Tanzania Mining Cadastre Portal ni mfumo wa kuisababishia nchi hasara badala ya faida

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,829
21,461
Mh. Waziri hongera kwa kuteuliwa kuwa waziri wa wizara hii muhimu kwa Taifa hili.

Pamoja na hongera nyingi ila ninaomba kukujulisha kuwa wizara yako imeshindwa kuisimamia Tume ya Madini nchini, kwasababu baada ya kuteuliwa yapo mambo ambayo kwa muda mfupi yameanza kuharibika tena kwa haraka na tunakoelekea hali sio shwari hata kidogo.

Mfano:
1. Mfumo unaosimamiwa na Tume ya madini “Tanzania Mining Cadastre Portal” umebadilisha kutoka mfumo wa zamani na kuwa mfumo mpya. Mfumo huu mpya serikali imeufanya kwa zaidi ya Trilion moja fedha za kitanzania.

Mfumo huu haufunguki, hauna nguvu wa speed bali upo kwa ajili ya kutumia internet bure.

Hasara ya mtandao huo kutokufanya kazi ni kukosekana kwa ukusanyaji wa mapato ya serikali kupitia madini.

2. Wafanyakazi wa Tume ya Madini kulipwa mishahara ya bure nchi nzima kwani wakiwa ofisini na field ndio mfumo unaowasaidiwa kufanya kazi.

3. Mfumo huo umefungwa na tume ya madini bila kufanyiwa utafiti na kutoa elimu kwa wadau wa madini na wachimbaji wadogo namna ya kuutumia japo umetumia trilion of money ila utakuwa faida ya wachache iwapo mfumo huu ukifanya kazi japo kwa sasa haufanyi kazi.

3. Waziri nikukumbushe kuwa masoko yaliyoanzishwa na Hayati Magufuli na Mh. Doto biteko ya kuuzia madini sasa hayafanyi kazi tena na utoroshaji wa madini ni mkubwa kupita kiasi.

4. Mwisho nikushauri kuwa usipofanya mabadiliko ya kiuongozi kuanzia Tume ya madini makao makuu hadi ngazi ya mikoa na wilaya, utadumu wizara hiyo kwa muda mfupi kuliko mawaziri waliotangulia na utalisababishia Taifa hasara kubwa.

Hili nalo nendeni mkalitizame.
 
Back
Top Bottom