Maelezo binafsi ya mgombea wa CCM jimbo la Igunga Dk. Kafumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maelezo binafsi ya mgombea wa CCM jimbo la Igunga Dk. Kafumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Sep 3, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Huu ni wasifu wa Dr Kafumu. Hapo kwenye red panatia shaka kwa mustakabali wa wana Igunga ambao sio waislamu


  JINA: Dk. Dalaly Peter Kafumu
  KUZALIWA: Agosti 4, 1957
  MAHALI: Kijiji cha Itumba, Tarafa ya Igunga Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
  NDOA: Nina mke na watoto watano ambao kati yao watatu ni Madaktari wa binadamu, wengine wawili bado wanasomea Udaktari wa Binadamu na mmoja anasoma Stashahada ya Ufamasia.


  ELIMU:

  *Shahada ya kwanza ya Madini- BSc (Geology)-1983
  *Stashahada ya Elimu-PGD (Education)-1987
  *Shahada ya Uzamili ya Madini-BSc (Geology)-1995
  *Stashahada ya Utafutaji Madini-PGD (Mineral Exploration)-1991
  * Sahahada ya Uzamivu ya Madini-Ph.D (Geology)-2000

  UZOEFU CCM
  *Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa TANU (TYL) tawi la Itumba (1971-1972)
  *Mjumbe wa Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu ya Tawi la CCM, Madini (1983-1992).
  *Mjumbe wa Mkutno Mkuu wa Wilaya na mkoa wa Dodoma (1983-1992).
  *Katibu wa Tawi la CCM, Madini Dodoma (1988-2011).
  *Kada wa CCM (1988-2011).


  UTUMISHI WA UMMA
  *Kamishna wa Madini Tanzania (2006-2011)
  *Mkuu wa Mawasiliano Wizara ya Nishati na Mdini (2004-2006)
  *Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji na Takwimu Wizara ya Nishati na Madini (2002-2004).
  *Mtaalam Mwandamizi wa Madini (1993-2002)
  *Mhadhiri Chuo cha Mdini Dodoma (1978-1992)
  *Mtaalam wa Madini Wizara ya Nishati na Madini (1983-1987).

  TAALUMA
  *Mtaalam Bingwa wa Madini Nchini.
  *Mwanachama wa Chama Cha Wataalam wa Madini Tanzania na Afrika.
  *Mjumbe wa (II)) Bodi za Usajili wa Makandarasi (II) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

  MCHANGO KWA TAIFA
  *Mtaalam wa Madini (1983-1987)
  Nilishiriki kwenye utafutaji wa madini na kugundua machimbo mengi ambayo sasa yanachimbwa na kuleta mapato, ajira na kukuza uchumi wa taifa.
  *Mhadhiri wa Chuo cha Madini (1987-1992)
  Nilifundisha mafundi sanifu katika fani ya madini, zaidi ya wahitimu 1,000 wanalitumikia taifa katika nafasi nyingi serikalini na kwenye sekta ya madini nchini.
  *Mhadhiri wa Nje wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (2004-2006)
  Nilifundisha masuala ya Jiolojia ya Mazingira na kuhitimisha wanafunzi zaidi ya 500 ambao sasa wanalitumikia taifa na katika sekta mbalimbali nchini.
  *Kamishna wa Madini (2006-2011)

  Nimesimamia marekebisho ya sheria ya Madini ya mwaka 1998 ili kupata sheria ya mwaka 2010. Sheria mpya inahakikisha kwamba:-
  (i) Serikali na Wananchi wanashiriki zaidi katika uwekezaji madini kwa kupata hisa kwenye migodi.
  (ii) Wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya migodi wanafidiwa vizuri, kujengewa makazi mazuri na kushiriki kwenye mradi husika.
  (iii) Kampuni kulipa kodi na mrahaba kwa viwango vya juu zaidi.
  (iv) Wachimbaji wadogo wanatengewa maeneo yao, kupewa leseni zenye muda mrefu ili waweze kupata mitaji kutoka kwenye taasisi za fedha;na
  (v) Viwanda vya uongezaji thamani ya madini vinajengwa hapa nchini ili kuongeza ajira na kukuza uchuni; na
  (vi)Madini ya vito (Almasi, Tanzanite, Ruby na mengineyo) yanachimbwa na Watanzania tu.


