Mafunzo ya njiwa...

Mafunzo ya njiwa...

Mimi nimesikia njiwa ni ndege wa baraka sana kiasi kwamba
kama una mikosi au nuksi kubwa kubwa huwezi kuwafuga
hapa nazungumzia watu kama wauaji
au wachawi sugu nasikia njiwa hawakai majumbani mwao

au watu wenye kufanya taboo kama kutembea mtu na mzazi wake na kadhalika

Mkuu,umenena mambo ya kweli. Nimejionea kwa miaka 6
 
Sijawahi kujaribu kumfunga barua apeleke Tu na I wish nifanye hiyo maana wanasema kua eti ukishamfunga unamuonesha na picha ya yule unaempelekea barua na ukimwambia usiondoke had akujibu akifika huko haondoki had apewe majib arudishe hii sijawah hats ishuhudia na sinaa hakika if so

Njiwa wa Tanga wanaweza!!
 
Kuanzia mwaka 1994,nilipokuwa darasa la nne, hadi mwaka 2000 nilipokuwa kidato cha tatu, nilikuwa nafuga njiwa. Nilifanikiwa kuwa na njiwa takribani 2000. Kilichofanya nisiendelee kufuga ni kuhamia kwangu Bweni nikiwa kidato cha tatu.Nyumbani hakukuwa na muangalizi mbadala kwangu.

Kwa miaka 6 ya ufugaji wa njiwa, nimepata mafunzo mengi sana. Nitashiriki nanyi katika mafunzo hayo kutokana na nilichokiona na kukizoea.

Kwanza, njiwa wana wivu. Dume la njiwa haliruhusu kabisa jike lake kufuatwa au kuvutiwa na dume lingine. Wivu huongezeka mno wakati jike anapokaribia kutaga. Dume husika humtinga jike popote aendapo na kumfukuza ili aelekee hasa tunduni. Wivu wa hali ya juu.

Pili, njiwa wana mapenzi, ikiwemo huba (intimacy) na uaminifu.Njiwa hugawana wawili wawili-jike na dume kwa kila kundi. Ni kama ndoa hivi. Hapo,kila mmoja huwa na huyo huyo tu. Hata pale jike au dume fulani linapokosekana,anayebakia hapati mwingine hadi pale ambapo upungufu utajitokeza mahali pengine au mpya kuletwa. Hii ina maana kuwa,kama dume ni moja na majike ni mawili au madume mawili na jike ni moja, hakutakuwa na mapenzi yoyote.

Pia, njiwa 'hula denda' kabla ya kupandana. Denda husaidia kuamsha hisia za mwenza. Ya kwamba, njiwa huandaana kabla ya 'majambo'.

Tatu, njiwa husikitika. Panapotokea msiba, njiwa wote husimama kwa mguu mmoja kama alama ya huzuni na masikitiko. Siku hiyo,mapenzi na kula husimama kwa muda.Ilikuwa ikinipasa 'kuwaambia' msiba husika pale ili kuwarudisha kawaida. Kama taarifa haitolewi,wote huruka na kupotea pindi mwili wa marehemu unapotolewa ndani.

Nne, njiwa wana uelewa mkubwa. Huikariri mbinja ya mfugaji. Mbinja ikibadilishwa,hawaji. Hii hutumika kuwaita ili waje kula. Kwa kufurahi kwao,njiwa waweza kutua mabegani,kichwani na viganjani huku wakijidai kwa furaha. Wakati wa kula,njiwa hawapigani lakini kila mmoja hula kwa kasi kubwa na akitosheka huondoka kwenda kupumzika.

Tano, njiwa husaidiana.Hapa ni hasa jike na dume lake.Kusaidiana kwao hasa huanzia pale jike linapotaka kutaga. Ni mayai mawili tu. Wakati huo,dume humsaidia jike kumpelekea vijiti na manyoya kwa jike kutengeneza kiota ndani ya tundu rasmi lililotengenezwa. Halafu,dume na jike husaidia katika kulalia mayai yao.Hulalia kwa siku 21. Hufanya zamu. Tena,husaidiana katika kulisha makinda na kuyafunza kuruka na kadhalika.

Kiukweli,kupitia njiwa wangu nimejifunza mambo mengi. Mengine nitaandika siku nyingine. Wameniongezea vitu maishani. Asanteni njiwa wangu!

Unanikumbusha enzi za kombokombo zamani sana umenifanya ntamani kulia nkikumbuka
 
Ni kweri yte uloeleza hsa kutochukuliana madem tulikuwa tunabadilishana km una madume mawili araf mwenzako ana majike mawili mnabadilisha unampa jike anakupa dumee ilikuwa poa sana kitambo hcho mwananyamala home hyo namkumbuka jamaa yangu mmoja anaitwa rama mijicho tulikuwa tunafanya sana mchezo huo sm tyme JF inakupa raha sana
 
Makinda (watoto) wakifikia umri wa kujitegemea ufukuzwa bila huruma hivyo mfugaji lazima uongeze matundu. Kwa Malkia Elizabeth II wamejaa kwenye hii square jijini London.

Last edited by a moderator:
Mimi nimesikia njiwa ni ndege wa baraka sana kiasi kwamba
kama una mikosi au nuksi kubwa kubwa huwezi kuwafuga
hapa nazungumzia watu kama wauaji
au wachawi sugu nasikia njiwa hawakai majumbani mwao

au watu wenye kufanya taboo kama kutembea mtu na mzazi wake na kadhalika

Itakuwa kuna ka UKWELI flani amazing.

