Huduma zinatolewa...lakini si kama kawaida. katika kila kitengo kwatika hospitali hizo wameachwa madaktari wachache kuhudumia wagonjwa wa dharura (emergency)...clinic zote leo zimefungwa Temeke, Amana, Ilala, na Muhimbili ( pamoja na MOI na Ocean Road). Kwa kifupi mgomo umeanza japo taratibu lakini mpaka kesho huduma nyingi zitakuwa zimefreeze.
Kama unadhani utani nenda sasa hivi pale Don Bosco uone kuna madaktari wangapi wapo pale kwa mkutano tangu asubuhi, na huko mikoani leo jioni hii wanaitisha vikao, tayari Bugando, Mount Meru, Mbeya Referral na Mbeya Regional wameshaconfirm kufanya vikao jioni hii kujiunga na mgomo...hali itakuwa mbaya siku chache zijazo.

@NDYOKO kama unafuatila historia madaktari tumefanya hivi mara kadahaa 95 Meghji akajiururu,2005 H.mwinyi alitufuata uumbini saa tano ya usiku na mishahara ikapandishwa kwa cdre zote za serikali ukianzia na afya cha muhimu tunaomba sapoti yenu ndugu zetu kwani at the end madai yetu nimadai ya watumishii wa umma na mwishowe ni heri kwa mwananchi wa kawaida
Nipo Regency hospital Madaktari wa kumwaga
Huyu Blandina Nyoni sijui yukoje, na pengine najiuliza kwa nini wanawake wakishika madaraka ya juu huwa na kiburi sana?
Siyo sahihi kugoma kutibu wagonjwa kisa madai. Binadamu yoyote anaunga mkono daktari kugoma kutibu mgonjwa kisa madai hana tofauti na gaidi. Ni muuaji huyo. Hivi ni wafanyakazi wangapi wanafanyakazi bila posho? Daktari analipwa Tsh. 700000(laki saba) na posho ya asilimia 10, wakati huo huo kuna mtu analipwa Tsh. elfu themanini(80,000/=) na wote wanahitaji kula, wanasomesha n.k. Hakika unyeti wa kazi zao madaktari mimi hainishawishi niunge mkono watende dhambi ya kuua. Maana huo ni unyama. Hivi jeshi letu likisema linagoma patatosha kweli? au wao wana mishahara mikubwa kuliko Madaktari? au Jeshi siyo nyeti kuliko daktari?. Sasa wakitaka walipwe posho nyingi si ni wazi kwamba hawatapata hata wagonjwa wa kutibu kwa vile tayari watakuwa wameshakufa kwa njaa baada ya fedha zote kuelekezwa kwao? Najua wengi watasuta mtazamo wangu ila kweli utabaki pale pale kwamba hawa Madaktari wanagoma siyo kwamba hawaridhiki na kile wanacholipwa , bali ni kiburi tu cha kutaka kuonesha kwamba wao ndiyo wameshikilia uhai wetu na kwa maana hiyo wanaweza kufanya wapendavyo. Hii kwa mujibu maandiko ya vitabu vitakatibu ni kiburi, majivuno na kwa maana hiyo Shetani ameshatawala mioyo yao. Watanzania tuzidi kuomba shetani asichukue nafasi yake.MADAKTARI wametangaza rasmi kuanza mgomo katika hospitali zote za rufaa na vituo mbalimbali vya afya nchini kote hadi hapo madai yao yatakaposhughulikiwa na Serikali. Pia wamepitisha azimio la kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuifumua na kuiunda upya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao Waziri Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya kutokana na kile wanachodai kuwa ni kudhalilisha taaluma yao.
Dk Uliomboka pia aliwataja Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa kwamba wanapaswa kuwajibishwa na Rais. Akitangaza mgomo huo, Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Jumuiya ya Madaktari hao, Dk Stephene Ulimboka alisema hatua hiyo inalenga kupata ufumbuzi wa madai waliyotoa kwa muda mrefu na kuongeza kwamba, leo wanatarajia kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Dk Ulimboka alitaja baadhi ya madai yao kuwa ni kuwawekea mazingira bora ya kazi madaktari kwa kupeleka vifaa vya kazi hospitalini na kwenye vituo vya afya, kuboresha malipo ya posho na kuwapatia sitahili zote wanataalamu hao. Hata hivyo, tafauti na ilivyokuwa awali, kikao cha jana ambacho kilikuwa cha majumuisho, kilitumika pia kupokea ripoti ya mikutano iliyokuwa ikiongozwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na kupokea majukumu ya kuongoza harakati hizo.