  MCHANGO KWA IGUNGA
  *Kamishna wa Madini (2006-2011)
  (i) Nilisaidia wachimbaji wadogo nchi nzima kupata maeneo na viwanja kwa ajili ya uchimbaji madini.
  Kwenye Wilaya ya Igunga nimewasaidia wachimbaji wadogo wa madini kuwapa leseni maeneo ya Bulangamilwa na Nanga.
  (ii) Kuwapatia soko la dhahabu mjini Nzega na Dar es Salaam wachimbaji wadogo wa dhahabu wa wilaya ya Igunga.
  (iii) Kuwashauri wachimbaji wadogo nchini na Igunga kuhusu umuhimu wa kufuata sheria na kanuni za madini ili wasidanganywe na watu wanaotumia sekta ya madini kutapeli na kuwaibia.
  (v)Ofisi yangu kama Kamishna wa Madini ilikuwa wazi kwa wana Igunga wote kufika na kuopata ushauri, maelekezo na msaada waliohitaji.


  HUDUMA KWA JAMII (2005-2011)
  (i) Kujenga Misikiti miwili katika Kata ya Itumga, kutoa vitabu vya rejea na kiada kwa shule kumi za sekondari wilaya ya Igunga:- Itimba, Igunga, Mwamashimba, Mwisi,Mwanzugi, Igurubi, Manshiku, Simbo na Nanga.
  (ii) Kufadhili vikundi vya kina mama, Kata ya Itumba, Kwaya za Madhehebu ya Kikristo Igunga mjini na Mwanzugi.
  (iii) Nikiwa mwanachama wa Igunga SACCOS nimekisaidia chama changu kwa ushauri wa kitaalam na kutoa ada na hisa na michango yangu kwa wakati.
  (v) Nikiwa mlezi wa Vijana Kata za Mwamashimba na Itumba nilifadhili vifaa vya michezo (mipira, jezi na kombe) na kuendesha ligi ya mpira wa miguu katika kata hizo mwaka 2009-2010.
  (vi) Nilitoa mchango wa sh. 800,000 kuchangia ujenzi wa visima virefu viwili Kata ya Itumbi.

  HUDUMA KWA UMMA WA TANZANIA
  *NikiwaMjumbe wa Bodi ya Makandarasi (2006-2011) nimesimamia kuandikisha makandarasi nchini wanaotoa huduma za ujenzi kwenye sekta ya barabara na majengo na nikiwa mjumbe wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (2009-2011) nilishiriki katika usimamizi wa chuo hicho ili kutoa viajana wasomi bora wa kulitumikia Taifa la Tanzania.
   
 2. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hata hayo ma cv hayasaidii mkienda bungeni 2 mnaanza kuota magamba
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kamishna wa madini????ajira gani ametoa kwa wachimbaji wadogo??aseme hivi "NIMEWASAIDIA WACHIMBAJI WAKUBWA KWA KUWEKA MGAWANYO TOFAUTI AMBAPO WAGEN WANABEBA MADINI MENGI NA TAIFA HALIPAT KITU"
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Duh mkuu Kafumu umetishaje, yaani kwa CV hiyo unapata kura kiulainiii kama unanawaaa. Sasa ngoja tuone CV ya mgombea wa MAGWANDA, yaani haifiki hata robo ya ukurasa.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwenye taaluma kaandika: 'Mtaalam Bingwa wa Madini'

  Hivi kuna mtu anaweza kunieleza ni viwango/vigezo gani vinatumika kusema 'huyu ni bingwa'? Who decides who is bingwa? What is bingwa? Ni uzoefu wa muda mrefu? au una mapembe?

  Nimewahi kusikia watu wakisema mwandishi aliyebobea, najiuliza kubobea ni nini? na nani anatakiwa afanye evalaution ili kujua kama mtu kabobea?
  au unasikia daktari bingwa! really? daktari bingwa anakuwaje? na daktari ambaye sio bingwa anakuwaje? Au kwenye vyeti vyao kumeandikwa nini hasa?
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  I am very sad that he has decided to abandon all of his professional carrier and jump into a dirty game a.k.a politics ..... he has been walking on a clear and clean path and now he has decided to step on shit

  Wish him all the best
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Tukizungumzia urefu na ukubwa wa cv za wanamagamb hiyo sio issue kabisa na ndivyo mlivyo kwamba mna uwezo mkubwa sana wa kuandika.

  Tatizo tulilonalo na magamba ni output ya hayo macv ni zero! Kama magamba mnathubutu kufanya ufisadi wa elimu mtashindwa nini kujaza kurasa mia za cv ya magamba mmoja.
   
 8. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu wabunge wa CCM wanaongoza kwa ma CV uchwara , tatizo wakifika 2 bungeni wanatumia masaburi kufikiria
   
 9. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Siku zote huwa napenda kuona wabunge wakiwa ni watu makini, maana kosa moja linaweza kuligharimu taifa kama tulivyoona kwenye issue ya madini ingawa imenisikitisha kuwa kumbe hata hayu hawezi kukwepa lawama.

