Mafanikio ya serikali ya CCM chini ya Kikwete, DETAILED!

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
k37gxu.jpg

2hf2aec.jpg

1051k53.jpg


magari_serikali.jpg

Nimejaribu kufanya photo-journalism kwa kukusanya picha za matukio mbalimbali ya Kikwete a.k.a "Chaguo la Mungu" na kumwachia tafakuri msomaji aamue kama anastahili kurejea Ikulu.

Maji+1%5B1%5D.jpg

MAJI BWERERE

MAISHA+BORA.jpg

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YAMEWEZEKANA

HURUMA.jpg

USHAHIDI WA MAISHA BORA UNAONEKANA HATA KWA WATOTO WADOGO

ADHA+YA+MAJI.JPG

YOU SEE, TATIZO LA MAJI MIJINI NA VIJIJINI LIMEPATIWA UFUMBUZI WA KUDUMU

USAFIRI+WA+WANAFUNZI.jpg

TATIZO LA USAFIRI KWA WANAFUNZI MIJINI LIMEMALIZWA.MNATAKA MAISHA BORA YAPI ZAIDI YA HAYA?

POLISI+MSIMBAZI.jpg

MNAONA?POLISI WENYE MAKAZI DUNI SASA WANA SWIMMING POOL HAPO MSIMBAZI POLICE FLATS.MAISHA BORA KWA POLISI YAMEPELEKEA WAACHE KUDAI RUSHWA NA KUBAMBIKIZA KESI KWA WALALAHOI

MATREKTA+KILIMO+KWANZA.JPG

BARABARA ZETU NI MARIDADI.TUMELETEWA MATREKTA MENGI MNO KWA KILIMO KWANZA HADI INABIDI YAFANYE KAZI YA KUVUTA MALORI.EBO!KWANI CHA AJABU NINI TREKTA KUVUTA LORI?NI FERI ZA NCHI KAVU HIZO

MATOPE.JPG

CHAGUA KIKWETE NA CCM KWA BARABARA BORA.NA 2010-2015 BARABARA KAMA HIYO HAPO JUU ZITAKUWA UPGRADED TO FLYOVER.
 
Kwanini unamashaka, hakuna kitu chochote kitakachosababisha hii mada iondolewe, maana hizo ni picha halali za Mkuu, na kauli ya "chaguo la Mungu" ilitolewa na Methodius Kilaini!

Picha hizo ni nzuri sana!

Mkuu aikuwa anamaanisha kuwa maisha bora kwake na familia yake, ndo maana sasa hivi amewaajiri wanafamilia wote kwenye kampeni, wanatumia fedha za wavuja jasho bila huruma!
 
Aisee ile picha ya mwanzo naona mkuu wangu alivyokuwa anapepea angani jamaika wakati wananchi wake kule same waliangukiwa na maporomoko ya mlima na wakati huohuo wananchi wa mara kama sikosei 15 walichinjwa kwenye vita vya kikabila
 
Tumechoka na nyimbo za kukosoa, tunahitaji kusikia nini kinaweza kufanywa na namna gani kinaweza kufanyika kuendeleza nchi yetu. Mtizamo wangu vyama vyote vina nia njema ya kuendeleza nchi lakini je kinachoelezwa ni FEASIBLE?? hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa ufundi wa kukosoa. We need constructive ideas man.
 
Tumechoka na nyimbo za kukosoa, tunahitaji kusikia nini kinaweza kufanywa na namna gani kinaweza kufanyika kuendeleza nchi yetu. Mtizamo wangu vyama vyote vina nia njema ya kuendeleza nchi lakini je kinachoelezwa ni FEASIBLE?? hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa ufundi wa kukosoa. We need constructive ideas man.

Bila kukosoa tutaenenda vipi? Nchi itapataje maendeleo?
 
Tumechoka na nyimbo za kukosoa, tunahitaji kusikia nini kinaweza kufanywa na namna gani kinaweza kufanyika kuendeleza nchi yetu. Mtizamo wangu vyama vyote vina nia njema ya kuendeleza nchi lakini je kinachoelezwa ni FEASIBLE?? hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa ufundi wa kukosoa. We need constructive ideas man.

The problem is corruption. Good ideas are already in place. Ideas will never work unless implemented. The implementation require good governance. So I would say the constructive is to remove CCM from the power and give Slaa who has shown and interested in fighting corruption.
 
