Mafanikio ya haraka,naogopa.

Mafanikio ya haraka,naogopa.

Sijui itakuwaje kila mtu akianza kuelezea vitu anavyomiliki na njia alizotumia kupata!! nadhani ingekuwa aibu sana kwa weng!! Nashukuru mungu mm sijapata kama wewe na sijafikiria kupata kwa njia zisizo sahii na kumchukiza Mungu ila napenda sana kipato changu kinachonitosha kulipa kodi, kula, kuvaa na akiba bila kumtegemea mtu yoyote na kupata hela yoyote isiyo halali..........................

endelea hivo hivo,na usiache.
Ukionja dhambi hii hauta iacha.
 
We bwana kama kuna chance kula,hao wanaotoa blabla hawajapata hizo nafasi,serikali yenyewe ya ccm hii chukua chako mapema,cha kufanya jiwekee miradi mbalimbali ujijenge nje ya kazi.hata usipochukua wenzio watachukua.baba yangu mimi alikuwa mtiifu sana hili nalishuhudia kiasi kwamba hadi alitaka kuuwawa na waliokuwa wanaona anawazibia riski,leo hii kastaafu kiinua mgongo chenyewe anahangaika kupata.ukipata chance kulaaaa nakushangaa hofu ya nn?

Na hilo ndilo balaa.
ukiwa melini wale warusi ni either ukubaliane nao,au ipo siku utakosa nafasi ya kujuta.
 
Aibu.
Lakini nafanya kazi kwenye mazingira hatari mno,how do i repay myself?
Crude oil ina H2S ambayo ni hatari sana kwa maisha yangu. HFO ina Sulphur ambayo sio nzuri hata kidogo.

Hayo ni mazingira ninayo tembelea kila siku,kwa mshahara mbuzi.

Siibi,narudia siibi. ninacho fanya ni ile gain siioneshi tunauza na kugawana.

Ungefanyaje kama ni wewe? Upokee toka melini upate gain ya lita elf50,umwambie bosi wako
tumepata faida hiyo. auze apate zaidi ya mil75 afu AKULIPE 1M? Eti akili hiyo?

Kumbuka hiyo gain hailipii kodi anyway. Kipi bora,kumnufaisha bosi wako asiye mtanzania
na asiye lipa kodi au kujinufaisha wewe uliye mtanzania?

hapo sasa umeongea point, unaogopa nn ss? hivo si vitu vya kawaida tu kzn, ni utoto tu unakusumbua ukikua utaacha
 
Wala Lowasa sio fisadi,kuna mafisadi ambao hata huwezi wadhania.
Yeye basi tu upepo wa kisiasa ulimpitia.

wote ndio wale wale,mwizi wa kufoji sahihi za watu na mwizi wa kupiga watu kabali wote ni wezi
 
hapo sasa umeongea point, unaogopa nn ss? hivo si vitu vya kawaida tu kzn, ni utoto tu unakusumbua ukikua utaacha

Na fact ya utoto ndio ina niogofya zaidi.
 
...mkuuu speaker acha kunata na biti kwanza weka hoja vizuri,ujue watu hawajakuelewa bado...!
 
Huyu haibi...ni kutokana na nature ya kazi yake anayoifanya...

ni mwizi ingawa hatumii mtutu,yeye mwenyewe kasema anapata kwa njia zisizo sahihi,,,,,,,,,,,,it means anatengeneza madili ya uongo ili kujinufaisha yeye binafsi,kwangu mimi ni mwizi
 
Ha ha ha,atleast kwakua hatu fahamiani naweza kusema yes,mimi ni mwizi.
Lakini nioneshe mtu aliye ajiriwa na akafanya mambo makubwa kwa mshahara wake
nami nitakuita "muongo"
 
Leo,mwaka mmoja toka nimeanza kazi na kujitegemea.
Shukrani za pekee namrudishia mwenyezi Mungu,nikimuomba pia anisamehe kwa kufanya tofauti na vile ninavo sukumwa toka ndani yangu.

Shukrani ni kwa mafanikio niliyo yapata ndani ya mda huu mfupi.
Nikiwa mpangaji hapa mtaani,lakini miezi mi2 ijayo nikitegemea kuitwa "baba mwenye nyumba".

