya anasa sana huku hana kazi anayoifanya nalo hili ni la kusubiri? Anatoa wapi hela ya kukodisha ndege binafsi kwenda kufanya ulevi na uhuni Afrika ya Kusini? Anatoa wapi hela ya kukodisha yatch na kundi la wahuni wenzake na kufanya anasa? Hivi mnawaonaje watanzania?

Haya yote yanafanywa mnataka watu wakae kimya na wakisema mnaanza kuwatafuta muwauwe na kuwapa sumu! Kwani mkiwauwa mafuta yatapatikana? Mkiwapa sumu wakafa umeme utapatikana?

Ifike mahali sasa serikali iamue kutoa kauli kuwa mtu huyu ni wao wanamtuma na hakuna haja ya kulalamika kwa sababu kila anachofanya kuanzia kununua mita za LUKU mbovu , kulipa vyura bila utaratibu, kukwapua mabilioni kwenye mikataba REA,kuficha hela Indonesia ni maagizo yao hivyo watanzania wakae walime maharage na mahindi wasihangaike. TUTAWAELEWA

Narudia tena! Yalikuwa ni makosa makubwa sana kuwarudisha hawa vijana kwenye serikali na yakawa makosa makubwa zaidi kumtudisha god father wao Kinana kwenye chama maana madhara yake ndiyo haya sasa. Majitu MAJIZI haya yanawaza kuitafuna tu nchi na hayana huruma na watanzania. Ndiyo maana kuwezi ona wanaongelea athari wanapata watanzania kwa kukosa mafuta kwa kuwa tu waziri hatoi vibali mpaka apewe rushwa

Kuna siku watanzania itafika watalazimika kuingia barabarani na ikifika hatua hii hawatataka waziri mwizi na mla rushwa atoke bali watataka CCM na serikali nzima iondoke kwa kuwa mnatetea MAJIZI haya ya akina Kinana na Janaury

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikao cha dharura kati EWURA na waagizaji wa mafuta hakijafua dafu baada ya kutawaliwa na shutuma dhidi ya mkurugenzi wa EWURA na waziri wa nishati na jinsi wanavyojaribu mfumo mzima wa bulk procurement na upendeleo na rushwa zinazofanywa kuwapa watu vibali

Wafanyabiashara hao wamemwambia Mkurugenzi wa EWURA hana uwezo wa kutatua mgogoro huo na mgomo huo kwa kuwa malalamiko yao yako kwake zaidi ya mwaka na hakuna kitu amefanya zaidi ya kutoa vitisho

Kikao hicho kilichosusiwa na wengi wa waagizaji mafuta kilikuwa kitoke na suluhu ya mgogoro uliopo wa kuadimika kwa mafuta na mgomo wa kimya kimya wa waagizaji mafuta.

Kwa mara ya kwanza waagizaji mafuta hao wamesema ndani ya kikao kuwa waziri January Makamba ni mtu asiyejua sekta ya mafuta inaendeshwaje na yeye anachowaza ni kupokea rushwa tu bila kufikiria hiyo ni biashara na watu wanataka kupata faida. Moja ya mjumbe alisema ni bora akatafuta biashara nyingine ya kufanya lakini hawezi kutoa $400,000 karibia 1bn TZS kwa ajili ya rushwa ili apewe kibali ambapo faida ya biashara hiyo haifiki hata hiyo 1bn TZS anayotaka apewe.

Tukiondoka kwenye kikao hicho ni wazi kuwa uhaba na kutokuwepo kwa mafuta na kuanza kuuzwa mafuta kwa magendo kumeanza kusambaa nchi nzima na hii ni dalili kuwa tatizo hili linakwenda kuwa sugu na linakwenda kuathiri sana uchumi wa taifa hili.
.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waagizaji wakishauza mafuta yao ndani, inachukua muda kuweza kupata dollar ya kuagizia mzigo mwingine.

Kama bank kuu aina hata ya kuagizia mafuta ya kuwapa waagizaji wa mafuta; commodity ambayo ni muhimu kwa uchumi ndio tuelewe tatizo la uhaba wa dollar sio dogo.
 
Kuna story nyingi mjini, wengine wanasema wafanyabishara wanafanya mgomo baridi kutokana na rushwa na ubabe wa wizara ya nishati. Huku wengine wakisema taifa limekubwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni. Kile kidogo tunachoingiza kinaishia kulipa ripa za mikopo mizito mizito aliyokopa kwa pupa ndugu Ng'wigulu.
 
Back
Top Bottom