Habari za majukumu wakuu?
Kiukweli mademu wakimya sana wana boa mno.. Una kuta demu mzurii kabisa na elimu yake lakini yupo kama bubu hawezi hata kuchangia maada yoyote katika vikao vya ukoo au familia. Yaani kila kitu mpaka mwanaume aseme, yeye ni kusikiliza tu yaani hachangii chochote mpaka kero..
Back to the main point..
Yaani huyu demu wangu nafikiri ndo rais wa mademu wakimya duniani, nisipo msemesha mimi jua siku hiyo nzima hata ongea.
Mashemeji zake na mawifi zake wote wanamuogopa yaani baada ya salamu tu hana time nao tena.
Mi huwa naongea nae kwa kumuuliza vi maswali vya hapa na pale ndo wakati anajibu hapo ndo tunapiga story hivo.. Sasa inafika wakati na mimi maswali ya kumuuliza yanaisha tunabaki tunatazamana tu..
Tuna miaka mitatu kwenye mahusiano ila yupo vile vile tu.. Nilipo jaribu kumuuliza kuhusu ukimya wake akasema ndivo alivo tu..
Ni mtu anae penda sana kujifunza vitu vingi, akimaliza kazi zake anaenda kwenye tv kufatilia BBC na CNN news pia ni shabiki mzurii wa mpira wa miguu anaweza taja hata kikosi kizima cha buyern munchen..
Watu wanamuogopa mnoo hata wageni hawaji siku akiwepo home.. Yaani hata ushoboke vipi hana time na wewe..
Ni mzurii sana wa sura na umbo na elimu nzuri anayo shida ipo hapo kwenye ukimya ulio pitiliza..
Alafu yupo emotional sana, yaani nikimtia mkwara kidogo tu atashinda analia siku hiyo..
Kweli "too much of any thing is harmful"
Simaanishi napenda mademu wanaoongea kama chiriku.. Kila
kitu kiwe cha wastani
Location: dodoma