Maelezo binafsi ya mgombea wa CCM jimbo la Igunga Dk. Kafumu

"Tumekua na lundo la maProf kibao achilia mbali huyu Dr" lakin efficiency zao sifuri so hayo ni makaratasi tu kama vipi, Mwalimu atamfundisha kuumba herufi ktk siasa kuko vipi .
 
Katika hali ya kawaida huyu jamaa ilitakiwa awe MAABUSU SASA HIVI. Maana ni miongoni mwa walioliibia taifa, ni mwizi hajaitumia taaluma yake, halafu kikubwa ni yeye aliye fanya wawekezaji wawaue watu wanaokaa karibu na madini. JAMANI WANA IGUNGA HUYO NDO ANAYEUA WATU KWA KUKUBALI UWEKEZAJI WA KIFISADI, NDO ALIYE FANYA TANZANIA ISINUFAIKE NA MADINI. JAMANI NATOA WITO IKIWEZEKANA AWEKEW PINGAMIZI MAANA AKIINGIA BUNGENI NDO ATAKAEKUWA ANAJIBU MASWALI TATA YA WIZI WA MADINI BADALA YA WAZIRI, SI MNAKUMBUKA KABOYONGA ALIYEKUWA WA TABORA MJINI ALIVYOKUWA ANAJIBU MASUALA YA RELI? KAFUMU AHUKUMIWE KWA NAFASI ALIYOKUWA nayo kwenye madini.

Kwanza hela za watanzania alizosomeshwa nazo kashalipa? au hawa ndo wale wale walojipa misamaha na baadae kuanza kuwaandama vija wa leo walipe mikopo ya vyuo vikuu!!!! swine kabisa
 
(vi)Madini ya vito (Almasi, Tanzanite, Ruby na mengineyo) yanachimbwa na Watanzania tu.

Kama mheshimiwa huyu asiposema ukweli wakati huu wa kampeini, je akishakuwa mbunge ataweza kusema ukweli tena? Madai hayo aliyoweka kwenye statement yake hapo juu si kweli kwa sababu Almasi inachimbwa na Petra Diamonds
wakati Tanzanite inachimbwa na AFGEM. Makampuni hayo si ya Watanzania hata kidogo bali ni ya Afrika ya Kusini. Sana sana watanzania waliomdo ndani ya makampuni hayo ni hao viongozi wa serikali waliopewa share kinyemela ili kulinda maslahi ya wenye makampuni.
 
kama mheshimiwa huyu asiposema ukweli wakati huu wa kampeini, je akishakuwa mbunge ataweza kusema ukweli tena? Madai hayo aliyoweka kwenye statement yake hapo juu si kweli kwa sababu almasi inachimbwa na petra diamonds
wakati tanzania inachimbwa na afgem. Makampuni hayo si ya watanzania hata kidogo bali ni ya afrika ya kusini. Sana sana watanzania waliomdo ndani ya makampuni hayo ni hao viongozi wa serikali waliopewa share kinyemela ili kulinda maslahi ya wenye makampuni.

wapiga kura wa igunga wanamkubali dr. Kafumu, kawajengea misikiti, kagawa mipira na kuchangia saccos! Nyie wanamagwanda mmeonekana igunga kipinidi hiki cha uchaguzi mdogo
 
CV nzuri sana, ingawa siku hizi tumegundua CV hazina tija kwawananchi mana kuna maprofesa, wengine tangia ujana wao na sasa wanazeekea mjengoni hakuna wanachofanya, otherwise wananchi wa IGUNGA wataamua nani awaongoze,tusubili

