Maendeleo ya Mgomo wa Madaktari na Mwitikio wa Serikali

Hivi bila ya mgomo wagonjwa walikuwa hawaathiriki na huduma mbovu au maisha duni ya madaktari? Hivi wagonjwa wanakuwaje salama au nafuu wakati madaktari wana manung'uniko na malalamiko ya msingi? Nawaunga mkono kwani salama yao ni salama ya wagonjwa. Tukitaka huduma nzuri toka mahospitali yetu tupiganie maslahi yao.
 
Bado siamini kama masrahi ya madaktari wanayolipwa sasa hayatoshi,mimi naamni madaktari mmesahau kuwa kazi yenu siyo kazi pekee hapa tanzania na kwamba hakuna serikali ambayo itawabagua watumishi wake.

Mmekiri wenyewe kwamba mwaka 2005 mlikuwa mnaloipwa 124,000 leo mnalipwa 700,000 kwanza nampongeza jk na nawataka mfahamu kuwa kuomba nyongeza kwa kujilinganisha na wanasiasa ni ujinga,kama mnataka posho za siasa nendeni mkagombee,dunia nzima posho za wanasiasa ziko juu na watumishi wanalipwa kwa scales zao kulingana na policy.

Kweli we ni mwanasiasa.!!! Nenda kaangalie rais wa Marekani analipwa shillingi ngapi na daktari wa marekani analipwaje na ndo utajua tofauti ya nchi yenye akili na ki ngo fulani kinaitwa serikali ya Tanzania. Nchi yenye akili inawekeza kwenye afya, kilimo, sayansi na teknologia.

Kwao siasa ni kwa ajili ya kuboresha vitu vya msingi Kiserikali chako kinafanya kinyume, kinawekeza kwenye siasa na maslahi ya wanasiasa tu. Tuliobaki ni wagonjwa tupu. Na wewe ni mgonjwa sana tena ugonnjwa wako ni ugonjwa wa akili. Sasa laki 7 kwa mwezi ndio maslahi gani hayo kwa daktari?

Mbunge pekee posho yake ya wiki moja ni milioni 1.5 bado mkuu wa mkoa, katibu wa wizara, naibu waziri, waziri.....list ya wanasiasa haiishii hapo. Ndo maana nasema watu kama wewe wasioona mambo ya msingi mlipaswa kuzaliwa Somalia au Yemen.

Au msiumbwe kabisa. Maana uwepo wenu hapa Tanzania unatusababishia umaskini wa kupindukia.
 
Hospitali za Amana, Mwananyamala na Temeke pamoja na Muhimbili huduma zinatolewa kama kawaida

Huduma zinatolewa...lakini si kama kawaida. katika kila kitengo kwatika hospitali hizo wameachwa madaktari wachache kuhudumia wagonjwa wa dharura (emergency)...clinic zote leo zimefungwa Temeke, Amana, Ilala, na Muhimbili ( pamoja na MOI na Ocean Road). Kwa kifupi mgomo umeanza japo taratibu lakini mpaka kesho huduma nyingi zitakuwa zimefreeze.

Kama unadhani utani nenda sasa hivi pale Don Bosco uone kuna madaktari wangapi wapo pale kwa mkutano tangu asubuhi, na huko mikoani leo jioni hii wanaitisha vikao, tayari Bugando, Mount Meru, Mbeya Referral na Mbeya Regional wameshaconfirm kufanya vikao jioni hii kujiunga na mgomo...hali itakuwa mbaya siku chache zijazo.
 
View attachment 46033
CDM bwana ni wachochea vurugu nchini,
1. Walianza kutoka bungeni wakati rais akiwepo
2. Maandamano Arusha
3. Kususia vikao vya bunge juu ya mswada wa katiba
4. Kuwaunga mkono TUCTA na Mgaya
5. Kuwaunga mkono CWT na Mkoba
6. Kuunga wa interns Muhimbili,
7. Leo wapo na madaktari

Itapobidi tutaitisha maandamano nchi nzima kuwalaini CDM na MAT kwa kukosesha huduma ya afya wananchi wa TZ

Wewe sio makosa yako, njaa ikizidi mtu hafikiri, na wengine huenda mbali zaidi kwa kusema usifanye makubaliano na mtu mwenye njaa .

Njaa zako ndio zimekufanya uwe na mfadhaiko wa ubungo hasa CCm inapo tajwa, na kuomba usiombe samaki omba ndoano.

