Mafanikio ya haraka,naogopa.

Mafanikio ya haraka,naogopa.

Speaker

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
6,324
Reaction score
2,244
Leo,mwaka mmoja toka nimeanza kazi na kujitegemea.
Shukrani za pekee namrudishia mwenyezi Mungu,nikimuomba pia anisamehe kwa kufanya tofauti na vile ninavo sukumwa toka ndani yangu.

Shukrani ni kwa mafanikio niliyo yapata ndani ya mda huu mfupi.
Nikiwa mpangaji hapa mtaani,lakini miezi mi2 ijayo nikitegemea kuitwa "baba mwenye nyumba".

Nikiwa na usafiri mdogo wa kunifaa pia. Tatizo ni jinsi nilivo vipata vyote hivyo.

Sio kwa kujeruhi mtu au kwa kufanya mambo ambayo yange waacha wengine katika hali ya kuwa sikitisha. Ni ma-deal ambayo ni safi kwa hali ya kibinadamu,lakini yanayo endana kinyume na "imani yangu".

Nilipo anza kazi sikupenda nilicho kua nikikiona,nili jitahidi sana kupigana ili kuokoa hali iliyo kuwepo lakini utamu wa cash ulifanya nitangulize shida zangu na kusahau ninacho takiwa kusimamia.

Poor me, huu ni mwaka mmoja,natamani kubadilisha kazi. Lakini nitaenda wapi kwenye njaa? Hakuna anae penda shida lakini.

Ila ni nini hiki kinacho pingana na mimi?

Kila nikikumbuka msemo kua "mali ikija haraka,huondoka haraka pia" naogopa.
Maana nawafahamu walio kua na hela na sasa wako zero.

I am really afraid of my beginning.
 
kama waogopa kwanini unaendelea kufanya,,,,,hujutii bado maana ungejutia ungebadilika,haijalishi uko ofisi inayonuka kiasi gani cha msingi kukumbuka ni ktk msafara wa mamba kenge nao wamo,,,nikimaanisha kwamba kama system uliyoikuta ni "mamba" kwanini hukuendelea kuwa "kenge" yaani kuwa tofauti na nyayo zao,cha maana nahisi umekuja kutujulisha kwamba unamiliki nyumba,ka usafiri,na blah blah zingine.Kila la kheri mkuu
 
Ha ha ha...hebu weka bayana hizo shughuli uzifanyazo...
 
Imani kama haikuruhusu ni bora ujirudi mapema uliyoyafanya yanatosha tubu anza upya tena waweza kuendelea hapo hapo lakini ufanye kazi kwa nidhamu usiziruhusu tamaa zikutawale utaishia pabaya na kama unaona majaribu yanakushinda anza kusaka kazi mi naamini utafanikiwa tu kama unania njema
 
weka wazi aina ya kazi unayoifanya ili tukupe maujanja ya kuachana na hilo linalokutia mashaka...usiogope!
 
Pole.
Unatakiwa kuondoka hapo mapema, hayo ni machale yameanza kukucheza. Za mwizi siku hizi ni 36, hata kama haumdhuru mtu. Fraud is Fraud, hujawaza mwajiri akikukamata? Aibu yako kitaa?
 
Vijana wa siku hizi.......

The-surest-way-to-corrupt-a-youth-is-to-instruct-him-to-hold-in-higher-esteem-those-who-think-alike-than-those-who-think-differently.jpg
 
xema kaz yako hyo unazan utaxema you 're afraid kwa kaz ip hyo funguka ucje ukawa zee la cocaine
 
Bahati mbaya mwanadamu akishapoteza DHAMIRI anakuwa hana tofauti na vitu vingine. mkuu kabla haijapotea kama inavyoendelea kukushtaki, kimbia.

Mi mwenyewe kuna vihela nasimamia vya wafadhili lakini nikifikiria mtu huko ulaya ametoa hela yake kwa ajili ya watu wa Tanzania hata hawajui na hata hatokuja kuwaona. then leo hii mtu ujichukulie hizo sadaka za hawa watu ukale, kweli utabali salama? hata kama unajiona unamiliki vitu unadhani vitakuletea furaha?? hata hazingekuwa za msaada, Fikiria unachukua hela ya walipa kodi masikini wa Tanzania then unaaminiwa kusimamia kazi fulani tena ulioisomea miaka karibu ishirini then unajichukulia eti kisa uendelee, do you think utabaki salama????

Anyway, right thinking produce right answers and the contrary is also true. depending on which angle you are, its easier to defend your side and ignore the other.

''SIN IS ANY VIOLATION OF PURPOSE''
 
kama waogopa kwanini unaendelea kufanya,,,,,hujutii bado maana ungejutia ungebadilika,haijalishi uko ofisi inayonuka kiasi gani cha msingi kukumbuka ni ktk msafara wa mamba kenge nao wamo,,,nikimaanisha kwamba kama system uliyoikuta ni "mamba" kwanini hukuendelea kuwa "kenge" yaani kuwa tofauti na nyayo zao,cha maana nahisi umekuja kutujulisha kwamba unamiliki nyumba,ka usafiri,na blah blah zingine.Kila la kheri mkuu

Easier said than done.
 
Ndugu km unawasiwasi na yatayokukuta mbeleni..nakushauri ktk kazi unayofanya tafuta hela fungua biashara then achana na hiyo kazi inayokunyima raha na amani japo pesa yake ni tamu
 
Back
Top Bottom