Mafunzo ya njiwa...

Mafunzo ya njiwa...

Njiwa anachukua muda gani mpaka kuanza kutaga mayai
 
Kuanzia mwaka 1994,nilipokuwa darasa la nne, hadi mwaka 2000 nilipokuwa kidato cha tatu, nilikuwa nafuga njiwa. Nilifanikiwa kuwa na njiwa takribani 2000. Kilichofanya nisiendelee kufuga ni kuhamia kwangu Bweni nikiwa kidato cha tatu.Nyumbani hakukuwa na muangalizi mbadala kwangu.

Kwa miaka 6 ya ufugaji wa njiwa, nimepata mafunzo mengi sana. Nitashiriki nanyi katika mafunzo hayo kutokana na nilichokiona na kukizoea.
Njiwa 2000? Uliwajengea nyumba?
 
Napenda Sana Hawa viumbe
Miaka ya 1980+ ilikuwa kama fasheni hivi, kwa vijana/watoto wa kiume Mbeya mjini kuwafuga ndege hawa.
Binafsi, kuna rafiki yangu mmoja tulikuwa darasa moja pale Azimio shule ya msingi, yeye akiishi Jacaranda, nami maeneo ya REJIKO, aliniuzia wawili, dume na jike. Sasa, ilikuwa, ukiwapata wakubwa wanaoruka, basi unawatoa manyoya yale marefu kwenye mabawa yao ili wasiruke, kabla hawajazoea makazi mapya. Wengine walikuwa wanatumia njia katiri ya kuwatengua mabawa, na wataanza kuruka baada ya kupona.

Sasa, njiwa wangu, walipoanza kuokota majani yakiwa ni maandalizi ya kutaga, jike akakanyagwa na gari na kufa. Akabaki dume peke yake. Sasa hili dume, lilikuwa lina tabia ya kutoka pale home, na kwenda mbali nisikokujua. Baada ya siku chache, akaja na jike, alikompata, hataaa sijui.

Baada ya siku chache, hilo jike likataga mayai mawili. Baadaye nikapata vifaranga. Kabla hawajaanza kuruka vizuri, wakataga tena. Sasa, kimbembe kilichoniudhi, na kuchukia kuwafuga hao ndege, ni tabia iliyokuwa nayo hilo dume. Pamoja na kuwa nilijenga mabanda mengi, lakini watoto wake wakianza kuruka vizuri tu, alikuwa anaondoka nao, na kuwaacha huko huko. Kwa hiyo muda mrefu, nilikuwa nina vifaranga tu, wakikua, wanahamishwa.

Nikaona huo ni ujinga, walipokaribia kuanza kutaga, nikawachinja, vifaranga nikawauza, kwani walishaanza kula wenyewe.
Wakati ule, tulikuwa tunaambiwa kuwa, kuna matunda fulani hivi, yana umbo kama chungwa hivi, ukiyaning'iniza kwenye banda, hawatoroki/hawahami. Lakini waapii. Pia, tulikuwa tunaambiwa kuwa, kikitokea kilio/msiba hapo nyumbani, basi tupia ushanga kwenye mabanda, ili wasiondoke. Kwa sababu hakikutokea kilio wakati ninafuga hao ndege, hivyo sina uhakika.

Lakini, ukiwa na hao ndege wengi, na wakiwa na rangi tofauti tofauti, ni burudani tosha kuwaangalia!
 
Miaka ya 1980+ ilikuwa kama fasheni hivi, kwa vijana/watoto wa kiume Mbeya mjini kuwafuga ndege hawa.
Binafsi, kuna rafiki yangu mmoja tulikuwa darasa moja pale Azimio shule ya msingi, yeye akiishi Jacaranda, nami maeneo ya REJIKO, aliniuzia wawili,
Mkuu ulikuwa hujalipia mahari ya huyo jike ndiyo maana dime likipata Watoto wanarudishwa kwao
 
Pia njiwa ndo kiumbe cha pili baada ya MWANADAMU kufanya ngono km STAREHE! viumbe walobaki wote NGONO ni kwa ajili ya UZAZI tu
Yeah nakubali njiwa wanapenda romance Sana nalishuhudia daily hili
 
Nami nimefuga Sana njiwa.
Naweka nyongeza yangu
1. Njiwa Mara nyingi hutaga mayai mawili. Ila wapo wanaotaga mayai matatu. Nilikuwa nao wawatu.

2. Kulisha makinda kwa sehemu kubwa ufanywa na dume. Ila kulalia mayai sehemu kubwa ufanywa na jike.

3. Njiwa analalia mayai siku 14/15 sio siku 21.

4. Njia Mara njingi Sana wanaanguliwa dume na jike, ndo uona Kaka na dada. Mara chache mnooo kuanguliwa madume tupu, ama majike matupu. Ila utokea.

5. Wapo njiwa Malaya pia. Ila Mara chache mnooo. Nilikuwa na madume yana majike mawili.

NB: njiwa jike uvutiwa na dume lenye nguvu
 
Nakataa hii dhana. Njiwa upenda sehemu yenye msosi wa uhakika. Ukiwa unawalisha vzr hawahami.
Mimi nimechinja wanaona. Wamevamiwa Mara kadhaa na paka na kuliwa lakin hawajahama
Jambo hilo ni kweli. Njiwa hukamatwa hata hadharani. Lakini huchinjwa sirini. Kinyume chake wanaruka wote kwa pamoja na kupotea
 
Njiwa hawahami kwa kuchinjwa mwenzao. Hawapend usumbufu wa Mara kwa Mara, kushikwa shikwa bandani. Kama utakuwa na utaratibu mzuri Wala hawaami
Nini inapelekea hiyo halii ya wao kuruka na kupotea kushuhudia mwenzao akichinjwa
 
Back
Top Bottom