Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

wakati wakifikiri wanafaidi sana kwa katiba hiyo, wanasahau kwamba madaraka ni kitu cha muda tu, lakini mabadiliko na maendeleo wanayoyachelewesha yana madhara kwa jamii nzima including wao wenyewe, watoto wao na vizazi vyao kwa ujumla. Nchii hii ikiwa maskini, wote sisi tunaathirika, vita ikitokea tunaathirika wote hata kama utakuwa na uwezo wakuhamia nchi nyingine, lakinmi kumbuka home is home, mkataa kwao ni mtumwa.

Kubadlli inahitaji special task force kwa pande zote, upinzani, taasisi za kijamii, na wananchi kwa ujumla, kila atakayepata pa kuongea aongelee hilo kwa nguvu zake zote. Katiba hii inawafaidisha wao kuweza kubaki madarakani. Nothing else.
 
Katiba mpya ndio mkombozi wa kweli tukiunganisha nguvu inawezekana manake kila mtanzania mzalendo anaunga vita hii ya katiba mpya. Nawasihi tuungunishe nguvu kuwasha moto wa katiba mpya tunayo support kubwa.
 
Okay, kwa wale ambao walikuwa wameniomba ni generate 'Hardy Copy' ya petition, tayari nimefanya hivyo. So if you wish to hep us collect more signatures from the people who don't have access to a computer at home, we kindly ask you to download the attached file/PDF to your computer (print it/make as many copies as you wish), collect the signatures, and then email it back to us for collation.

P.S. Our online petition is still active (so please continue to promote it): TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition

With thanks,

KatibaMpya.org
 
Katiba mpya,katiba mpya...wimbo mpya upendezao masikioni....kwani ikiwa mpya ndo inakuwa bora au nzuri?..katiba mpya iletwayo na chama cha zamani, tena kilicholeta uhuru miaka 49 iliyopita si lolote si chochote..lets think bigger kama kauli mbiu ya JF ilivyo..tusubiri, narudia tena great thinkers tusubiri

Tumepokonywa ajenda na tujipange namna ya kuirudisha

mungu ibariki katiba mpya
 
WAJITOLEE WATU KUANDIKA RASIMU THEN TUPELEKE KWA MWANAHALISI, RAIA MWEMA, MAJIRA, MWANANCHI NA THE GUARDIAN ON SUNDAY

Kwanza nikupeni shime wewe na waandaji wengine kuliona hili la katiba mpya kama high priority, lakini pia niwape shime kwa kusimama mstari sahihi manake wana habari wengine ama hawajui ama ni wanafiki -wameshindwa kujua kwamba media ni mhimili wa nne baada ya bunge, mahakama na executives(serikali). Mawazo
1. Serikali lazima itambua kuwa KATIBA MPYA ni lazima kwa sasa kuepusha uvungifu wa AMANI
2. Katiba ya sasa ni kandamizi kwa mfano inatoa fursa TUME YA UCHAGUZI kuteua rais wa nchi ama kwa kupenda au kushinikizwa manake ikitangaza hakuna chombo chochote kinaweza kuhoji
3. Katiba ya sasa ipo kimfumo wa chama kimoja kwamba Rais anweza kuamua mambo mengi bila kuhojiwa mfano idadi ya mawaziri na wizara
4. Katiba ya sasa inaruhusu mbunge kuwa waziri hivi mbuinge kama waziri alawahudumaia vipi wananchi wake au ndio kusema atatumia uwaziri wake kufuja mali ya umma kwa ajili ya jimbo?
5. Katiba ya sasa imeweka nyasifa ambazo tunaona hazina tija kwa manufaa ya nchi -mfano mkuu wa wilaya na mkurugenzi, naibu waziri na kaitibu wa wizara, huu ni ufujaji wa mali na rasilimali za umma.
6. Katiba ya sasa inakandamiza haki ya kuwa na mgombea binafsi huu ni ukandamizaji why???
7. Katiba ya sasa inamruhusu RAIS kuteua wakuu wa tume ya uchaguzi -huu ni uzandiki na usultani -ibadilike
8. Katiba ya sasa inavitaka mamulaka kama PCCB kumutumia rais kama atakavyo-inaripot kwa rais -kwanini PCCB isiwajibike kwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, hii ni pamoja na CAG
9. KATIBA ya sasa inaruhusu viti maalumu huu ni uzandiki na ufujaji wa mali ya umma, wanamwakilisha nani??????
10. Katiba ya haitoi uhuru wa principles of separation of powers, waziri mkuu na mawaziri wanatokana na bunge na ni wabunge? watawala wengi wako juu ya sheria mahakama haipo huru -huu ni uzandiki katiba hii haitufai.

