Mafundisho ya ndoa miezi tisa ni sahihi?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,694
106,841
Wakuu,

Kikawaida mafundisho ya ndoa za kikatoliki hua kati ya wiki 2 mpaka mwezi 1 lakini katika jimbo XXX (Jimbo katoliki) na parokia zake zote hali ni tofauti kabisa mafundisho ya ndoa ni lazima uhudhurie kwa miezi 9. Watu wamelalama kuhusu hili lakini askofu wala hana habari sana paroko atakwambia kama hujarizika na utaratibu hama Makanisa mengine.

Since utii ndio nguzo ya ukatolikii watu inabidi tuwe wapole tutii...yaani unahudhuria mafundisho mpaka unaweza kuachana bure na mchumba wako mkiwa bado mpo kwenye mafundisho.

Lakini vijana wa hovyo hovyo wamebuni mbinu ya kukwepa miezi hiyo ya mufundisho. Ambayo sitaisema Ili kama paroko au askofu husika akisoma mada hii asigundue siri za kambo😅

___

Unaweza kujiuliza miezi tisa yote hiyo wanafundishwa vitu gani? Wanafundisha vitu viiiingi sana, hadi wanasaikolojia kama Carl Jung na Maria Montessori wanawasoma. Baadhi ni topic zifundishwazo
  • Saikolojia, hasa maswala ya Personalities
  • Reproduction
  • Genetics
  • Malezi ya mtoto from prenatal to postnatal Stage
  • Uzazi wa mpango
  • Sheria za ndoa KiKatiba
  • Sheria za ndoa Kikanisa
  • Jinsi ya kumuandaa na kumlizisha mwenza wako kitandani 🤣🤣🤣🏃🏃🏃
  • Nk..
Halafu kuna mtihani na nilazima ufaulu... Nongekua na soft copy ningewawekea mjisomee.
Chini hapo nitaweka baadhi ya maswali yanayoulizwa kwenye paper.

Wakuu swala hili ni swa kweli jamani kufuata mafundisho kwa muda wote huo?

IMG-20230903-WA0007~2.jpg

IMG-20230903-WA0008~2.jpg
 
Back
Top Bottom