Nikiwa na usafiri mdogo wa kunifaa pia. Tatizo ni jinsi nilivo vipata vyote hivyo.

Sio kwa kujeruhi mtu au kwa kufanya mambo ambayo yange waacha wengine katika hali ya kuwa sikitisha. Ni ma-deal ambayo ni safi kwa hali ya kibinadamu,lakini yanayo endana kinyume na "imani yangu".

Nilipo anza kazi sikupenda nilicho kua nikikiona,nili jitahidi sana kupigana ili kuokoa hali iliyo kuwepo lakini utamu wa cash ulifanya nitangulize shida zangu na kusahau ninacho takiwa kusimamia.

Poor me, huu ni mwaka mmoja,natamani kubadilisha kazi. Lakini nitaenda wapi kwenye njaa? Hakuna anae penda shida lakini.

Ila ni nini hiki kinacho pingana na mimi?

Kila nikikumbuka msemo kua "mali ikija haraka,huondoka haraka pia" naogopa.
Maana nawafahamu walio kua na hela na sasa wako zero.

I am really afraid of my beginning.
pale penye giza; Dhambi ni tamu kweli lakini madhara/matokeo yake ndio machungu. Proverbs 16:8 Better a little with righteousness than much gain with injustice. kinachokuumiza kwa ndani ukienda zaidi ya hapo ndio kunakoitwa KUTUBU lakini ukimaanisha kuacha na kutokurudia tena.Mungu akusaidie ndugu yangu.
 
Ha ha ha,atleast kwakua hatu fahamiani naweza kusema yes,mimi ni mwizi.
Lakini nioneshe mtu aliye ajiriwa na akafanya mambo makubwa kwa mshahara wake
nami nitakuita "muongo"

ukipenda vya juu lazima uchape kazi za ziada zitakazokuingizia kipato na sio kutegemea mshahara wa laki mbili kwa mwezi,otherwise wizi utakuhusu au utakufa maskini,,,,,siwezi kukutajia watu kwa sababu nikikutajia hutawafahamu na sio public figure kwamba kila mtu atawajua. Inaonyesha umekuja hapa kutangaza hisa zako ili atakayevutiwa apate kununua na sio kuomba ushauri wa kukubadilisha maana akilini kwako umeshajiambia bila wizi huwezi kufanikiwa,All the best.
 
Siibi,narudia siibi. ninacho fanya ni ile gain siioneshi tunauza na kugawana.

Ungefanyaje kama ni wewe? Upokee toka melini upate gain ya lita elf50,umwambie bosi wako
tumepata faida hiyo. auze apate zaidi ya mil75 afu AKULIPE 1M? Eti akili hiyo?

Kumbuka hiyo gain hailipii kodi anyway. Kipi bora,kumnufaisha bosi wako asiye mtanzania
na asiye lipa kodi au kujinufaisha wewe uliye mtanzania?

Speaker endelea kula tu ndugu yangu, ila usiache kugawana na wazawa wenzako.

...daaah lizzy kwa kugundua fursa,uko vizuri sana ....

Hahaha. . .bado tu wakuitumia!!
 
Last edited by a moderator:
kama waogopa kwanini unaendelea kufanya,,,,,hujutii bado maana ungejutia ungebadilika,haijalishi uko ofisi inayonuka kiasi gani cha msingi kukumbuka ni ktk msafara wa mamba kenge nao wamo,,,nikimaanisha kwamba kama system uliyoikuta ni "mamba" kwanini hukuendelea kuwa "kenge" yaani kuwa tofauti na nyayo zao,cha maana nahisi umekuja kutujulisha kwamba unamiliki nyumba,ka usafiri,na blah blah zingine.Kila la kheri mkuu

My dia umeongea kitu cha msingi sana lakini unafikiri unaitaji a single day ili uwe kenge katikati ya mamba?unajua ni payment gani watu wanaukuwa kenge katika mamba wanapata ?ingawa nimegundua ukiwa mtu wa njia moja hutala nje.

Kusutwa na dhamira ni hatua kubwa sana na kuchua uamuzi ni second step.

Mtoa mada aashaanza hatua ya mwanzo na labda ndo maana amesema hapa ili aone mawazo ya walimwengu.