ninayo mengi lakini la mwisho tunamwomba RAIS ampangie kazi nyingine Celina Kombani ameonesha toka mwanzo hawezi kuongoza wizara hii, ni mchapa kazi lakini hapa amechemesha hawezi kuanza kazi kwa matusi kwa kauli yake ya kibabe na kinafiki. Ninaomba usome mawzo yangu tafadhari usichakachue manake itakuwa hakuna maana ya kuanzisha maada hii halafu uchakachue michango yetu -please tunaimani una dhamira ya kweli kwa Tanzania. Yangu maskio hiyo Kesho.-STAR TV
 
WanaJF, I think we're making some progress here... [Read this Editorial piece from "The Guardian on Sunday". It pretty much covered all items that we have already outlined in our petition (much thanks to the Editor!!):
New Constitution, cry of a Nation

By Editor

12th December 2010

Just after the General Elections many voices of prominent people as well as ordinary Tanzanians have been raised against the current Constitution, calling it a time barred document that serves the interests of the ruling party at the expense of 43 million plus citizens of this country.
These voices demand an overhaul of the current Constitution, by drafting a new one, others seeking a re-write, while still a few, mostly on the Government side, are comfortable with allowing patches where amendments, in what they claim to match with time, can safely do and carry the nation going, and smoothly.
The 1977 Constitution has been amended severally, actually 14 times to be exact while the 15th amendment is in the offing, an indication that all is not too well. It is undeniably a product of colonial inheritance, that by itself is enough to set the stage for a new draft, albeit five decades after independence although it could not mean detaching from colonialism.
As the basic or fundamental Law of the Land, the Mother of all Laws, our Constitution is outdated, not comfortably matching the current political environment.
Already people are not too happy with the nomination of Cabinet Ministers from elected Members of Parliament, there are opinions that Regional Commissioners should directly be voted in by the electorate in the respective regions and the loud cry from various sections of the country and community wanting Independent or Private Candidates.
It has been clearly in the open that people want the powers of the President to be reduced, as well as petitioning in a Court of law the Presidential Election results. There are still opinions widely ranging from having an independent Electoral Commission whose head should not be appointed by the President, every region to have its own Attorney-General while the post of District Commissioners be abolished constitutionally and development directors work responsibly in their place.
The list of changes in the Constitution is endless and there is great public demand on this. For is it news anymore that opposing opinion on the size of the Ministries has been heard? That the Constitution goes open on that the size of ministries, and subsequently that of Cabinet Ministers?
Not only that. Why is the Constitution silent on the number of Regions, Districts or Constituencies? Or the President should not have the mandate to increase or decrease the size of the Cabinet?
The list of what should be in the Constitution becomes all the more endless. There are those who believe that Members of Parliament should not be permitted by the Constitution to make personal gains such as arranging their emoluments; that all politicians should pay income taxes as the case is to all other ordinary citizens.
The Elections Act, for example, is allowed silently by the Constitution about announcing results not officially at the voting stations but by the Commission itself, which allows room for doctoring results, and so more and more. There are also opinions that a president should garner more than 50 percent of the votes cast to be legitimate.
We at The Guardian on Sunday strongly believe that it was high time the government responded to these voices by initiating a thorough process to re-write a new Constitution that will serves all Tanzanians.
We can't continue to have a flawed and time barred constitution that doesn't accommodate the major economic, social and political changes this country has gone through during the past 49 years.
GUARDIAN ON SUNDAY

P.S. Please continue to sign/promote our online petition:TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition
With Thanks,
KatibaMpya.org




 
JAMBO WANA JAMII WAPENDA NCHI YAO!!!

