Watu 8 wamefariki dunia kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo,kinondoni wamefariki watu 6 na Temeke watu wawili.
MAFURIKO DAR - BARABARA YA MOROGORO YAFUNGWA
Kufuatia mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha mafuriko ambayo yamepelekea barabara kadhaa kufunikwa na maji; Serikali imetangaza kuifunga Barabara ya Morogoro katika eneo la Jangwani kufuatia daraja kufunikwa na maji.
Aidha, watu wametakiwa kuondoka mapema maeneo ya katikati ya ambako kuna foleni ndefu za magari na kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa, mvua hizi zitaendelea kunyesha na ambapo madhara yanaweza kuwa makubwa zaidi.
Hadi wakazi wengi wa maeneo ya mabondeni wameripotiwa kuathiriwa na hali hii kwa nyumba zao kujaa maji na mali zao kusombwa na maji.
Mtu mmoja amefariki Dunia baada ya kusombwa na Maji kutokana na mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea Kunyesha Dar es salaam.
Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha usiku kucha nimepita baadhi ya mitaa alfajiri hii na kukuta wananchi wakikimbia nyumba zao sababu ya kujaa maji ndani.
Nimepita maeneo ya Tabata, Buguruni, Vingunguti nimekuja kuiona tena hali hiyo Kigogo na sasa nipo magomeni sijajua kwa ndugu zangu pale Kino kutakuwaje.
Leo watu wnaopiga Pepa, za NBAA na form six kazi wanayo
Yeah nilikuwa natoka kinyerezi kwa mchepuko nipo ofisini now. Nilikatizia barracuda.
Hakuna anaependa kujenga bondeni ni maisha tu, mtu hela ya kujenga pazuri hana na kachoka kupanga.
Hehehe,aiseee
Aisee hapo kino nilihama mwezi uliopita. Leo watakuwa wanaogelea hapo
Mkuu kino ndiyo / iko wapi?