Mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2016

Mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2016

Eti mzee Waitara mjukuu wake akose fomu ya kwenda jkt mpaka akazunguke uwanja? au Msuguli na Muhuga wakati huo utaratibu ulikwepo kitambo tu, familia wa Nyerere yenyewe wanapewa fomu 50..wanawapa wajukuu na marafiki.

Nenda uko jkt utakutana na watu kutoka Butiama mpaka utashangaa
Naweza kukubaliana na wewe kwasababu kwa miaka iliyopita Msuguli alikua anagawa form sana na ushahidi wa hilo,siwezi kusemea ya huu mwaka kwa sababu sina uthibitisho.
 
Ngoja tuangalie hii muvi ila ukweli ni huo baba kanituma hamna msikariri zama zimebadilika endeleeni kujifariji
mnajua kukatisha watu tamaa nyie afu wewe kama ulifanya usahili basi wewe ni askari feki jeshini hatukatishani tamaa afu kuhusu fomu lazma hiyo
 
mnajua kukatisha watu tamaa nyie afu wewe kama ulifanya usahili basi wewe ni askari feki jeshini hatukatishani tamaa afu kuhusu fomu lazma hiyo
Askari feki ni wew unayehamasisha wenzako mpite kwa njia ya rushwa jeshin hamna rushwa mbona unatokwa mapovu sana ukweli unauma lqkin lazima usemwe na nasisitiza acha upotoshaji vijana mjipange mwakan usaili baba kanituma hakuna
 
Hivi mkuu unacheo gani jeshini?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nilishazionaga kitambo izo ishu za baba kanituma na kuna madogo nilitaka niwafanyie kupitia MTU moja mkubwa sana hapa nchin ktk chombo ambaye alikua anawapa fomu ndug zake wanaziuza na wengi tuu wapo chomboni kupitia yeye lakn mwaka huu alisema fomu hazitatoka
 
Masada jamani mimi baba kunitumia... ' baba amenipa chance ya kuchagua kambi yoyote ya Jakata, naomba kujua kambi hisiokua na shuruba Sana.... Si mnajua tena baba kanituma wengi wetu mayai.....
 
Masada jamani mimi baba kunitumia... ' baba amenipa chance ya kuchagua kambi yoyote ya Jakata, naomba kujua kambi hisiokua na shuruba Sana.... Si mnajua tena baba kanituma wengi wetu mayai.....
Jeshi halina Double Standard, Kama Umeamua Kwenda Jeshi Tambua ile ni Kazi ya Kiume... Kama wewe Mayai bakia home endeleaKula Mayai ya Kuku Uwafugao hapo Nyumbani.
 
Jeshi halina Double Standard, Kama Umeamua Kwenda Jeshi Tambua ile ni Kazi ya Kiume... Kama wewe Mayai bakia home endeleaKula Mayai ya Kuku Uwafugao hapo Nyumbani.
Kazi ya kiume Lakin Kuna wanawake pia.. Pia hali ya hewa, na mazingira tofauti
 
Baba Kantuma wataenda ila sio wote. Wale wenye chance za Kibeto tu. kama mbuyu wako ni luteni subiri nafac mwakani uende ukaombe wilayani.
 
Nafasi zimeshaanza kutangazwa ktk baadhi ya wilaya zenu hivyo kwa wale wanaohitaji nenda ktk wilaya yako husika ktk office za mshauri wa mgambo
430615db541eb94305fd3c27653afcbd.jpg
54639a4f587a961997fd5c08cde08986.jpg

Kwa wale wa wilaya ya kinondoni mkoa wa dar es salaam hiyo hapo juu

===================

TANGAZO

180681_158735330845567_2210285_n.jpg

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, anawatangazia vijana wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2016.

Barua zilizoainisha sifa za kijana kujiunga na mafunzo ya JKT zimetumwa kwa Waheshimiwa Wakuu wa mikoa. Mchakato wa zoezi la kuwapata vijana wenye sifa unaanza Aprili 2016 hadi tarehe 20 Mei 2016.

Sifa za mwombaji ni kama zifuatazo:-

1. Awe raia halisi wa Tanzania.

2. Umri. Kwa vijana wenye elimu ya Darasa la saba hadi kidato cha sita ni miaka 18 hadi 23.Vijana wenye elimu ya Stashahada umri ni miaka 18 hadi 26 na Vijana wenye elimu ya Shahada na kuendelea umri ni miaka 18 hadi 30.

3. Awe na afya njema, akili timamu.

4. Asiwe na alama yeyote ya michoro mwilini (Tattoo).

5. Mwenye tabia nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.

6. Kwa vijana waliomaliza elimu ya Sekondari kidato cha nne wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2010, 2011, 2012, 2013 na 2014 wenye ufaulu ufuatao:-

(a) Waliomaliza 2010 hadi 2012 wawe wamefaulu na wawe na alama (Points) zisizopungua 32.

(b) Waliomaliza 2013 wawe wamefaulu na wawe na alama (Points) zisizopungua 38.

(c) Waliomaliza 2014 wawe wamefaulu na wawe na GPA isiyopungua 0.6.

7. Awe na elimu ya msingi aliyehitimu darasa la saba.

8. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).

9. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving Certificate)

10. Awe na cheti halisi cha matokeo (Original Academic Certificate/Transcript).

11. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.

12. Asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma.

13. Asiwe amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na yanayofanana na hayo..

Waombaji wenye sifa wapeleke maombi yao kwa Waheshimiwa wakuu wa mikoa. Makao Makuu ya JKT hayatapokea na hayapokei maombi yoyote, kwa vijana watakaoomba nafasi hizo wazingatie maelekezo yatakayotolewa kuepuka usumbufu.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya JKT

Tarehe 05 Aprili 2016

Chanzo: TANGAZO MAALUM VIJANA WA KUJITOLEA 2016
Jkt ni jipu aisee kuna wadogo zetu kule wapo tangia july 2015 hadi leo wanakula msoto tu hamna cha ajira wala nini soon miaka miwili tena wengine wana degree mpaka master pia wapo kudaaaaaaaadeki walahi

Posho kwa mwezi sh elfu 50 tu eti
 
Jkt ni jipu aisee kuna wadogo zetu kule wapo tangia july 2015 hadi leo wanakula msoto tu hamna cha ajira wala nini soon miaka miwili tena wengine wana degree mpaka master pia wapo kudaaaaaaaadeki walahi

Posho kwa mwezi sh elfu 50 tu eti
Nani kakuambia jkt inaajiri?
Umeshaambiwa unaenda kujitolea kule then kupata nafasi vyombo vingine ni mambo ya Bahati tuu na usifikiri hapo unaowasemea watarudi wote kuna watakaobahatika kuajiriwa
 
Back
Top Bottom