Maisha bora si ndio hayo madktari wanyoyahitaji sawa sawa na kauli mbiu ya CCM, basi naweza sema Migomo inayoendelea nchini inachochochewa na kauli mbiu ya CCM maisha bora kwa kila mtanzania.
 
hebu wekeni facts basi, tusiwe tunapiga gumzo la sokoni, we need facts here, so that, information can reliable.
 
Muda si mrefu utasikia Chadema wanahusika na hii movement! CCM bana!
Ngoja tutaona kweli wee ngoja.....
Hawa madaktari walikuwa na ajenda ya siri tangu mwanzoni walitafuta pa kutokea; walianza na kuwatetea interns, sasa wamekuja na madai mapya!! Kulikoni ?? Ama wanataka wakpate muda mwingi wa kuchota pesa za wananchi kwa kutumia hospitali zao binafsi kwa kisingizio cha mgomo. Ndipo suala la KUKOSA uzalendo linaibuka.
kweli nimeamini watu tupo tofauti....
 
Kuna post nyingi sana zimenyofolewa kwenye hii thread na kuacha kauli nyepesi zikielea... au basi thread zimeunganishwa na sasa hakuna hata flow; in the morning i saw very useful insight za madaktari, lakini sasa amejaa mafiflili tu sijui lengo hasa ni nini
Kuna muda jamii forum ili stuck au jamaa wamei hack
 
Hi lawama zinazoelekezwa Wizara ya Afya kama wampewe pesa kidogo na hazina wao wafanyeje? Sema lile la Wabunge na posho zao za kukaa za 200,000 kwa siku litaamsha hata mabubu
 
MADAKTARI wametangaza rasmi kuanza mgomo katika hospitali zote za rufaa na vituo mbalimbali vya afya nchini kote hadi hapo madai yao yatakaposhughulikiwa na Serikali. Pia wamepitisha azimio la kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuifumua na kuiunda upya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao Waziri Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya kutokana na kile wanachodai kuwa ni kudhalilisha taaluma yao.

Dk Uliomboka pia aliwataja Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa kwamba wanapaswa kuwajibishwa na Rais. Akitangaza mgomo huo, Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Jumuiya ya Madaktari hao, Dk Stephene Ulimboka alisema hatua hiyo inalenga kupata ufumbuzi wa madai waliyotoa kwa muda mrefu na kuongeza kwamba, leo wanatarajia kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


Dk Ulimboka alitaja baadhi ya madai yao kuwa ni kuwawekea mazingira bora ya kazi madaktari kwa kupeleka vifaa vya kazi hospitalini na kwenye vituo vya afya, kuboresha malipo ya posho na kuwapatia sitahili zote wanataalamu hao. Hata hivyo, tafauti na ilivyokuwa awali, kikao cha jana ambacho kilikuwa cha majumuisho, kilitumika pia kupokea ripoti ya mikutano iliyokuwa ikiongozwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na kupokea majukumu ya kuongoza harakati hizo.


"Kuanzia leo tunatangaza kuwa madaktari wote wanaoguswa na hili kote nchini kuacha kufanya kazi hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yetu, tunataka Serikali iboreshe mazingira ya kutolea huduma za afya, ili kumwezesha daktari kumpatia huduma mgonjwa katika kiwango kinachostahili," alisema Dk Ulimboka.

Alitaja madai mengine matatu ambayo kamati anayoiongoza inasimamia kuhakikisha yanatekelezwa kuwa ni pamoja na madaktari kurejeshewa nyumba za kuishi kama inavyoelekezwa kwenye ‘Standard order' ya Serikali, ambayo inasema daktari atapatiwa nyumba ya kuishi na Serikali na kama sivyo atapatiwa asimilia 30 ya mshahara.

Alisema kipengele hicho kiliondolewa kinyemela bila wao kushirikisha wala kuelezwa sababu za kuondolewa kwake, jambo linalowaongezea ugumu wa maisha na kuwafanya wadharaulike. Madai mengine yalihusu nyongeza za mishahara, ambayo alisema kumekuwa na ugumu wa kutekeleza suala hilo kila mara hadi wanapofanya mgomo.

"Mwaka 2005 wakati tunaanza kazi, mshahara wa daktari ulikuwa unafikia Sh124, 000, lakini baada ya mgomo ndipo ukapandishwa hadi kufikia karibu ya laki 700,000 sisi tunataka suala hili lirekebishwe na nyongeza yake isisubiri shinikizo," alisema.