  Hoja yangu ianzie kwenye idadi ya watoto alionao. Ukiangalia kwenye highlights zangu juu, amesema ana watoto 5 lakini ukijumlisha mchanganuo alioutoa unaleta watotot 6, Sasa je tuamini lipi? Je huyu ni mtu makini kweli?

  Upande wa elimu anasema hivi *Shahada ya Uzamili ya Madini-BSc (Geology)-1995
  Inaelekea huyu mkubwa hajui kuwa kuna tofauti kati ya shahada ya uzamili (Msc) na Bachelor of Science (Bsc) Sasa sijui hapo alimaanaisha kuwa ni Bachelor au Masters maana maelezo ni Masters lakini abbreviation ni Bachelor. Je huyu ni mtu makini kweli?
  Anyway wana Igunga ndo wataamua kama wanataka mbunge makini au ili mradi mbunge
   
 10. m

  mukama talemwa Senior Member

  #10
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Dk Kafumu kama suala la shule yuko juu ila wasiwasi wangu nikwanini jitihada zake za kusaidia wana Igunga zimeanza pindi alipofikilia kuwa mbunge?Yaani kuazia 2006 kwanini akufanya hivyo kabla ya hapo,suala la shule na uadilifu na kusaidia wananchi ni vitu viwili tofauti.
   
 11. L

  LAT JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu ... daktari bingwa ni yule ambaye ameweza ku perform a special case (ambayo ni peculiar compared to anyone) either ya tiba au upasuaji kwa kutumia utaalamu wake wa udaktari
   
 12. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Acha kudanganya watu wewe. Tunahitaji wasomi kama hawa kwenye siasa ili kusaidia kuharakisha maendeleo.
   
 13. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  We unafikiri kaandika mwenyewe! jopo la magamba ndiyo wamemwandikia hiyo....tena usikute imetokea ikulu
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  LAT, hapo ndio napata shida. Kwani si alisomea ku-perform hiyo special case? Sio kila mtu anasomea kila kitu, ila ukiwa na profession fulani ina maana unao ujuzi wa kufanya hicho ulichosomea. Hivi nilitegemea aitwe daktari wa 'whatever' lakini hivi vikirombwezo naona uma-chinoo!

  Na hapa Tanzania tuna tunauguwa huu ugonjwa wa kuremba qualifications mno. Can you believe Dr Benson Bana wanasema (TBC1) kuwa amebobea kwenye mambo ya siasa? Benson Bana!
   
 15. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo unataka kusema wamedanganya?
   
 16. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,139
  Likes Received: 7,391
  Trophy Points: 280
  Kiufupi jamaa amebobea kwenye madini,
  Katika sekta ambazo haziwanufaishi kabisa wananchi nii hii ya madini,
  Kama kuna wasiofahamu ukweli ni kua asilimia kubwa ya mgao tulionao unachangiwa na makampuni ya madini ambayo hayatunufaishi kwa mrahaba wala mrabaha wowote.
  Makampuni haya yanatumia megawati kibao tu kwenye shughuli zao za kila siku.
  Sasa kama tuna watu kama hawa ambao wanajiita wataalamu halafu hatunufaiki nao ni wazi kua wanapiga porojo tu maofisini, zaidi kuwaza political opportunity ili wainufaishe tu.
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kama CV ina-matter basi Prof Lipumba leo hii angekuwa Rais wa Tanzania, maana 10% ya CV yake ndiyo aliyonayo JK. Kwa kushinda uchaguzi, Kafumu hatashinda ila ubunge atapewa. Hii imezoeleka but sooner or later this corrupt practice will end.
   
 18. A

  August JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  cv ni nzuri nk nk na kuwasaidia watu wa igunga na nzega, lakini mbona ulicho toa kwa jamii au maendeleo ya tz, igunga, nzega nk ni kidogo saaanaaaaa ukilinganisha na ulicho kipotezea nchi in terms ya gharama ya masomo yako, madini kupoteza mabillioni kama sio matrillioni, na wewe ndio mshauri mwenyewe? duh! akili kweli mkichwa, kila mtu anazake
   
 19. L

  LAT JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  ha haa haaaaaa .... duh .... hata siasa nayo ina daktari bingwa?
   
 20. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hawajadanganya, ila wamemrembea kwa kuipaka mafuta ili inoge......hata hivyo magamba hawashindwi kufanya chochote pale wanapotaka
  kitu chao kitimie....unaweza kuta yote yaliyomo kwenye cv hiyo ni 0 tu ndiyo ya kweli na mengine yote ni magumashi
   
Loading...