Emmathy, ni kweli kabisa. Unajua viongozi na wananchi kwa ujumla bado tunafikiri kiongozi mzuri ni yule mwenye IQ ya juu wakati si kweli. IQ haitoshi kumpa mtu uongozi, we need someone with EI(emotional intelligence). Kiongozi ambaye ata empathize with the needs of the people, engage people, find creative options for our existing problems etc. In short a person who can resonate with people. Hiki kitu ndio tunakosa kwa viongozi tulionao (ingawa kuna viongozi wetu wengi hata hiyo high IQ yenyewe hawana); nafikiri nasisi labda hatujui tunatakiwa kuangalia nini hasa tunapochagua. Nasema hivi si kum-disqualify Dr Kafumu kwasababu CV haijaniwezesha kujua EI yake ikoje, na pia siwezi kuwa disqualify hao wagombea wengine based on CV info as well. Hivyo basi in reference to Igunga; wananchi wa huko wanatakiwa wawaangalie candidates wao kwa ukaribu zaidi na sio vyeti tu.
Ni wakati sasa umefika wakuangalia EI ya viongozi tunaowachagua i.e. a candidate/person with self awareness (recognize his/her people's feelings/recognize feeling as it happens), self control (kiongozi ambaye ni trustworth, responsible, can handle change, committed, and has high integrity), motivated i.e. willing to initiate, influence and accept (one that is willing to challenge the status quo and not accept everything). Tunahitaji viongozi wetu wawe na ability yaku-persuade, listen, and when necessary send convincing messages. Hii itasaidia kuhakikisha despite our political, religion, culture differences we always work as a team to attain a shared goal.
 
Duh mkuu Kafumu umetishaje, yaani kwa CV hiyo unapata kura kiulainiii kama unanawaaa. Sasa ngoja tuone CV ya mgombea wa MAGWANDA, yaani haifiki hata robo ya ukurasa.

Hivi wewe Mwita mbona hakuna hata siku moja ukaongea point hata moja walau nikusifie. Duh, nani kakuambia CV ni kigezo cha ubora kwenye ubunge? Au ndo masaburi yako yalikushauri. Napata kichefu chefu kila ninapoona thread yako **** yako
 
mkubwa naomba nikuulize maswali mawili yenye vipengele a na b;
1.umesaidiaje nchi yako katika mikataba feki
a)inakuaje mnapeleka nje ya nchi mchanga na kuacha mashimo?
b)kwanini hadi sasa hivi madini hayachangii asilimia kubwa katika bajeti ya taifa huku mkihamisha watu bila kulipwa?
2.cv yako tumeiona.je ahadi zako ni zipi?
a)nini dhamila yako katika kupambana na ufisadi ukianza na rostam aziz?
b)cv ya uongozi tanu itatusidiaje kwenye vyama vingi na mchango wako ni upi uliotoa dhidi ya maalbino?.mia
 
Duh mkuu Kafumu umetishaje, yaani kwa CV hiyo unapata kura kiulainiii kama unanawaaa. Sasa ngoja tuone CV ya mgombea wa MAGWANDA, yaani haifiki hata robo ya ukurasa.
mkuu Mwita25, kazi yako hata ningeambiwa nitalipwa mamilioni ya shilingi siwezi kuifanya itanidharirisha na kuniondolea utu wangu.
 
mkuu Mwita25, kazi yako hata ningeambiwa nitalipwa mamilioni ya shilingi siwezi kuifanya itanidhririsha na kuniondolea utu wangu.
Ukishakubali kazi hiyo ni rahisi hata kuingiliwa kinyume na maumbile na wanaume wenzako kwa ahadi ya pesa na gari. Binadamu kamili hawezi kuwa na bei.
 
Huu ni wasifu wa Dr Kafumu. Hapo kwenye red panatia shaka kwa mustakabali wa wana Igunga ambao sio waislamu


JINA: Dk. Dalaly Peter Kafumu
KUZALIWA: Agosti 4, 1957
MAHALI: Kijiji cha Itumba, Tarafa ya Igunga Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
NDOA: Nina mke na watoto watano ambao kati yao watatu ni Madaktari wa binadamu, wengine wawili bado wanasomea Udaktari wa Binadamu na mmoja anasoma Stashahada ya Ufamasia.