Kuanzia leo tunatangaza kuwa madaktari wote wanaoguswa na hili kote nchini kuacha kufanya kazi hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yetu, tunataka Serikali iboreshe mazingira ya kutolea huduma za afya, ili kumwezesha daktari kumpatia huduma mgonjwa katika kiwango kinachostahili, alisema Dk Ulimboka.
Alitaja madai mengine matatu ambayo kamati anayoiongoza inasimamia kuhakikisha yanatekelezwa kuwa ni pamoja na madaktari kurejeshewa nyumba za kuishi kama inavyoelekezwa kwenye Standard order ya Serikali, ambayo inasema daktari atapatiwa nyumba ya kuishi na Serikali na kama sivyo atapatiwa asimilia 30 ya mshahara.
Alisema kipengele hicho kiliondolewa kinyemela bila wao kushirikisha wala kuelezwa sababu za kuondolewa kwake, jambo linalowaongezea ugumu wa maisha na kuwafanya wadharaulike. Madai mengine yalihusu nyongeza za mishahara, ambayo alisema kumekuwa na ugumu wa kutekeleza suala hilo kila mara hadi wanapofanya mgomo.
Mwaka 2005 wakati tunaanza kazi, mshahara wa daktari ulikuwa unafikia Sh124, 000, lakini baada ya mgomo ndipo ukapandishwa hadi kufikia karibu ya laki 700,000 sisi tunataka suala hili lirekebishwe na nyongeza yake isisubiri shinikizo, alisema.
Madai mengine ni malipo kwa madaktari pindi wanapofanya kazi katika mazingira hatarishi na kupendekeza walipwe asimilia 30 ya mshahara wao, posho wakati wa kazi ya ziada ambayo kwa sasa wanalipwa asimilia 10 ya mshahara wao. Kuhusu mshahara, alisema yapo mapendekezo ambayo alisema wataitaarifu Serikali watakapokutana na viongozi wake.Madaktari hao leo wanatarajia kuendelea na mkutano wao katika ukumbi wa Don Bosco.
Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi alisema alikabidhi majukumu kwa kamati iliyoundwa na wanachama baada ya kuonekana kuwa hadi sasa Serikali imekuwa ikiwazungusha. Wanachama wamesema hapo mlipofikia tunashukuru mmejitahidi vya kutosha na sasa tunaomba mtukabidhi majukumu ili shughuli hii iweze kusimamiwa na kamati ya madaktari, alisema Dk Mkopi.
Hatua hiyo imelenga kuongeza wigo wa washiriki ambao watawahusisha madaktari wasio wanachama wa MAT na wafanyakazi wengine katika sekta hiyo ya afya.
Mwananchi
Mbona kuna mahali nilisoma kuwa Maintern waliofukuzwa Muhimbili ni zaidi ya 1900. Sasa kama wanaweza kuwa intern wote hao ambao ni miaka miwili tu inakuwaje kwa miaka 50 ya uhuru bado tuna madaktari 2000 tu???
Afadhali umeliona hilo. Tunafanya ushabiki hata kwenye uhai wa watu. Hata kama Serikali ingekuwa na makosa kiasi gani mimi sisubutu kuunga mkono na kushabikia mgomo wa madaktari. Lipi la muhimu kwanza, Maslahi ya Daktari au uhai wa wagonjwa?.hebu wekeni facts basi, tusiwe tunapiga gumzo la sokoni, we need facts here, so that, information can reliable.
Afadhali umeliona hilo. Tunafanya ushabiki hata kwenye uhai wa watu. Hata kama Serikali ingekuwa na makosa kiasi gani mimi sisubutu kuunga mkono na kushabikia mgomo wa madaktari. Lipi la muhimu kwanza, Maslahi ya Daktari au uhai wa wagonjwa?.

Ninawashangaa sana wanaosuport huu mgomo...hawajui what is going to happen to them in the next few minutes, assume unapata ajali, unafikishwa MOI unakuta hamna huduma...sijui utamlaumu nani!!
Chamuhimu ni madaktari wakae na wahusika(serikali) wasolve matatizo yao. Naamini wataafikiana.