Madereva wa Alteza, Subaru na Cruser V8 wakikutana na huu mkeka wa Zambia... Lazma tairi lichomoke

Mkuu hivi ile ya dom-arusha via kondoa ilishakamilika? Kumbe mie bwege huwa nazungukia singida-katesh-babati!
Ile IPO tayari alafu ni mkeka balaa. Mimi nilitoka dom SAA kumi alfajiri na probox, nikaingia SAA NNE asubuhi Arusha.
Imagine ningekuwa na mark x, au BMW. Daadeq.
 
Hizo ndio umeona gari zenye spidi zaidi hapa bongo? Asilimia 90 ya hizo ulizotaja spidi yake mwisho 180km/h ambayo ni ya kawaida sana, cruising speed!! Barabara za lami zilizonyooka vizuri zaidi ya hiyo uliyoona wewe zipo karibu kila mkoa Tanzania..Ukiwa na gari nzuri BMW, Mercedes, Audi, Range etc unawezakimbia hata 250km/h au zaidi..
Bongo kuna mkeka gani? Hizi zenye bampa kila baada ya mita mia na matuta? Na torch kila mahali
 
Mkuu hivi ile ya dom-arusha via kondoa ilishakamilika? Kumbe mie bwege huwa nazungukia singida-katesh-babati!
Imekamilika mkuu ni barabara nzuri ila kuwa makini ina kona za hatari, Dom- Babati km 248
 
Tanzania hatuna highway yenye double roads.Mleta hoja anamaanisha kukanyaga accelerator bila kuhofia kukutana na gari mbele yako.Hizi za Tanzania ukifika mbezi kama unaenda mikoani unaingia kwenye danger zone
 
Hizo ndio umeona gari zenye spidi zaidi hapa bongo? Asilimia 90 ya hizo ulizotaja spidi yake mwisho 180km/h ambayo ni ya kawaida sana, cruising speed!! Barabara za lami zilizonyooka vizuri zaidi ya hiyo uliyoona wewe zipo karibu kila mkoa Tanzania..Ukiwa na gari nzuri BMW, Mercedes, Audi, Range etc unawezakimbia hata 250km/h au zaidi..
two way traffic zilizonyooka zipo karibu kila kona ya tanzania?
 
26169917_321609668326909_4192658413194107432_n.jpg
Kwa mkeka huu halafu eti unakuta tule tu alama twa 50.......
Wallah watanipiga faini deilee
 
Hizo ndio umeona gari zenye spidi zaidi hapa bongo? Asilimia 90 ya hizo ulizotaja spidi yake mwisho 180km/h ambayo ni ya kawaida sana, cruising speed!! Barabara za lami zilizonyooka vizuri zaidi ya hiyo uliyoona wewe zipo karibu kila mkoa Tanzania..Ukiwa na gari nzuri BMW, Mercedes, Audi, Range etc unawezakimbia hata 250km/h au zaidi..
Acha kufanganya malori yamejaa barabarani na speed bump kibao labda kama unatoka Bahi kwenda Manyoni huwa kuna mnyooko mzuri lakini overtaking muhimu
 
Back
Top Bottom