Speaker hicho unachokifanya named it any coloured name ni wizi its up for you to choose
 
Last edited by a moderator:
Lakini nafanya kazi kwenye mazingira hatari mno,how do i repay myself?
Crude oil ina H2S ambayo ni hatari sana kwa maisha yangu. HFO ina Sulphur ambayo sio nzuri hata kidogo.
Hayo ni mazingira ninayo tembelea kila siku,kwa mshahara mbuzi.

Hayo yote yanapaswa yawe covered na mwajiri kupitia occupational healthy and safety standards!!

Kama haiko hivyo ni kiasi cha kudai; hiyo ni halali yako kisheria.

Kutokuwepo kwa hizo standards si sababu ya wewe kuiba ama kufanya illegal deals!

Siibi,narudia siibi. ninacho fanya ni ile gain siioneshi tunauza na kugawana.

Huo ndio wizi wenyewe; wizi wa kutumia kalamu!

Ungefanyaje kama ni wewe? Upokee toka melini upate gain ya lita elf50,umwambie bosi wako
tumepata faida hiyo. auze apate zaidi ya mil75 afu AKULIPE 1M? Eti akili hiyo?

Hukujua yote hayo kabla hujakubali kazi? Hakufahamu mazingira ya kazi unayoiomba na malipo utakayopata?

Kumbuka hiyo gain hailipii kodi anyway. Kipi bora,kumnufaisha bosi wako asiye mtanzania
na asiye lipa kodi au kujinufaisha wewe uliye mtanzania?

Kama una nia njema na taifa lako na watu wake, hakikisha unapigania huyo bosi wako alipe kodi! Husikae kimya; kama upo kwenye nafasi ya kufahamu bosi alipi kodi, tumia nafasi hiyo kuleta msukumo wa bosi alipe kodi.
 
Leo,mwaka mmoja toka nimeanza kazi na kujitegemea.
Shukrani za pekee namrudishia mwenyezi Mungu,nikimuomba pia anisamehe kwa kufanya tofauti na vile ninavo sukumwa toka ndani yangu.

Shukrani ni kwa mafanikio niliyo yapata ndani ya mda huu mfupi.
Nikiwa mpangaji hapa mtaani,lakini miezi mi2 ijayo nikitegemea kuitwa "baba mwenye nyumba".

Nikiwa na usafiri mdogo wa kunifaa pia. Tatizo ni jinsi nilivo vipata vyote hivyo.

Sio kwa kujeruhi mtu au kwa kufanya mambo ambayo yange waacha wengine katika hali ya kuwa sikitisha. Ni ma-deal ambayo ni safi kwa hali ya kibinadamu,lakini yanayo endana kinyume na "imani yangu".

Nilipo anza kazi sikupenda nilicho kua nikikiona,nili jitahidi sana kupigana ili kuokoa hali iliyo kuwepo lakini utamu wa cash ulifanya nitangulize shida zangu na kusahau ninacho takiwa kusimamia.

Poor me, huu ni mwaka mmoja,natamani kubadilisha kazi. Lakini nitaenda wapi kwenye njaa? Hakuna anae penda shida lakini.

Ila ni nini hiki kinacho pingana na mimi?

Kila nikikumbuka msemo kua "mali ikija haraka,huondoka haraka pia" naogopa.
Maana nawafahamu walio kua na hela na sasa wako zero.

I am really afraid of my beginning.

wewe ni 'mwashi huru'?

angalia sana usije mtoa sadaka mamayo!!!!!

halafu ukaja tena hapa kwa jukwaa kusema hukuenda, ila tu utamu wa pesa!!!

damn!!!!
 
My dia umeongea kitu cha msingi sana lakini unafikiri unaitaji a single day ili uwe kenge katikati ya mamba?unajua ni payment gani watu wanaukuwa kenge katika mamba wanapata ?ingawa nimegundua ukiwa mtu wa njia moja hutala nje.

Kusutwa na dhamira ni hatua kubwa sana na kuchua uamuzi ni second step.

Mtoa mada aashaanza hatua ya mwanzo na labda ndo maana amesema hapa ili aone mawazo ya walimwengu.

Speaker hicho unachokifanya named it any coloured name ni wizi its up for you to choose

Asante Cynthia Chriss . Ushauri wako ni wa thamani sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom