Mademu wakimya mnakera mnoo

Mademu wakimya mnakera mnoo

Mkuu una moyo.. Mimi nilikua na wa namna hiyo ila miezi 6 nikanawa mikono...

Mtu hacheki, akicheka anaonesha tuu meno ya mbele au utasikia 'mmh' hapo kamaliza.. Wageni wakija kama sipo hua hawakai, kwa wageni ana sentensi zake tatu 'karibuni sana' 'niwahudumie nini' na 'karibu tena' hapo kamaliza,ataendelea na shughuli zake..

Unaweza toka nae Dar hadi Kigoma akakuongelesha sentensi tatu tuu.. Nikawa naenda nae kwenye vibanda umiza kuangalia nae mpira ili kumchangamsha wapi, kwenye vijiwe vya drafti wapi, nunua kila aina ya muvi za vichekesho ila hola!

Nikamkazia siku tatu sianzishi mazungumzo namtegea yeye aanzishe nikaishia kunuka mdomo tuu.. Kuuliza ndugu zake kuhusu huo ukimya wake, wananiambia tangu amekua na mimi kabadilika sana anachangamka tofauti na huko nyuma, eboooh!!

Mwisho wa siku nikaona hii ni special case, nikanyoosha mikono juu...
ayaaaa!!! mkuu nipe number yake
 
Maisha yangu yote naoembea nije kupata msichana Kama huyo,
Tutakua tunaongea swali kwa jibu, swali kwa jibu, nyumba nzima ni ububu.


Mkuu umeitupa bahati, ngoja upate anayeongea Kama kameza CD, alafu utagundua kuwa hadi masikio huwa yanahitaji muda wa kupumzika.
 
Ikiwepo hekima meneno huchujwa sana na huchagua la kuongea, namwona ana hekima kuzidi hongera kwa hilo rafiki
 
Ndugu zangu wanamuona ni mtu mwenye kiburi sana
kwni ameolewa na ndugu zako au wewe ndo umemuona ukimpenda, ukamthamini, ukamjali na kumchukulia alivyo inatosha sio lazima kila mtu amfurahie kwani ata angekuwa anawachangamkia ni bado wangemsemaaa. Inaonekana na ww pia unamchoka kwa hilo kwani hukuliona kuanzia mwanzo?
 
Back
Top Bottom