Mjombangu alikuwa Sheikh, na alikuwa mfugaji mzuri wa njiwa, jirani yetu kulikuwa na "BIBI wa busara", ajabu njiwa wa mjomba walikuwa wengi kiasi baadhi kuhamia kwa majirani lkn hawakuwahi kuhamia kwa Bibi huyu!
 
Huwaambia kwa lugha ya Kiswahili tu kwa maneno-taarifa. Kwa mfano: "Jamani hapa kuna tatizo limetokea.Kuna msiba. Ndiyo maan kuna watu wengi na vilio.Msishangae wala kushtuka." Wakati wa kusema hivyo,ni wakati wa kuwapa chakula kwa pamoja ili waje wote mahali fulani

Wakati wa utoto wangu, hii kazi ya kuwapa njiwa taarifa za msiba nilikuwa naifanya Mimi kwa niaba ya mjombangu mfugaji!

Hata njiwa wa nyumba za jirani, nilikuwa naenda kuwapa taarifa huku nikiwa nawapa mtama!

Taarifa za kazi yangu hii zilifika shuleni, wengi walikuwa wananshangaa!
 
Zile mechi za kishule ama mtaani, tukiwa wadogo, nlikuwa ili kuwatisha tu wapinzani, naenda uwanjani na njiwa niliemfunga hirizi mguuni na kumrusha hewani! Ile taharuki ilikuwa burudani tosha
 
Kuanzia mwaka 1994,nilipokuwa darasa la nne, hadi mwaka 2000 nilipokuwa kidato cha tatu, nilikuwa nafuga njiwa. Nilifanikiwa kuwa na njiwa takribani 2000. Kilichofanya nisiendelee kufuga ni kuhamia kwangu Bweni nikiwa kidato cha tatu.Nyumbani hakukuwa na muangalizi mbadala kwangu.

Kwa miaka 6 ya ufugaji wa njiwa, nimepata mafunzo mengi sana. Nitashiriki nanyi katika mafunzo hayo kutokana na nilichokiona na kukizoea.

Kwanza, njiwa wana wivu. Dume la njiwa haliruhusu kabisa jike lake kufuatwa au kuvutiwa na dume lingine. Wivu huongezeka mno wakati jike anapokaribia kutaga. Dume husika humtinga jike popote aendapo na kumfukuza ili aelekee hasa tunduni. Wivu wa hali ya juu.

Pili, njiwa wana mapenzi, ikiwemo huba (intimacy) na uaminifu.Njiwa hugawana wawili wawili-jike na dume kwa kila kundi. Ni kama ndoa hivi. Hapo,kila mmoja huwa na huyo huyo tu. Hata pale jike au dume fulani linapokosekana,anayebakia hapati mwingine hadi pale ambapo upungufu utajitokeza mahali pengine au mpya kuletwa. Hii ina maana kuwa,kama dume ni moja na majike ni mawili au madume mawili na jike ni moja, hakutakuwa na mapenzi yoyote.

Pia, njiwa 'hula denda' kabla ya kupandana. Denda husaidia kuamsha hisia za mwenza. Ya kwamba, njiwa huandaana kabla ya 'majambo'.

Tatu, njiwa husikitika. Panapotokea msiba, njiwa wote husimama kwa mguu mmoja kama alama ya huzuni na masikitiko. Siku hiyo,mapenzi na kula husimama kwa muda.Ilikuwa ikinipasa 'kuwaambia' msiba husika pale ili kuwarudisha kawaida. Kama taarifa haitolewi,wote huruka na kupotea pindi mwili wa marehemu unapotolewa ndani.

Nne, njiwa wana uelewa mkubwa. Huikariri mbinja ya mfugaji. Mbinja ikibadilishwa,hawaji. Hii hutumika kuwaita ili waje kula. Kwa kufurahi kwao,njiwa waweza kutua mabegani,kichwani na viganjani huku wakijidai kwa furaha. Wakati wa kula,njiwa hawapigani lakini kila mmoja hula kwa kasi kubwa na akitosheka huondoka kwenda kupumzika.

Tano, njiwa husaidiana.Hapa ni hasa jike na dume lake.Kusaidiana kwao hasa huanzia pale jike linapotaka kutaga. Ni mayai mawili tu. Wakati huo,dume humsaidia jike kumpelekea vijiti na manyoya kwa jike kutengeneza kiota ndani ya tundu rasmi lililotengenezwa. Halafu,dume na jike husaidia katika kulalia mayai yao.Hulalia kwa siku 21. Hufanya zamu. Tena,husaidiana katika kulisha makinda na kuyafunza kuruka na kadhalika.

Kiukweli,kupitia njiwa wangu nimejifunza mambo mengi. Mengine nitaandika siku nyingine. Wameniongezea vitu maishani. Asanteni njiwa wangu!
Hiyo nzuri iandikie then uitoe gazetini. Ji moja ya tafiti nzur ya kipekee. Unaweza kwenda mbali zaidi kuwachunguza na ikakutoa kimaisha
 
Makinda (watoto) wakifikia umri wa kujitegemea ufukuzwa bila huruma hivyo mfugaji lazima uongeze matundu. Kwa Malkia Elizabeth II wamejaa kwenye hii square jijini London.

Asante sana Mkuu Mwanamayu kwa video yako. Imenogesha mada yangu
 
Last edited by a moderator:
Daaaah....nasisimka balaa nikiisoma hii story za njiwa. Natamani niisome kila mara. Nimeipenda sana na nitajawafuga tu lazima. Inshallah
 
Back
Top Bottom