Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Dsm watu wengi wana maisha duni sana sana hawana kazi ni ubabaishaji tuu,hawana stock za vyakula hununua wanapotaka kula unga nusu,mafuta ya kula robo,fungu la dagaaa!!! Yani shida tupu !!! Ukikuta wana kunywa hizo supu zao za buku(1000) utacheka
Lakini wanajiona wajanjaaa!!!
Hao watu wa keko mkuu, ila maeneo mengi DSM maisha mazuri
 
My deduction: binadamu tunategemeana, mwenye nacho anamtegemea asiye nacho ili apate labour. Hivyo tuishi kwa kuheshimiana. Nakumbuka Kuna uzi humu unaeleza asili ya majina ya maeneo, na hilo la Msasani(hali ya chini) lilitokana na wafanyakazi wa kimachinga waliokuwa wameajiriwa na mzungu Michael Chain(Mikocheni-hali bora) kushindwa kutamka jina la mnyampara wao Musa Hassan (Msasani)
Mikocheni imetokana na miti aina ya Mikoche,kama ilivyo mbuyuni,mtendeni,nk
 
Yafuatayo in baadhi ya maeneo yaliyokaribu sana kijeografia ila yana hadhi tofauti kimaisha.
1. Sinza na Tandale
Mitaa hii ipo karibu sana ila hali ya maisha ya watu wake in tofauti kabisa. Tandale watu wengi wana maisha ya chini na uswahili pia.
2. Kawe na mikocheni
Kawe kuna uswazi ila jirani zao mikocheni kwa warioba wanakula upepo
3. Masaki na msasani
Hapa tajiri anakutana na maskini moja kwa moja. Ukimaliza tu masaki na kuanza msasani unaanza kuona ladha ya umasikini. Msasani kuna slum.
4. Mtongani na bahari beach/ununio.
Watu wa mtongani wana maisha ya chini sana shughuli yao ni uvuvi, kokoto na bodaboda ila jirani zao bahari beach ni maghorofa na mitaa iliyopangika vizuri na watu maarufu wako huko.
Hayo ni maeneo ambayo wenye nacho na pangu pakavu wanaishi pamoja kwa ukaribu
Kumbe mtongani iko karibu na bahari beach eet wenzetu wa mbagala mtuambie ni kweli
 
Dsm watu wengi wana maisha duni sana sana hawana kazi ni ubabaishaji tuu,hawana stock za vyakula hununua wanapotaka kula unga nusu,mafuta ya kula robo,fungu la dagaaa!!! Yani shida tupu !!! Ukikuta wana kunywa hizo supu zao za buku(1000) utacheka
Lakini wanajiona wajanjaaa!!!
Kweli kiongozi,hata wanaoishi Nanjilinji maisha yao ni bora kuliko watu wengi wa Dsm.
 
Hlf videm vya pande hizo utavisikia "mi niko mbez beach" ...pmbaff kumbe wiz mtupu. Mwngine kasema yuko kinondon, kumbe yupo tandale kwa tumbo!
Hakuna anaependa umaskini, sawa na wabongo wakiwa nje ya nchi ukimuuliza Tanzania unaishi wapi kila MTU anasema DSM hakuna atakayesema Buhigwe au Simiyu
 
Back
Top Bottom