Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Hiyo husababishwa na uvamizi yaan ukiona eneo flani limeendelea na jingine hapana wakati ni majirani ujue kuna sehem walivamia na pengine palipimwa na kuuzwa kama viwanja.
Yafuatayo in baadhi ya maeneo yaliyokaribu sana kijeografia ila yana hadhi tofauti kimaisha.

1. Sinza na Tandale
Mitaa hii ipo karibu sana ila hali ya maisha ya watu wake in tofauti kabisa. Tandale watu wengi wana maisha ya chini na uswahili pia.

2. Kawe na mikocheni
Kawe kuna uswazi ila jirani zao mikocheni kwa warioba wanakula upepo

3. Masaki na msasani
Hapa tajiri anakutana na maskini moja kwa moja. Ukimaliza tu masaki na kuanza msasani unaanza kuona ladha ya umasikini. Msasani kuna slum.

4. Mtongani na bahari beach/ununio.
Watu wa mtongani wana maisha ya chini sana shughuli yao ni uvuvi, kokoto na bodaboda ila jirani zao bahari beach ni maghorofa na mitaa iliyopangika vizuri na watu maarufu wako huko.

Hayo ni maeneo ambayo wenye nacho na pangu pakavu wanaishi pamoja kwa ukaribu
 
Dsm watu wengi wana maisha duni sana sana hawana kazi ni ubabaishaji tuu,hawana stock za vyakula hununua wanapotaka kula unga nusu,mafuta ya kula robo,fungu la dagaaa!!! Yani shida tupu !!! Ukikuta wana kunywa hizo supu zao za buku(1000) utacheka
Lakini wanajiona wajanjaaa!!!
Mikoani kuna maisha ya hadhi mara kumi ya dar
 
3. Masaki na msasani
Hapa tajiri anakutana na maskini moja kwa moja. Ukimaliza tu masaki na kuanza msasani unaanza kuona ladha ya umasikini. Msasani kuna slum.

Kweli pale Msasani katikati kabla ya kanisani kwenye lile bonde ni proper Slum, sijawahi ona sehemu yeyeto Dar iko hivi
Nilishapotea kwenye vichochoro nikajikuta nimeingia Chooni
na Maandazi road kule sio mchezo sijui bado upo huu mtaa, kwa wauza katerero, miaka ya 90s
 
Huko mbeleni nako yapo maeneo km hayoView attachment 1589645
IMG_20201004_065907.jpg
 
Kweli pale Msasani katikati kabla ya kanisani kwenye lile bonde ni proper Slum, sijawahi ona sehemu yeyeto Dar iko hivi
Nilishapotea kwenye vichochoro nikajikuta nimeingia Chooni
na Maandazi road kule sio mchezo sijui bado upo huu mtaa, kwa wauza katerero, miaka ya 90s
Mtaa upo ila katerero hakuna sasa hivi.
Katerero imebaki mwananyamala Hosp, sugar ray temeke, tegeta kibo, tabata 40/40, sinza bigbon sheli, conar bar, meeda orodha inaendelea.....
 
yes napajua huko.
Halafu kukaa mikocheni ni pagumu sana kwa watu wa maisha ya chini ni bora hata kuishi tandale.
Ubaya wa mikocheni hakuna huduma muhimu zile za mitaani kama migahawa na magenge.
Na usafiri pia ni shida kwa sababu pamejitenga
Wengi wanategemea daladala za kawe na na kutembea kwa mguu
 
Kwa mikumi syo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna mtaa wa idrisa mtaa mzima wmepanga wakina delicious

Ova
Hata ukiwa unakatiza magomeni. Sura nyingi za kiume zimekaa kaa kipisi pisi kali
 
Back
Top Bottom