Mademu wakimya mnakera mnoo

Mademu wakimya mnakera mnoo

Muulize "kwanini Punda anatoa mlio kila baada ya saa moja?" Nakuhakikishia mtapiga story siku nzima.

Watu wakimya wanapenda mental challenges sababu maisha yao yako kichwani zaidi kuliko mdomoni, kumtoa kichwani mwambie kitu ambacho kichwa chake hakiwezi kutatua.

Mfanooo
 
ukiongea ni balaa. ukinyamaza ni balaa. macho mkubwa ni balaa .macho mdogo ni balaa. maskio mkubwa ni balaa maskio madogo ni balaa. unahela ni balaa huna hela ni balaa .majameni mnataka nn.????

 
Aaah aaah aaah hongera boss umelamba cha maana hapo
Habari za majukumu wakuu?

Kiukweli mademu wakimya sana wana boa mno.. Una kuta demu mzurii kabisa na elimu yake lakini yupo kama bubu hawezi hata kuchangia maada yoyote katika vikao vya ukoo au familia. Yaani kila kitu mpaka mwanaume aseme, yeye ni kusikiliza tu yaani hachangii chochote mpaka kero..
Back to the main point..

Yaani huyu demu wangu nafikiri ndo rais wa mademu wakimya duniani, nisipo msemesha mimi jua siku hiyo nzima hata ongea.
Mashemeji zake na mawifi zake wote wanamuogopa yaani baada ya salamu tu hana time nao tena.
Mi huwa naongea nae kwa kumuuliza vi maswali vya hapa na pale ndo wakati anajibu hapo ndo tunapiga story hivo.. Sasa inafika wakati na mimi maswali ya kumuuliza yanaisha tunabaki tunatazamana tu.

Tuna miaka mitatu kwenye mahusiano ila yupo vile vile tu.. Nilipo jaribu kumuuliza kuhusu ukimya wake akasema ndivo alivo tuNi mtu anae penda sana kujifunza vitu vingi, akimaliza kazi zake anaenda kwenye tv kufatilia BBC na CNN news pia ni shabiki mzurii wa mpira wa miguu anaweza taja hata kikosi kizima cha buyern munchen..

Watu wanamuogopa mnoo hata wageni hawaji siku akiwepo home.. Yaani hata ushoboke vipi hana time na wewe.Ni mzurii sana wa sura na umbo na elimu nzuri anayo shida ipo hapo kwenye ukimya ulio pitiliza..Alafu yupo emotional sana, yaani nikimtia mkwara kidogo tu atashinda analia siku hiyo..
Kweli "too much of any thing is harmful"

Simaanishi napenda mademu wanaoongea kama chiriku.. Kila
kitu kiwe cha wastani

Location: dodoma
 
Nadhani wengine wanakuwa na matatizo ya kisaikolojia tokea utotoni mwao, inawezekana kabisa wazazi/mzazi walichangia kwa kiasi huyo binti kuwa hivyo. Wengine ni kwasababu wazazi walikuwa wanamchunga sana na viboko na kukaripia mara kwa mara. Mtoto atakuwa kama unavyotaka sawa atakuwa successful kwenye masomo lakini anajenga uoga na kutojiamini kwa kiasi kikubwa sana na ndio maana ukimpiga mkwala unamuumiza sana maana huwa anakumbuka mateso matusi aliyokumbana nayo alipokuwa mtoto, wengine waliwahi kubakwa na wazazi wao na kuwatishia Maisha, kwa style hio hio ya Question and Answer unaweza kujifunza mengi toka kwake, ukianza na wewe kuelezea past zako ulipokuwa mtoto na shida ulizopitia naamini na yeye anaweza kufunguka.
 
Mkuu una moyo.. Mimi nilikua na wa namna hiyo ila miezi 6 nikanawa mikono...

Mtu hacheki, akicheka anaonesha tuu meno ya mbele au utasikia 'mmh' hapo kamaliza.. Wageni wakija kama sipo hua hawakai, kwa wageni ana sentensi zake tatu 'karibuni sana' 'niwahudumie nini' na 'karibu tena' hapo kamaliza,ataendelea na shughuli zake..

Unaweza toka nae Dar hadi Kigoma akakuongelesha sentensi tatu tuu.. Nikawa naenda nae kwenye vibanda umiza kuangalia nae mpira ili kumchangamsha wapi, kwenye vijiwe vya drafti wapi, nunua kila aina ya muvi za vichekesho ila hola!

Nikamkazia siku tatu sianzishi mazungumzo namtegea yeye aanzishe nikaishia kunuka mdomo tuu.. Kuuliza ndugu zake kuhusu huo ukimya wake, wananiambia tangu amekua na mimi kabadilika sana anachangamka tofauti na huko nyuma, eboooh!!

Mwisho wa siku nikaona hii ni special case, nikanyoosha mikono juu...
 
Yaan acha tu Mi nakutanaga pia na waongeaji wenzangu tunaweza kesha tunaongea usiku kucha
Ohoooooo hahahahahhahahaha ha hiyo kali...

Ila Pia Kuna wanaume wanaongea jamani kushinda wanawake loool
 
Bila sh
joanah huyu huyu au kuna mwingine?

Asee mkuu tunaogolea bahari 1..mi wangu hua nakaaga kimya alafu nikikaa kimya utamsikia "una shida gani hubby" mi namjibu "sina shida nimeamua tu kukuigia kua mkimya" anazuga anacheka..ukimkazia uko kimya vile vile Mnuno unafata na madeko..Yani naboeka sema ndo hivyo sina jinsi..Huyu wangu yeye ukitaka aongeee Simu yake ikose game...yani ni anapenda kucheza game huyooo.

Sema namshukuru MUNGU kwa kila jambo..niki miss makelele najua pakuyapata
Bila Shaka ni game la tample run mkuu
 
Back
Top Bottom