Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,237
- 9,871
aiseee.....labda mkuu ulipata sup nyingi.....
bongo bana....
mimi ndiye ninayewazidi mshahara...hadi naona aibu kuonyesha salary slip yangu..
aiseee.....labda mkuu ulipata sup nyingi.....
bongo bana....
Kumbe ni wewe wasalimie bagamoyo.Hoja zako hazina mshiko, nimesema madaktari walitakiwa tokea mwanzo waeleze tatizo lao ni maslahi siyo kila mara kugeuka kama vinyonga; walianza na interns na sasa maslahi bora. Pia wanashinikiza masuala yaliyo nje ya uwezo wao: KUMTAKA BLANDINA, DR. DEO NA DR. NKYA WATUMULIWE! hata siku moja serikali iliyopewa dhamana na watz kwa kura nyingi haiwezi kufuata matakwa ya kila kundi ndani ya jamii
MADAKTARI wametangaza rasmi kuanza mgomo katika hospitali zote za rufaa na vituo mbalimbali vya afya nchini kote hadi hapo madai yao yatakaposhughulikiwa na Serikali. Pia wamepitisha azimio la kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuifumua na kuiunda upya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao Waziri Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya kutokana na kile wanachodai kuwa ni kudhalilisha taaluma yao.
Dk Uliomboka pia aliwataja Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa kwamba wanapaswa kuwajibishwa na Rais. Akitangaza mgomo huo, Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Jumuiya ya Madaktari hao, Dk Stephene Ulimboka alisema hatua hiyo inalenga kupata ufumbuzi wa madai waliyotoa kwa muda mrefu na kuongeza kwamba, leo wanatarajia kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Dk Ulimboka alitaja baadhi ya madai yao kuwa ni kuwawekea mazingira bora ya kazi madaktari kwa kupeleka vifaa vya kazi hospitalini na kwenye vituo vya afya, kuboresha malipo ya posho na kuwapatia sitahili zote wanataalamu hao. Hata hivyo, tafauti na ilivyokuwa awali, kikao cha jana ambacho kilikuwa cha majumuisho, kilitumika pia kupokea ripoti ya mikutano iliyokuwa ikiongozwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na kupokea majukumu ya kuongoza harakati hizo.
Kuanzia leo tunatangaza kuwa madaktari wote wanaoguswa na hili kote nchini kuacha kufanya kazi hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yetu, tunataka Serikali iboreshe mazingira ya kutolea huduma za afya, ili kumwezesha daktari kumpatia huduma mgonjwa katika kiwango kinachostahili, alisema Dk Ulimboka.
Alitaja madai mengine matatu ambayo kamati anayoiongoza inasimamia kuhakikisha yanatekelezwa kuwa ni pamoja na madaktari kurejeshewa nyumba za kuishi kama inavyoelekezwa kwenye Standard order ya Serikali, ambayo inasema daktari atapatiwa nyumba ya kuishi na Serikali na kama sivyo atapatiwa asimilia 30 ya mshahara.
Alisema kipengele hicho kiliondolewa kinyemela bila wao kushirikisha wala kuelezwa sababu za kuondolewa kwake, jambo linalowaongezea ugumu wa maisha na kuwafanya wadharaulike. Madai mengine yalihusu nyongeza za mishahara, ambayo alisema kumekuwa na ugumu wa kutekeleza suala hilo kila mara hadi wanapofanya mgomo.
Mwaka 2005 wakati tunaanza kazi, mshahara wa daktari ulikuwa unafikia Sh124, 000, lakini baada ya mgomo ndipo ukapandishwa hadi kufikia karibu ya laki 700,000 sisi tunataka suala hili lirekebishwe na nyongeza yake isisubiri shinikizo, alisema.
Madai mengine ni malipo kwa madaktari pindi wanapofanya kazi katika mazingira hatarishi na kupendekeza walipwe asimilia 30 ya mshahara wao, posho wakati wa kazi ya ziada ambayo kwa sasa wanalipwa asimilia 10 ya mshahara wao. Kuhusu mshahara, alisema yapo mapendekezo ambayo alisema wataitaarifu Serikali watakapokutana na viongozi wake.Madaktari hao leo wanatarajia kuendelea na mkutano wao katika ukumbi wa Don Bosco.
Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi alisema alikabidhi majukumu kwa kamati iliyoundwa na wanachama baada ya kuonekana kuwa hadi sasa Serikali imekuwa ikiwazungusha. Wanachama wamesema hapo mlipofikia tunashukuru mmejitahidi vya kutosha na sasa tunaomba mtukabidhi majukumu ili shughuli hii iweze kusimamiwa na kamati ya madaktari, alisema Dk Mkopi.
Hatua hiyo imelenga kuongeza wigo wa washiriki ambao watawahusisha madaktari wasio wanachama wa MAT na wafanyakazi wengine katika sekta hiyo ya afya.
Mwananchi
Huyu Blandina Nyoni sijui yukoje, na pengine najiuliza kwa nini wanawake wakishika madaraka ya juu huwa na kiburi sana?
Yaani hawa madaktari nawafagilia kwa msimamo wao. Ila wakilegeza huo msimamo wao huo watakuwa ndio the last cadre kujidhalilisha beyond imaginable boundaries. Msiwe kama walimu ambao kila uchao hawajui destiny yao,onyesheni kuwa mnamaanisha mnachokiongea na kukidai.
Hoja zako hazina mshiko, nimesema madaktari walitakiwa tokea mwanzo waeleze tatizo lao ni maslahi siyo kila mara kugeuka kama vinyonga; walianza na interns na sasa maslahi bora. Pia wanashinikiza masuala yaliyo nje ya uwezo wao: KUMTAKA BLANDINA, DR. DEO NA DR. NKYA WATUMULIWE! hata siku moja serikali iliyopewa dhamana na watz kwa kura nyingi haiwezi kufuata matakwa ya kila kundi ndani ya jamii
Bado siamini kama masrahi ya madaktari wanayolipwa sasa hayatoshi,mimi naamni madaktari mmesahau kuwa kazi yenu siyo kazi pekee hapa tanzania na kwamba hakuna serikali ambayo itawabagua watumishi wake.
Mmekiri wenyewe kwamba mwaka 2005 mlikuwa mnaloipwa 124,000 leo mnalipwa 700,000 kwanza nampongeza jk na nawataka mfahamu kuwa kuomba nyongeza kwa kujilinganisha na wanasiasa ni ujinga, kama mnataka posho za siasa nendeni mkagombee, dunia nzima posho za wanasiasa ziko juu na watumishi wanalipwa kwa scales zao kulingana na policy.
Jamani naomba niulize huyu Blandina nyoni kasomea hii professional ya udaktari? au kapewa kama katabia kao hawa jamaa.
Hakuna mgomaji hapo,tishia nyau tu.
Mbona nimepita rufaa mbeya na nimepewa huduma au mgomo ni
kwa baadhi ya siku tu?