Maendeleo ya Mgomo wa Madaktari na Mwitikio wa Serikali

sio kwamba wanashindwa au wanaficha kusema ukweli au kuwasikiliza doctaz kwa kutaka jf members...bali wanatunza kazi zao na watoto wao wapate hata kuimaliza elimu ya msingi.......
 
attachment.php

Madaktari wakiendelea na mkutano wao, siku ya tatu ya Mgomo, Star Light Hotel jana.
 
wananchi masikini wa kutupa wanaadhibiwa kwa makosa ya viongozi wao...hao viongozi wana watoto wao, wala hawatibiwi kwenye hizi hospitali zenye manesi wenye matusi.....hospitali za serikali....wanaotibiwa hapo wote ni masikini. mshahara wanaopewa madaktari tz unatosha wao pia kujitajirisha na kujenga mahotel kama mnavyosema....daktari gani haibi madawa kupeleka kwenye famacy yake?...mshahara mnapata mkubwa, madawa mnaiba kupeleka kweney maduka ya madawa na dispensary zenu, bado mnatugomea watu wetu wanakufa...upumbavuuu wa ajabu huu....naiomba serikali ichukua uamuzi mgumu juu ya hili kwa viongozi wa mgomo huu....ukitaka kupata uchungu juu ya hili tembelea hospitali kesho...masikini wa tz wanaadhibiwa kwa makosa ya viongozi wao? kisa mshahara? hamna maadili nyieee...

Hili ni fundisho kwa walalahoi wanaopewa ubwabwa na tshirt na kofia kuwachagua magamba. Next time watajifunza kuwa magamba ni janga la kidunia.
 
this picture sums it up for me, serikali isichoelewa aiwezi tibu wagonjwa bila ya expertise. Ni upumbavu wa hali ya juu kuweka kiburi kisicho na maana, but then what do you expect from people who do not use this sector of public services. Inachukua muda kumtengeneza doctor kuliko Mkullo na inasikitisha sana kuona mishahara ya wafanyakazi ya umma isivyolingana na umuhimu wa kijamii.

Hila madokta inabidi wafikirie in moral terms kuliko financial isn't ethical part of their training maana hawa wahalifu hiko siku yao tu.
 
1. Umuhimu na thamani ya taaluma fulani wanaijua vizuri wenyewe wahusika
2. Kuendelea kuwa Daktari, si lazima kuwe na wagonjwa, ndyo maana kitu cha kwanza wanachosomea ni kuzuia magonjwa
3. Mshahara wa Madaktari unaonekana mkubwa unapolinganishwa na watumishi wengine, hii si sahihi, mshahara wa watumishi wa kada zingine si benchmark ya kupanga maslahi ya madaktari, kila kada ipiganie kivyake, kama wanalivyofanya wabunge.
4. Huduma za tiba zinaendelea kutolewa na waganga wa jadi/sangomas, ambao wana leseni halali za ku-practice "altenative medicine" na ni wengi kuliko wa hospitalini, na kila mwaka kuna >5,000 graduates, pia wakemeaji mapepo (Lusekelo a.k.a Transfoma et al) wanaendela kutoa huduma, kusipokuwa na mgomo wagonjwa wengi >60% wanatibiwa huko, sasa malalamiko ya nini? wao hawagomi kwa kuwa mnawapelekea hela nyingi sana bila kulalamika!, ila madaktari wakidai haki zao wanaonekana wabaya, aaaagh!
Baelezeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
haya ni sehemu ya madai ya madaktari.madaktari wanajaribu kuwatetea wananchi dhidi ya huduma mbovu.