ELIMU:

*Shahada ya kwanza ya Madini- BSc (Geology)-1983
*Stashahada ya Elimu-PGD (Education)-1987
*Shahada ya Uzamili ya Madini-BSc (Geology)-1995
*Stashahada ya Utafutaji Madini-PGD (Mineral Exploration)-1991
* Sahahada ya Uzamivu ya Madini-Ph.D (Geology)-2000


UZOEFU CCM
*Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa TANU (TYL) tawi la Itumba (1971-1972)
*Mjumbe wa Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu ya Tawi la CCM, Madini (1983-1992).
*Mjumbe wa Mkutno Mkuu wa Wilaya na mkoa wa Dodoma (1983-1992).
*Katibu wa Tawi la CCM, Madini Dodoma (1988-2011).
*Kada wa CCM (1988-2011).


UTUMISHI WA UMMA
*Kamishna wa Madini Tanzania (2006-2011)
*Mkuu wa Mawasiliano Wizara ya Nishati na Mdini (2004-2006)
*Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji na Takwimu Wizara ya Nishati na Madini (2002-2004).
*Mtaalam Mwandamizi wa Madini (1993-2002)
*Mhadhiri Chuo cha Mdini Dodoma (1978-1992)
*Mtaalam wa Madini Wizara ya Nishati na Madini (1983-1987).

TAALUMA
*Mtaalam Bingwa wa Madini Nchini.
*Mwanachama wa Chama Cha Wataalam wa Madini Tanzania na Afrika.
*Mjumbe wa (II)) Bodi za Usajili wa Makandarasi (II) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

MCHANGO KWA TAIFA
*Mtaalam wa Madini (1983-1987)
Nilishiriki kwenye utafutaji wa madini na kugundua machimbo mengi ambayo sasa yanachimbwa na kuleta mapato, ajira na kukuza uchumi wa taifa.
*Mhadhiri wa Chuo cha Madini (1987-1992)
Nilifundisha mafundi sanifu katika fani ya madini, zaidi ya wahitimu 1,000 wanalitumikia taifa katika nafasi nyingi serikalini na kwenye sekta ya madini nchini.
*Mhadhiri wa Nje wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (2004-2006)
Nilifundisha masuala ya Jiolojia ya Mazingira na kuhitimisha wanafunzi zaidi ya 500 ambao sasa wanalitumikia taifa na katika sekta mbalimbali nchini.
*Kamishna wa Madini (2006-2011)

Nimesimamia marekebisho ya sheria ya Madini ya mwaka 1998 ili kupata sheria ya mwaka 2010. Sheria mpya inahakikisha kwamba:-
(i) Serikali na Wananchi wanashiriki zaidi katika uwekezaji madini kwa kupata hisa kwenye migodi.
(ii) Wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya migodi wanafidiwa vizuri, kujengewa makazi mazuri na kushiriki kwenye mradi husika.
(iii) Kampuni kulipa kodi na mrahaba kwa viwango vya juu zaidi.
(iv) Wachimbaji wadogo wanatengewa maeneo yao, kupewa leseni zenye muda mrefu ili waweze kupata mitaji kutoka kwenye taasisi za fedha;na
(v) Viwanda vya uongezaji thamani ya madini vinajengwa hapa nchini ili kuongeza ajira na kukuza uchuni; na
(vi)Madini ya vito (Almasi, Tanzanite, Ruby na mengineyo) yanachimbwa na Watanzania tu.