Swala hili lina nguvu na la msingi kabisa kwa wakati huu!
Kweli wakipatikana watu kama hao Jaji Waryuba , Generali Ulimwengu hata mama Mwakitwange ni wazuri, midahalo ipewe muda mrefu watu waulize maswali na habari za kina zilizoenda shule za Ulimwengu zielimishe umma, swala kubwa ni kuelimisha jamii na katiba mpya iundwe, pia naomba izungumzwe kifungu kwa kifung ili ieleweke iliyopo mapungufu ni yepi ili tukitengeneza katiba mpya tuangaliwe kwa muda mrefu ujao sio tutengeneze ya kufaa kwa miaka 5 au 10 itakayotugalimu kutengeneza tena mpya!!

Watanzania tunamshukureu Baba wa Taifa pamoja na wengine kumwona hakufanya kitu ila mimi nasema ndiye pekee ambaye alikuwa anaona mbele alijua umuhimu wa kusomesha watanganyika waelimike ili wapate utalamu wakuweza kutumia maliasili za nchi zao baada ya kuiva barabara!! wenye uchu waliona kachelewa!! baba wa Taifa huyo huyo hotuba zake ndio dira pekee inayotuongoza kwa sasa ( kwa wale tu ma -crical thinkers, wanao weza kutafakari hotuba zake kama Dr. Slaa na kuweza kuzitumia. any way lengo langu katika mjadala huu ni kuunga mkono asilimia mia kuwa mdahalo kuhusu katiba mpya ni muhimu na ni muda mwafaka!!

Watanzania wenye nia njema na mapenzi na nchi yao watakiunga mkono na kujumika kwa asilimia mia kutengeneza katiba mpya!! tunaelewa waliopo madarakani kaitba inawanufaisha ndio maana wanachelea kukubali haraka, matokeo yake waazusha vituko vipya mara udini mara chokochoko katika vyama mdradi tu tusielewane, jamani tuongee kwa ajili ya kutengeneza nchi yetu, au mnaona raha ukabaila na ubepari unavyokuja kwa kasi sasa hivi????

Nijaribu kuchokoza pia jambo moja kuhusu muungano wetu wa Tananyika + Zanzibar = Tanzania, leo hii kuna nchi ya Zanzibari maana wana Rais wao na na Tanzinia ina Rais wa Jamhuri ya Muungano,mbona Tanganyika haina Rais wake??? kweli Mch. Mtikila lile kundi lililokuwa likidai Tanganyika naona umuhimu wake!!! hivyo basi katika kutengeneza katiba hebu na hili nalo tuliangalie kwa undani zaidi!
msema kweli na mpenda haki, J. Nyanda
 
Yes!
Tuko pamoja,
Now it's the right time!

let us forget our different parties au itikadi za kidini or what ever! Katiba ndio mwongozo eti!

tume huru isiyoongozwa na chama chochote hasa inayoegemea upande mmoja haifai!!!

