Maendeleo ya Mgomo wa Madaktari na Mwitikio wa Serikali

MADAKTARI wametangaza rasmi kuanza mgomo katika hospitali zote za rufaa na vituo mbalimbali vya afya nchini kote hadi hapo madai yao yatakaposhughulikiwa na Serikali. Pia wamepitisha azimio la kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuifumua na kuiunda upya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao Waziri Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya kutokana na kile wanachodai kuwa ni kudhalilisha taaluma yao.

Dk Uliomboka pia aliwataja Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa kwamba wanapaswa kuwajibishwa na Rais. Akitangaza mgomo huo, Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Jumuiya ya Madaktari hao, Dk Stephene Ulimboka alisema hatua hiyo inalenga kupata ufumbuzi wa madai waliyotoa kwa muda mrefu na kuongeza kwamba, leo wanatarajia kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


Dk Ulimboka alitaja baadhi ya madai yao kuwa ni kuwawekea mazingira bora ya kazi madaktari kwa kupeleka vifaa vya kazi hospitalini na kwenye vituo vya afya, kuboresha malipo ya posho na kuwapatia sitahili zote wanataalamu hao. Hata hivyo, tafauti na ilivyokuwa awali, kikao cha jana ambacho kilikuwa cha majumuisho, kilitumika pia kupokea ripoti ya mikutano iliyokuwa ikiongozwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na kupokea majukumu ya kuongoza harakati hizo.


"Kuanzia leo tunatangaza kuwa madaktari wote wanaoguswa na hili kote nchini kuacha kufanya kazi hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yetu, tunataka Serikali iboreshe mazingira ya kutolea huduma za afya, ili kumwezesha daktari kumpatia huduma mgonjwa katika kiwango kinachostahili," alisema Dk Ulimboka.

Alitaja madai mengine matatu ambayo kamati anayoiongoza inasimamia kuhakikisha yanatekelezwa kuwa ni pamoja na madaktari kurejeshewa nyumba za kuishi kama inavyoelekezwa kwenye ‘Standard order' ya Serikali, ambayo inasema daktari atapatiwa nyumba ya kuishi na Serikali na kama sivyo atapatiwa asimilia 30 ya mshahara.

Alisema kipengele hicho kiliondolewa kinyemela bila wao kushirikisha wala kuelezwa sababu za kuondolewa kwake, jambo linalowaongezea ugumu wa maisha na kuwafanya wadharaulike. Madai mengine yalihusu nyongeza za mishahara, ambayo alisema kumekuwa na ugumu wa kutekeleza suala hilo kila mara hadi wanapofanya mgomo.

"Mwaka 2005 wakati tunaanza kazi, mshahara wa daktari ulikuwa unafikia Sh124, 000, lakini baada ya mgomo ndipo ukapandishwa hadi kufikia karibu ya laki 700,000 sisi tunataka suala hili lirekebishwe na nyongeza yake isisubiri shinikizo," alisema.

Madai mengine ni malipo kwa madaktari pindi wanapofanya kazi katika mazingira hatarishi na kupendekeza walipwe asimilia 30 ya mshahara wao, posho wakati wa kazi ya ziada ambayo kwa sasa wanalipwa asimilia 10 ya mshahara wao. Kuhusu mshahara, alisema yapo mapendekezo ambayo alisema wataitaarifu Serikali watakapokutana na viongozi wake.Madaktari hao leo wanatarajia kuendelea na mkutano wao katika ukumbi wa Don Bosco.

Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi alisema alikabidhi majukumu kwa kamati iliyoundwa na wanachama baada ya kuonekana kuwa hadi sasa Serikali imekuwa ikiwazungusha. "Wanachama wamesema hapo mlipofikia tunashukuru mmejitahidi vya kutosha na sasa tunaomba mtukabidhi majukumu ili shughuli hii iweze kusimamiwa na kamati ya madaktari," alisema Dk Mkopi.

Hatua hiyo imelenga kuongeza wigo wa washiriki ambao watawahusisha madaktari wasio wanachama wa MAT na wafanyakazi wengine katika sekta hiyo ya afya.

Mwananchi

 
Jamani naomba niulize huyu Blandina nyoni kasomea hii professional ya udaktari? au kapewa kama katabia kao hawa jamaa.
 
Tunawatakia mgomo mwema na uwe mgomo kweli nasisi walala hoi tutakwenda kwa babu Samunge kwa kipindi hiki,japo nako mhh!
 
Hivi hili la kutaka wizara and viongozi wake wabadilishwe pengine sio strategy nzuri sana maana kwa namna fulani inakuwa rahisi sana kwa serikali kukwepa na kusema ni madai ya kisiasa/au the whole issue ina harufu ya "siasa"! au pengine ni long term sio kitu wanachoweza kupewa fumba na kufumbua.

Wangeanza zaidi na suala la maslahi yao (ingawa najua kuna mwingiliano na viongozi na structure ya wizara) kama mishahara, posho na mazingira ya kazi halafu hilo la wizara likaja baadae.

Well, ngoja tuangalie usikivu au ubabe wa serikali sasa!
 
Mbona kuna gari yenye namba hizi NW,AF inazunguka hapa jijini Mwanza tangu jana, siyo Lucy Nkya huyo kweli?Nilikutana nalo pale mtaa wa misheni leo mida ya saa mbili likielekea kama AIRPORT nikapiga chabo kwa mbali nikaona kuna mwana mama kushoto kwa dereva kasinzia,sasa kama ndiye kazi ipo
 
kweli ziumiazo ni nyasi, wenyewe wanakwenda kuangalia afya tu London, matibabu india
 
Huyu Blandina Nyoni sijui yukoje, na pengine najiuliza kwa nini wanawake wakishika madaraka ya juu huwa na kiburi sana?

Siyo huyu tu hata mkurugenzi wa Muhimbili ambaye aliwarudisha madaktari hawa wizarani!
 
Jamani naomba niulize huyu Blandina nyoni kasomea hii professional ya udaktari? au kapewa kama katabia kao hawa jamaa.
Sio lazima, Katibu ni mtendaji zaidi sana sana awe anajua mambo ya fedha au mipango
 
Back
Top Bottom