MCHANGO KWA IGUNGA
*Kamishna wa Madini (2006-2011)
(i) Nilisaidia wachimbaji wadogo nchi nzima kupata maeneo na viwanja kwa ajili ya uchimbaji madini.
Kwenye Wilaya ya Igunga nimewasaidia wachimbaji wadogo wa madini kuwapa leseni maeneo ya Bulangamilwa na Nanga.
(ii) Kuwapatia soko la dhahabu mjini Nzega na Dar es Salaam wachimbaji wadogo wa dhahabu wa wilaya ya Igunga.
(iii) Kuwashauri wachimbaji wadogo nchini na Igunga kuhusu umuhimu wa kufuata sheria na kanuni za madini ili wasidanganywe na watu wanaotumia sekta ya madini kutapeli na kuwaibia.
(v)Ofisi yangu kama Kamishna wa Madini ilikuwa wazi kwa wana Igunga wote kufika na kuopata ushauri, maelekezo na msaada waliohitaji.


HUDUMA KWA JAMII (2005-2011)
(i) Kujenga Misikiti miwili katika Kata ya Itumga, kutoa vitabu vya rejea na kiada kwa shule kumi za sekondari wilaya ya Igunga:- Itimba, Igunga, Mwamashimba, Mwisi,Mwanzugi, Igurubi, Manshiku, Simbo na Nanga.
(ii) Kufadhili vikundi vya kina mama, Kata ya Itumba, Kwaya za Madhehebu ya Kikristo Igunga mjini na Mwanzugi.
(iii) Nikiwa mwanachama wa Igunga SACCOS nimekisaidia chama changu kwa ushauri wa kitaalam na kutoa ada na hisa na michango yangu kwa wakati.
(v) Nikiwa mlezi wa Vijana Kata za Mwamashimba na Itumba nilifadhili vifaa vya michezo (mipira, jezi na kombe) na kuendesha ligi ya mpira wa miguu katika kata hizo mwaka 2009-2010.
(vi) Nilitoa mchango wa sh. 800,000 kuchangia ujenzi wa visima virefu viwili Kata ya Itumbi.

HUDUMA KWA UMMA WA TANZANIA
*NikiwaMjumbe wa Bodi ya Makandarasi (2006-2011) nimesimamia kuandikisha makandarasi nchini wanaotoa huduma za ujenzi kwenye sekta ya barabara na majengo na nikiwa mjumbe wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (2009-2011) nilishiriki katika usimamizi wa chuo hicho ili kutoa viajana wasomi bora wa kulitumikia Taifa la Tanzania.



Mimi Dr kafumu naomba unisaidie kumention shule/ vyuo ulivyosomea kwani kuandika shahada, stashahada, mara uzamili bila kusema ulisomea wapi hiyo sio CV labda ni story kuhusu wewe. Lingine pengine mimi sifahamu uzuri kati ya advance diploma na post graduate diploma zote kwa kiswahili tunaziita Stashahada?
 
Wakuu hebu tuangalie yafuatayo

1.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa TANU (TYL) tawi la Itumba (1971-1972)
Dr. Kafumu amezaliwa in 1957, sasa ina maana wakati huu alikuwa na miaka 14 mpaka 15. Very likely alikuwa form1 au form2 (Kwa enzi hizi anweza pia kuwa alikuwa darasa la pili hahaha ahahah), Would that be possible kwamba alikuwa mwenyekiti au amechomekea hili akijua hakuna mahali kuna kumbukumbu.

2.
*Mtaalam wa Madini (1983-1987)
Nilishiriki kwenye utafutaji wa madini na kugundua machimbo mengi ambayo sasa yanachimbwa na kuleta mapato, ajira na kukuza uchumi wa taifa.

This is too general and too vague for a Dr., Why can't he be specific kwa kuyataja hayo machimbo na kuzungumza ushirikiwake ulikuwa vipi???? Kwa kuikoleza zaidi angetaja baadhi ya vijana wa Igunga waliopata hizo ajira as a result ya yeye " kushiriki kwenye utafutaji wa madini na kugundua machimbo mengi"
 
Wakuu hebu tuangalie yafuatayo

1.
Dr. Kafumu amezaliwa in 1957, sasa ina maana wakati huu alikuwa na miaka 14 mpaka 15. Very likely alikuwa form1 au form2 (Kwa enzi hizi anweza pia kuwa alikuwa darasa la pili hahaha ahahah), Would that be possible kwamba alikuwa mwenyekiti au amechomekea hili akijua hakuna mahali kuna kumbukumbu.