Watanzania tuamke, tunaipenda nchi yetu, hebu basi tuitengenezee mwelekeo mzuri tusije tukasutwa na watoto, vitukuu vyetu kuwa tulikuwa wapi hadi tena nchi inachukuliwa na wakoloni????? maana huu ndio mwanzo mbinu za kurudisha wageni kwa gia ya uwekezaji ni kero kubwa saana linanisumbua akili yangu hebu wana JF nisaidieni, uchungu na maumivu nayoyasikia nikiona neno "wawekezaji" ni mkali kuliko uchungu niloupata siku ya kujifungua mtoto wangu!! yaani linaniuma kuliko kawaida!! nina uchungu saana na maisha tunayoishi siku hizi. Mtu unakuwa mkweli, mwadilifu unatenda kila aina ya haki inavyopaswa, wengine wanopora mali sio waadilifu wanaishi maisha ya peponi wakati mimi nasota na waya mkali!!! naukataa ukabaila, ubepari na umaskini kwa asilimi 1000!!! Kuna mwanahabari mmoja ambaye nadhani anauchung kama mimi na nchi hii naomba anisamehe kama atachukia kwa jina ni Mr A. Ryoba! ni mmoja kati ya wale ambaohawpendi uuzo unaofanyika nchi hii ni vile tu mtu unakuwa hauko katika nafasi ya kuweza kuingia katika akili za watu ukawabadirisha fikra zao mgando na kuwawekea fikra yakinifu!

Mungu yupo, anasikia vilio vya watu wake! nani ajuaye kuna siku isiyo na jina yote haya yatakuwa hadharani na hapo watu watakapotambua uozo watasema kweli msema kweli na mpenda haki J. Nyanda alilonga!!!

All the best!
 
Hata mimi naungana na wana harakati katika kudai hili kwani mwisho wa siku tutajikuta tuko sehemu ambayao hakuna hata mmoja wetu alitarajia kufika huko. Kama kweli nchi yetu ni huru na ina demokrasia ya kutosha sioni tatizo la kuangalia mapungufu ya katiba yetu ya sasa na kuamua kufanya mabadiliko au marekebisho kwa manufaa ya kila Mtanzania bila kujali wadhifa alionao.
 
Katiba ni document inayoonesha jinsi nchi itakavyotawaliwa, mahusiano kati ya wanaotawala na watawaliwa. Kwa ujumla katiba inatoa ramani ya mfumo wa uendeshaji wa nchi. Kwa nchi kama Tanzania ambao tunafuata mfumo wa kidemokrasia unaoitwa mfumo wa kikatiba. Hata hivyo, kubadili katiba ni jambo moja, na kuona mabadiriko ni jambo jingine. Ni kweli kuwa kubadili katiba ni mwanzo mwema, ila wakati tukifanya hayo tukae tukijua kwa uhakika kabisa kuwa kuleta mabadiriko ndani ya jamii yetu ni zaidi tu ya kubadili katiba.

Katiba hazijitekelezi, katiba zinatekelezwa na watu. Ukiwa na watu kama tulio nao leo katika mfumo wa uongozi, ni wazi mabadiriko ya katiba itakuwa ni rangi tu. Watu tumekuwa tukilalamikia mfumo wa uchaguzi, lakini ni lazima tujiulize, yaliyofanyika kwenye uchaguzi yanaruhusiwa na katiba? Najua wengi tunalalamika kuwa katiba hairuhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani! Hilo ni sawa kabisa. Lakini je kule kwenye ubunge ambako matokeo yake yanapingwa mahakamani haki huwa inatendeka? Uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa taratibu zile tulizo nazo hata kama ni mbovu? Sasa ikiwa taratibu za leo, ambazo tayari zinawapendelea walioko madarakani, hazifuatwi, kwa nini tuamini kuwa tukiweka taratibu nyingine bora zaidi tutaweza kuzifuata?

Tatizo letu kubwa ni uwezo wa watu wanaosimamia mfumo wetu. Tatizo letu ni 'moral na immotional incompetence' ambazo zinaonekana kutuandama watu wengi wa nchi hii kwa hali ya kushangaza mno. Mtu akishapewa uongozi hata uwe wa kikampuni kidogo tu, ubinafsi linakuwa tatizo kubwa. Uongozi ni mbovu na dhaifu karibu kila mahali, na ukiangalia ugonjwa mkubwa ni ubinafsi! Je katiba mpya itatutibu na majeraha haya ya ubinafsi uliopitiliza? Watu hawataitafsiri katiba katika njia ambayo inawainua wao wenyewe wanaoitafsiri na kuwazamisha walio baki? Hapo mie ndo naishiwa nguvu.
 
i think the most important thing ni kuderive mechanism ya kuwapata watu wengi zaidi kusaini petition! tunaomba sasa hata NGO zitende hela na kushiriki in such activities.
 