tafakari na tuache propaganda

asante mkuu kwa kumpa hiyo.kuna watu wanaangalia kuhusu madai ya mshahara tu. Lengo ni kuboresha huduma za afya zitolewe kwa viwango vitakavyofanya wagonjwa watibiwe kwa uhakika! Katibu mkuu analipwa m 12 kila mwezi,nyumba bure,anabadilisha shangingi kila mwaka,bado alowance zingine za vikao huku mawodi na vitanda hospitalini havitoshi, mara nyingi wanafanya ununuzi wa vifaa vibovu usiozingatia sheria ambavyo hata havitatumika. Kuna mashine ilinunuliwa moi kwa gharama kubwa tu ya kodi za watanzania,ikagundulika kuwa haifanyi kazi wakaiweka pembeni na kuanza mchakato wa kununua nyingine. Mnh miezi miwili imepita hakuna solutions kwa ajili ya vipimo,continuation form zimegeuzwa ndo prescription form,tutafika? Hata ukinilipa vizuri kama wagonjwa wananifia kila siku siwezi kuishi kwa amani. Psychological trauma ninayoipata ni mbaya sana. Kumbuka hii serikali ya washkaji kila mtu amewekwa ili avune kila kilichopo ndo maana kwenye bajeti zao other charges zinakuwa kubwa kuliko vitu vingine. Unataka kuniambia matumizi ya vitu visivyofahamika ni makubwa kuliko vinavyofahamika?
 
this picture sums it up for me, serikali isichoelewa aiwezi tibu wagonjwa bila ya expertise. Ni upumbavu wa hali ya juu kuweka kiburi kisicho na maana, but then what do you expect from people who do not use this sector of public services. Inachukua muda kumtengeneza doctor kuliko Mkullo na inasikitisha sana kuona mishahara ya wafanyakazi ya umma isivyolingana na umuhimu wa kijamii.

Hila madokta inabidi wafikirie in moral terms kuliko financial isn't ethical part of their training maana hawa wahalifu hiko siku yao tu.

kusema ukweli, hawa wapumbavuu ipo siku yao...wagonjwa wengi wanakufa bure, si maadili kwa dr kufanya wanachofanya...
 
kusema ukweli, hawa wapumbavuu ipo siku yao...wagonjwa wengi wanakufa bure, si maadili kwa dr kufanya wanachofanya...
maadili ni kusherehekea miaka 50 ya uhuru kwa mabilioni ya sh. Huku hospitali zikikosa dawa.shame!!
 
jana waziri ghasia alizungumza nao pale starlight' akasema interns wote wa muhimbili wamerudishwa muhimbili wakaripoti j3..madaktari waliwasilisha taarifa yenye hoja na madai yao kwa ghasia ampe waziri mkuu.

Bado ni tatizo zito sana, serikali inaelekea kushindwa kulihandle kwa umakini na seriousness....SO MGOMO WA MADAKTARI UNAENDELEA!

Kikao chao kinaendelea tena leo pale starlight, na hadi sa hivi kuna taarifa kuwa kamati waliyounda imeanza kupokea vitisho kutoka kwa viongozi wa serikali, ikiwamo ofisi ya PM inasemekana WAMEWAAMURU WAMALIZE MGOMO kabla ya j3, na pia mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tanga nae amempigia simu mwenyekiti wa kamati nakum'command kuhakikisha mgomo huo unaisha haraka iwezekanavyo! narudia tena kum'command!

video ya mkutano unaoendelea leo hii hapa Bambuser | Mkutano wa wafanyakazi wa afya tz, starlight | gtlicous, pia kwenye hii web zipo video nyingine.
 
kusema ukweli, hawa wapumbavuu ipo siku yao...wagonjwa wengi wanakufa bure, si maadili kwa dr kufanya wanachofanya...

ungekuwa na akili ungesoma medicine ili ujitotolee kuhudumia wagonjwa. Hata hivyo hujachelewa unaweza kutoa msaada wa dawa na vifaa mbali mbali,tutarudi kazini. Kwani unadhani hayo madai hayakuwepo? Why now? Hali hospitali ni no longer torelable. We can not work any more bila hospitali kuboreshwa.
 