2.

This is too general and too vague for a Dr., Why can't he be specific kwa kuyataja hayo machimbo na kuzungumza ushirikiwake ulikuwa vipi???? Kwa kuikoleza zaidi angetaja baadhi ya vijana wa Igunga waliopata hizo ajira as a result ya yeye " kushiriki kwenye utafutaji wa madini na kugundua machimbo mengi"


Naona kama jamaa huyu pia ni mbabaishaji kisiasa japo ana madigrii mengi.
 
Naona kama jamaa huyu pia ni mbabaishaji kisiasa japo ana madigrii mengi.

Tatizo kubwa naloliona CCM ni wao kutofahamu aidha makusudi au kwa bahati mbaya kwamba mambo yanabadilika very fast. Ndiyo maana JK pamoja na kwamba hii nni 2011 bado anataka kutawala kinyerere nyerere au kama Mwinyi na akikosolewa anashangaa!!! Sasa ukianagalia hii CV ya Kafumu inafanafanana na ile ya JK 2005.
 
Inabidi ni changie juu ya hili, kwa taarifa yenu igunga Dr kafumu anakubalika saaaana tena sana, mtasema mengi but ukweli ndo huo na hata chadema wanajua hilo, mtaishia kunawa igunga!! Huwa mnadai Cv za watu leo hii yamewashinda hamtaki tena,, duh kweli watanzania tunaelekea kubaya!! Let's wait and see!! Nawakilisha!
<br />
<br />
mkuu unatakiwa ku-declare interest kabla hujamwaga mataputapu yako.....
 
wewe ni mmojawapo ya washauri kuhusu masuala ya mikataba mibovu ya madini inayowanyonya na kuwaumiza Watanzania, sasa kweli unajisifu kwa utumbo uliowafanyai watanzania, shame upon you. hustahili kuwa hata balozi wa kaya 10. wewe ni mtaalamu ambaye umelishwa unga wa ndere na viongoz wako wa CCM hubadiliki hata kidogo. Wanaigunga mkimpa huyu jamaa ubunge mmeliwa tena mmeliwa haswa, bora mpigie jiwe kura lakini si huyu jamaa
 
Kafumu ni bonge la opportunist hana huruma na Nchi .Kama unabisha unadhani wa maana basi ngojea kampeni zianze utasikia .Madini yana shida kubwa Nchini akiwa ni mmoja wa walio shiriki ujinga mwingi .Jamaa ni msiri na hana mpango wa kuiendeleza Taifa I know him personally nina yajua mengi yake only matter of time nitayamwaga hapa .

Kama kuna watu wa msaada ndani wa Magamba basi wako ma Prof wa kumwaga huko akiwemo maji marefu lakini leo Tanzania iko wapi ? Haina umeme , Maji safi , barabara, huduma bora hosp ,mawasiliano adimu nk migogoro nchi nzima nk hao wako huko zaidi ya Kafumu .

Pole sana Mwita Maranya .

Mkuu Lunyungu hapo mwisho naona umechanganya madesa.

Mwita Maranya ni mtu makini sana hafungamani na siasa za magamba,labda kama ulimkusudia mtumwa wa Nape anayemwaga pumba hapa JF kila leo.
 
Hili ni gamba lingine, kwa nini sekta ya madini haiongozi kwa mchango wa kodi ni kwa sababu ya haya magamba, including kafumu.
 
Namshauri aendelee kua mhadhiri nadhani atafaa sana hata pale udom atakua msaada sana kuliko kukimbilia siasa chafu za kimagamba na kuishia kustaafu kwa aibu
 
Back
Top Bottom