Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Davan

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
1,126
1,405
Yafuatayo in baadhi ya maeneo yaliyokaribu sana kijeografia ila yana hadhi tofauti kimaisha.

1. Sinza na Tandale
Mitaa hii ipo karibu sana ila hali ya maisha ya watu wake in tofauti kabisa. Tandale watu wengi wana maisha ya chini na uswahili pia.

2. Kawe na Mikocheni
Kawe kuna uswazi ila jirani zao mikocheni kwa warioba wanakula upepo

3. Masaki na Msasani
Hapa tajiri anakutana na maskini moja kwa moja. Ukimaliza tu masaki na kuanza msasani unaanza kuona ladha ya umasikini. Msasani kuna slum.

4. Mtongani na Bahari beach/Ununio
Watu wa mtongani wana maisha ya chini sana shughuli yao ni uvuvi, kokoto na bodaboda ila jirani zao bahari beach ni maghorofa na mitaa iliyopangika vizuri na watu maarufu wako huko.

Hayo ni maeneo ambayo wenye nacho na pangu pakavu wanaishi pamoja kwa ukaribu
 
My deduction: binadamu tunategemeana, mwenye nacho anamtegemea asiye nacho ili apate labour. Hivyo tuishi kwa kuheshimiana. Nakumbuka Kuna uzi humu unaeleza asili ya majina ya maeneo, na hilo la Msasani(hali ya chini) lilitokana na wafanyakazi wa kimachinga waliokuwa wameajiriwa na mzungu Michael Chain(Mikocheni-hali bora) kushindwa kutamka jina la mnyampara wao Musa Hassan (Msasani)
 
Hahaha!
 
Dsm watu wengi wana maisha duni sana sana hawana kazi ni ubabaishaji tuu,hawana stock za vyakula hununua wanapotaka kula unga nusu,mafuta ya kula robo,fungu la dagaaa!!! Yani shida tupu !!! Ukikuta wana kunywa hizo supu zao za buku(1000) utacheka
Lakini wanajiona wajanjaaa!!!
 
Hii ndio style ya maisha tuliyochagua. Tunanunua cha kula leo,kesho tutajua kesho.
 
Wakuja mna shida sana, watu mmewakuta na maisha yao mnawaona duni eti wahame au kuwauzia nyie! Kwanini nyinyi wa hali ya juu msiende kuanzisha makazi yenu ya watu wa juu?
Lakini zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa DSM ni wakuja kama wewe sio wa kuja wazazi wako yaweza kua ni wakuja, hata MO ni wakuja toka Singida
 
Back
Top Bottom