Madikteta wote duniani hufanana

Madikteta wote duniani hufanana

Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.

b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.

c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!

d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!

e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi).

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?

2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)

3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.

4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)
Mwanakijiji hapa sipunguzi neno, hii ilikuwa 2011, miaka michache baadae, yaani leo, yajayo yatafurahisha zaidi
 
Sifa yao ingine ni kwamba huhakikisha watu wote wenye uwezo hawapati nafasi katika fursa za uongozi wowote wala kupata kazi ya maana. Wakishindwa kabisa kuwakwamisha, huwafunga na/au kuwaua!
Daah mtu ukiwa nje ya mfumo wa ccm akili hufanya kazi yake sawasawa, lakini ukiingia tu ndani ya mfumo huo akili lazima ukabidhi kwa mwenyekiti wa chama
 
Anatafuta pa kuficha uso 'but the die is cast'. Watu ni wachumia tumbo tu.
 
Uko sahihi
Sifa yao ingine ni kwamba huhakikisha watu wote wenye uwezo hawapati nafasi katika fursa za uongozi wowote wala kupata kazi ya maana. Wakishindwa kabisa kuwakwamisha, huwafunga na/au kuwaua!
 
Vicious cirle
Inaonekana watu hawashindwi kuwatambua madikteta; Kitila umesema point moja muhimu sana. Madikteta wanahofia sana intellectuals vile vile. Lakini upande mwingine kundi la wasomi hujitengeneza kama watetezi wa madikteta hao.
 
Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.

b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.

c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!

d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!

e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi).

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?

2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)

3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.

4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)
Hii mada kuna nyakati ilipaswa ifufuliwe sijui kwanini ilijificha
 
Samia and her crew don’t have what it takes, if you watch the series on how to be a tyrant.

Hawa ni wapuuzi wanaotumia mamlaka ya katiba vibaya, na watafanya mabaya zaidi kama hawatozuiwa.

Hata dictators wana mikakati, Samia na genge lake ni mataahira tu with unlimited powers kutokana na tamaduni za nchi ambazo zilizopo kwenye katiba.

Tamaduni ambazo h azikufikiria powers wanazogawa raisi akiwa kiazi itakuwaje

Ndio tatizo letu, vinginevyo yeye na genge lake hawana akili ya kuongoza kama despots. Ni mataahira tu na watu wachache wenye tamaa za mali kwenye vyombo vya ulinzi waliotufikisha hapa.

Na wengi zaidi wanaona madhara ya madaraka ya raisi.

Huyo mama na genge lake hawatoboi, kuna watu wengi sana wenye hasira ambao hawajajipanga bado kuondoa huu upuuzi.
 
Tanganyika sasa iko katika himaya hiyo chini ya nyang'au mmoja ambaye anaamini kila neno lake ni amri na litekelezwe.
 
Back
Top Bottom