mkuu hiyo ndiyo hoja. Wakubwa wakienda muhimbili wakiwa wanaumwa malaria wanapewa referral kwenda India na haohao madaktari. Watanzania masikini ndio wanatibiwa hapo na leo hii ndio wanakufa kwa sababu ya mgomo wa madaktari! Jambo la kutia huruma na kusikitisha wanyonge ndio wanapewa adhabu wakati wakosaji ni wakubwa. Waoneeni huruma masikini hawa ambao wamekamuliwa hadi damu ili ninyi msome. Fanyeni ubinadamu.
Legho ni kulazimisha umma uilazimishe serikali iingie kwenye mazungumzo na madaktari na kutatua mgogoro huu. Ni sekta moja iliyogoma, walishawahi kugoma waendesha daladala serikali ikasikiliza madai yao, wakati lesini mpya za class c zilipoisha watu walipokosa usafiri serikali iliingilia haraka kutatua tatizo watu wengine wasafiri, mafuriko dar watu wamepata viwanja haraka licha ya wengine kuwa na maombi zaidi ya miaka 10 ya kupimiwa viwanja. ni namna ya sekta moja kuwakilisha madai yake. Jinsi jamii inavyopata maumivu tunatofautiana. Cha msingi mazungumzo ndio njia pekee ya kutatua tatizo hilo vitisho sidhani km vitasaidia ukizingatia ugumu wa kumfundisha daktari mmoja
 
wivu gani wewe punga bwabwa?.....hivi nani amwonee wivu daktari? akili zake kama ni za kugoma huku akishuhudia wananchi wanakufa, mtu wa aina hiyo si hana maana tu?..kwanza madaktari wenyewe hawana akili kudeserve mshahara mkubwa? kwasababu ni walevi na hawana maadili...mbona mnashindwa kutibu watu na kuwaambia waende india? mlikuwa mnasoma vitabu tofauti na ville vya madaktari wa india?..hopless teethless dogsss.
Sio kweli, kwenda nje ni kwa sababu hapa hakuna vifaa, lakini wana ujuzi tu ukishakuwa na vifaa utaweza kufanya operation complex na baada ya muda utapata uzoefu. Hapa ni hospitali ngapi zina CT Scan na zinaitwa za rufaa? Ngapi zina MRI machine? hivyo ni vipimo vidogo tu, ktk fani ya udaktari.
 
Gomeni tu ma Dr kwa kipindi hiki tutaenda hata kwa Babu Loliondo kupata dawa ya kutuliza maumivu mnayodai ni ya msingi sana..chonde chonde msiwatupe kina mama wajawazito na watoto..pia wale walio kwenye hali mbaya
 
Picha huzungumza zaidi ya maneno millioni.. Ukiitazama picha hii vizuri utagundua kwamba hakuna nafuu kwa mwananchi..
 
nimejiuliza sana hili swali, mfano baba unafanya kazi, mshahara wako si mkubwa na bajeti yako ndani ya nyumba ni ndogo ya kujinyima...wanatokea watoto wengine ndani yanyumba wanamwambia baba sisi ni wa muhimu kuliko watoto wako wengine, tunataka ugali mkubwa zaidi, au tunataka tupewe share kubwa zaidi toka kwenye mshahara wako baba...

Tanzania ni nchi ambayo kila mwaka bajeti inayumba

Umedai,madaktari ni hopeless,lakini nadhani sifa hiyo inakufaa wewe.Nani kasema wao ni muhimu zaidi kuliko wengine?Wao wanadai iliyohaki yao na kwa kadiri ya mikataba yao(nyumba na mazingira bora ya kazi).
Mtu yeyote asipopata anachostahili anatakiwa kudai kama anajua haki yake.Ni serikali inayosababisha watu kufa kwa kutowatimizia madai yao hao madaktari.Nani kakuambia serikali haina fedha?Tatizo lake ni namna ya kupanga vipaumbele na hapa sina haja ya kutoa mifano.
Pole,kama watu kudai haki yao wewe inakukera na wala sidhani kama watazingatia mawazo yenu ya kuabudu unyonge na ukondoo usio na tija.
 
Back
Top Bottom