Madai mengine ni malipo kwa madaktari pindi wanapofanya kazi katika mazingira hatarishi na kupendekeza walipwe asimilia 30 ya mshahara wao, posho wakati wa kazi ya ziada ambayo kwa sasa wanalipwa asimilia 10 ya mshahara wao. Kuhusu mshahara, alisema yapo mapendekezo ambayo alisema wataitaarifu Serikali watakapokutana na viongozi wake.Madaktari hao leo wanatarajia kuendelea na mkutano wao katika ukumbi wa Don Bosco.

Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi alisema alikabidhi majukumu kwa kamati iliyoundwa na wanachama baada ya kuonekana kuwa hadi sasa Serikali imekuwa ikiwazungusha. "Wanachama wamesema hapo mlipofikia tunashukuru mmejitahidi vya kutosha na sasa tunaomba mtukabidhi majukumu ili shughuli hii iweze kusimamiwa na kamati ya madaktari," alisema Dk Mkopi.

Hatua hiyo imelenga kuongeza wigo wa washiriki ambao watawahusisha madaktari wasio wanachama wa MAT na wafanyakazi wengine katika sekta hiyo ya afya.

Mwananchi

JK akishindwa kuwawajibisha hao anaoshauriwa MGOMO ukaofuata uwe wa kumtaka AJIUZULU kwa kushindwa kuongoza na kusababisha vifo makusudi!!
 
Wao wapeleke watoto wao kusoma majuu, wa madktari ndo
waende shule za msondo ngoma! kama serikali inamwaga
mboga acha madaktari wamwage ugali tena wasiumwage tu
wautie na mafuta ya taa kabisa wasije wakauokota wakaula bure.

Nimependa sana hii!
 
MOD naomba msaada huyu mtu atatutafutia ban bure kabisa??? hivi anajua ratio ya daktari kwa mgonjwa tanzania ikoje??? mimi nakuambia ya nurse kwa mgonjwa ni 1:1570 ikiwa WHO wanasema ration inatakiwa iwe 1:6 sasa unasema nini hapo.

Wewe huna akili kama wanaomshauri JK

Hoja zako hazina mshiko, nimesema madaktari walitakiwa tokea mwanzo waeleze tatizo lao ni maslahi siyo kila mara kugeuka kama vinyonga; walianza na interns na sasa maslahi bora. Pia wanashinikiza masuala yaliyo nje ya uwezo wao: KUMTAKA BLANDINA, DR. DEO NA DR. NKYA WATUMULIWE! hata siku moja serikali iliyopewa dhamana na watz kwa kura nyingi haiwezi kufuata matakwa ya kila kundi ndani ya jamii
 
Nchi haina madaktari hata 2000 lakini kuwahufumia imekuwa ugomvi!
hii nchi haina huruma kabisa......ukienda huko mahospitalini ki ukweli hawa watu wanafanya kazi katika mazingira magumu sana.....wako kwenye risk kubwa ya kuambukizwa magonjwa.....
Lakini serikali hii haioni hilo...katokea mwanamama mmoja katoa lake la moyoni..huu si uungwana kabisa
 
Nchi haina madaktari hata 2000 lakini kuwahufumia imekuwa ugomvi!

Mbona kuna mahali nilisoma kuwa Maintern waliofukuzwa Muhimbili ni zaidi ya 1900. Sasa kama wanaweza kuwa intern wote hao ambao ni miaka miwili tu inakuwaje kwa miaka 50 ya uhuru bado tuna madaktari 2000 tu???
 
Kuna watu tumesoma wote chuo kimoja,kada moja na kuhitimu mwaka mmoja,tumeajiriwa mwaka moja nakupangwa vituo vya kazi tofauti Ukerewe,Missungwi nk.ajabu tunalipwa mishahara tofauti kwa asilimia 43, nyie acheni hii wizara ina mambo....
 
Kuna watu tumesoma wote chuo kimoja,kada moja na kuhitimu mwaka mmoja,tumeajiriwa mwaka moja nakupangwa vituo vya kazi tofauti Ukerewe,Missungwi nk.ajabu tunalipwa mishahara tofauti kwa asilimia 43, nyie acheni hii wizara ina mambo....
aiseee.....labda mkuu ulipata sup nyingi.....

bongo bana....
 
Back
Top Bottom