Tumechoka na nyimbo za kukosoa, tunahitaji kusikia nini kinaweza kufanywa na namna gani kinaweza kufanyika kuendeleza nchi yetu. Mtizamo wangu vyama vyote vina nia njema ya kuendeleza nchi lakini je kinachoelezwa ni FEASIBLE?? hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa ufundi wa kukosoa. We need constructive ideas man.
:A S 100:..... kukosoa kunasaidia kuifundisha jamii ione ukweli, hasa kwa wale wasioyaona makosa... tutaedelea tu kukosoa hata CCM ikichukia lol
 
Hivi CCM iko duniani miaka 25 kumbe? Kuanzia 1977 mpaka 1985 ilikuwa haipo au mnaficha kitu?

Nchi imejaa wagonjwa wa akili. Kazi kweli kweli.
 
Tumejaribu jamani, tupeni tena!!!! :israel::caked:


View attachment 14171

Yafuatayo ni baadhi ya yale ambayo CCM imefanya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita 2005 - 2010

2005 – 2010
TULIAHIDI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Ujenzi wa miradi 15 ya barabara kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa
Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010 huku ujenzi ambao
unaendelea ukiwa ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4

TULIAHIDI KUONGEZA BAJETI YA KILIMO NA KUKUZA SEKTA YA VIWANDA
Bajeti ya sekta ya kilimo imeongezeka kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005
hadi asilimia 7.9 mwaka 2010 huku ukuaji wa sekta ya viwanda ukiongezeka kutoka asilimia 8.4 mwaka
2005 hadi asilimia 9.9 mwaka 2008.
Idadi ya wakulima wanaopata mbolea ya ruzuku imeongezeka kutoka wakulima 750,000 mwaka 2005/2006 hadi 2,076,710 mwaka 2009/2010 huku bajeti ya ruzuku ya pembejeo ikiongezeka kutoka bilioni 7.5 hadi bilioni 101.4 katika kipindi hicho cha miaka mitano.
Idadi ya wataalamu wa ugani walioajiriwa katika halmashauri imeongezeka kutoka wataalamu 3,379 mwaka 2007/2008 hadi 4,439 mwaka 2009/2010.

TULIAHIDI KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU
Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini Tanzania waliongezeka kutoka 55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000mwaka 2009/2010.
Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo vikuu 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo 31 mwaka 2010.
Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kina wanafunzi 17,282
Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka 493,636 hadi 999,070 huku idadi ya wanafunzi wanaogharamiwa na serikali toka familia zenye kipato duni ikiongezeka toka 16,345 hadi 58,843. Ongezeko hili ni kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2009
Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 hadi wanafunzi 889,363.


TULIAHIDI KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA AFYA
Kutoka mwaka 2005 hadi 2009,jumla ya zahanati 464,vituo vya afya 98
na nyumba za waganga 394 zilijengwa.Zahanati 1,037,vituo vya afya 285 na hospitali 112 zimekarabatiwa.
Vifo vya watoto wachanga vimepungua hadi kufikia 58 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai mwaka 2009/2010.

TULIAHIDI KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA ZA MAJI
Huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa vijijini hapa nchini imeongezeka kutoka asilimia 58.7 mwaka 2005 hadi asilimia 60.1 mwaka 2009.
Fedha katika Mifuko ya maji zimeongezeka kutoka Sh bilioni 1.4 mwaka 2005 /2006 hadi bilioni 1.8 mwaka 2009/2010.

TULIAHIDI KUBORESHA MASUALA YA KIJINSIA
Nafasi za wanawake katika ngazi ya maamuzi zimeongezeka kutoka asilimia 26 mwaka 2005 hadi 31 mwaka 2010.
 
KWA KWELI CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza mema katika miaka 25. Ninarudia tena ku
waomba watanzania tumpe kura za ndio Mgombea wetu kipenzi cha watu Mhe. JAKAYA MRISHO
KIKWETE tarehe 31 Oktoba 2010.
 
Miaka 25 ya CCM. Mafanikio mengi yamepatikana katika sekta zote . Watanzania wenzangu mnafahamu hilo. Hivyo hatuna sababu ya kuchelewa tumpe kura za ndio DK Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 31 Oktoba 2010
 
ningependa kujua CCM wakipewa miaka mingapi zaidi itawatosha kufanya positive maajabu katika nchi hii?
 
Back
Top Bottom