Madhara ya uvutaji wa sigara ktk ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madhara ya uvutaji wa sigara ktk ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 5, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,095
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Uvutaji wa sigara katika ndoa:
  Wake au waume wa wanandoa ambao wanavuta sigara wamekuwa na wakati mgumu sana katika hisia zao hasa kutokana na tabia ya kuvuta sigara kwa hao partners wao.
  Hisia huweza kuwa ni za hofu, mashaka na kujisikia kutothaminiwa au kuwa disappointed na hata kuumizwa na hiyo tabia.

  Wapo partners ambao hutafsiri kwamba kitendo cha kutoacha kuvuta sigara ni kuonesha kutojali afya yake mvutaji na familia kwa ujumla yaani mke, mume na watoto.

  Anyway, kila mvutaji hupenda kuacha kuvuta sigara hata hivyo hamu na uhitaji wa kuvuta sigara huwa mkubwa zaidi kuliko makali ya kifo hii ina maana mvuta sigara akiwa na hamu ya sigara huwa ladhi kukubali kuvuta sigara kuliko kutovuta kwa kuogopa kifo.

  Ukishajiingiza kwenye kuvuta sigara na kuwa addicted na nicotine iliyomo utakuwa ladhi kukubali kifo kuliko kuacha kuvuta.

  Wakati mnaoana ulimuahidi partner wako kwamba utampenda, utamheshimu na zaidi mtasaidiana kuhakikisha ndoa yako inalindwa kiroho na kimwili na njia mojawapo ya kutimiza ahadi zako ni kuacha kuvuta sigara.

  Pia kama unataka kujifunza kuvuta sigara achana kabisa na hiyo tabia maana kuanza ni rahisi lakini kuacha ni ngumu mno.

  Kumbuka
  Wavuta sigara huwa na magonjwa mengi kuliko wasiovuta.
  Wavuta sigara huishi muda mfupi kuliko wasiovuta.
  Nchi zingine kama unavuta sigara; Health Insurance huwa kubwa zaidi kuliko wasiovuta.
  Magari au nyumba za wavuta sigara (ambao huvuta ndani ya gari au nyumba) kuuza ni ngumu sana kwani watu hukatishwa tamaa na harufu ya sigara.

  Ukivuta sigara kwa zaidi ya miaka 30 unaweza kuwa umekula pesa yenye thamani ya zaidi ya TSh. millioni 200.

  Sources
  http://www.quitsmoking.com/info/articles/costofsmoking.htm
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ahh basi avute KAYA ...lakin asivute sigara au siyo...

  ahh kuvuta sigara akumfany mtu asiwe renspnble na famili yake..cz wote wwasiokuwa rensponble si km wanavuta sigara..

  ni tabia tu ya mtu..
  PI DID SI KILA KITU UNACHOKIBANDIKA APA KUTOKA UKO UNAKOCHUKUA KINA MASHIKO NA MAUKWELI ASILIMIA 100

  kwenye i post ya sigara ukweli upo lakin pa kusema akivuta sgara anakuwa si wa kucare famil ake apana...cz wapo teeeeeeele sigara avut na familia yake inamshinda/aiangalii
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Je wee pdidy unakunywa pombe?
   
Loading...