Takalani Sesame
JF-Expert Member
- Jun 24, 2008
- 588
- 161
KWA KWELI CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza mema katika miaka 25. Ninarudia tena ku
waomba watanzania tumpe kura za ndio Mgombea wetu kipenzi cha watu Mhe. JAKAYA MRISHO
KIKWETE tarehe 31 Oktoba 2010.
Hivi CCM iko duniani miaka 25 kumbe? Kuanzia 1977 mpaka 1985 ilikuwa haipo au mnaficha kitu?
Nchi imejaa wagonjwa wa akili. Kazi kweli kweli.
wa ndima hiyo imetulia
TULIAHIDI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Ujenzi wa miradi 15 ya barabara kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa
Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010 huku ujenzi ambao
unaendelea ukiwa ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4
huwa nazunguka sana nchi hii kwenye shughuli zangu za kutafuta riziki sio kuomba riziki naomba nieleweke vizuri hapo. Hizo barabara za lami za umbali huo unaotaja ziko nchi gani? kama ile ndefu aliyoiacha Mkapa (MZ -DM)n mpaka leo haijaisha, hizo zilizokamilika kwanini hamzitaji kwa majina.
Tusiongea kiushabiki kusifu pasipo sifa. Napenda sana nisome tumefanya hili mpaka hapa tumekwama hapa, hiyo ndiyo hoja. lakini kusema tumejaribu hilo haliniingii akilini kwani kuongoza nchi sio kufanya majaribio. experiments zinafnywa na wanasayansi wakifanikiwa wanatoa taarifa kwa utekelzaji rasmi.
naipenda tanzania. nawapenda watanzania. mimi ni mtanzania halisi
Kumbe kweli tunaona. Wiki iliyopita nilikwenda kijijini kwetu mpaka leo barabara inayotumika ni ile ambayo mkoloni alipitisha grader, ever hakuna ofisa wa wizara hiyo aliyetembelea eneo hilo kuona hali ya barabara. Barabara wanazosema waheshimiwa niyingi ni zile alizojenga mwingereza na sio mpya, wanazungumzia kuziba mashimo au kukarabati kama zile za Mandela na Morogoro, upuuzi tu. Kuwadanganya wajinga.
Hakuna barabara yoyote ambayo awamu ya nne wanaweza kujisifia, ni porojo tu.
Hiyo picha hapo juu haina uhusiano wowote na Tanzania, CCM ili ahidi KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA AFYA
Kutoka mwaka 2005 hadi 2009,jumla ya zahanati 464,vituo vya afya 98
na nyumba za waganga 394 zilijengwa.Zahanati 1,037,vituo vya afya 285 na hospitali 112 zimekarabatiwa.
Vifo vya watoto wachanga vimepungua hadi kufikia 58 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai mwaka 2009/2010.