Mimi nionavyo, upinzani kuhusu katiba mpya inatoka tu kwa watu wachache tu wa CCM na wale wasioweza kutafakari musitakabali wa nchi yetu. Na hawa wachahe katika CCM ni baadhi tu ya wakubwa ambao ni walafi amabao wanapinga mjadala wa Katiba mpya kwa sababu wananufaika nayo kwa gharama ya wananchi ambao Katiba ya sasa inawaziba wananchi wengi kuelewa ni kwa nini maisha yao ni duni hivi na hivyo kuendela kukandamizwa haki zao. Sioni sababu ya kupinga Katiba mpya wengine wanansema haina maslahi kwa CCM. Kinanchoanza yaani msingi siyo wananchi kwa ajili ya Chama bali ni Chama kwa ajili ya wananchi. Yaani ni Chama kwa jaili ya wananchi kwa ajili ya Chama kwa ajili ya wananchi. Katiba Mpya lazima na kama kuna shaka ya kweli yakuonekana kuhusu madai ya katiba mpya katika tafiti zilizopita basi tufanye referendum na ianze mapema mwakani. Wanachi kumekucha, tuamke tuendelee.
 
Wewe kama mwananchi mpenda nchi yako unadhani kwa nini katiba mpya inatakiwa kwa sasa!!
Je ungetaka katiba mpya iweje??wapi unaona kuna mapungufu?
 
Kaka kiiza katiba iliyopo si kwamba Ina
mapungufu yapi tu Bali ni kitu kisichofaa
kwa matumizi kwa sasa sababu imechakaa
haifai imerepewa mpaka hakuna Tena
pakurepea .pili si katiba ya vyama vingi
ni ya chama kimoja haiendani na mfumo
uliopo wa vyama vingi..ndio maana tunataka
mpya.
 
1. Inakandamiza haki ya mgombea binafsi
2. Inatoa fursa ya kuwa na tume ya uchaguzi ya uchakachuaji
3. Inatoa fursa ya watawala kuwanyonya watanzania kwa kuficha mikataba
4. Inatoa fursa kwa rais wa nchi kuwakandamiza watanzania kwa maamuzi yasiyo na mpaka idadi ya wizara, teuzi mabalimbali
5. Inatoa fursa ya matumizi hovyo ya mali ya umma mfano kazi ya naibu waziri na mkuu wa wilaya v. Katibu wa wizara na mkurugenzi wa wilaya
6. Inavunja kanuni ya principle of separation of powers -mbunge anakuwa waziri, watawala wetu wengi wapo juu ya sheria
7. Inatoa fursa ya ufisadi kwa watawala wetu kwa kuzuia hatua yoyote dhidi yao
8. Ilitungwa kwa ajili ya chama kimoja na sasa ni vyama vingi
9. Katiba ya sasa ya tanzania haitambui zanzibar kama nchi
10. Katiba ya sasa inabeba sheria 40 za nyalali alizosema zifutwe
11. Katiba ya sasa inarusu uzandiki mwingi wa kuchakachua
 
mgombea binafsi hatakiwi hata kidogo ni inch gani yenye mgombea binafsi na akapita, au tunataka tuendeshwe kama familia wakati inch?
 
Wewe kama mwananchi mpenda nchi yako unadhani kwa nini katiba mpya inatakiwa kwa sasa!!
Je ungetaka katiba mpya iweje??wapi unaona kuna mapungufu?
kwa mara ya kwanza naona ukiongelea siasa, nimekuzoea kwenye suala la michakachuo ya mambo ya akina dada....
 
Back
Top Bottom